Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Naunga mkono hoja. Nadhani nafasi hizi ingependeza kama zingekuwa zinaombwa na watu wanafanyiwa usaili kwenye panel na TBC ccm inaonesha wazi kama Kenya.

Nafasi hizi zinahitaji mtu mwenye uzoefu na utumishi wa umma, lazima awe na utaalamu wa uhasibu au uchumi na pia usimamizi wa biashara.

Hakuna vitu vinarudisha nyuma utendaji serikalini kama kuteua makada wa ccm. Wengi wao vilaza na wanawaza kujinufaisha hawana uwajibikaji. Katiba mpya tungependa nafasi hizi ziombwe live on national tv interview. Mtu akianza ze chama ze ilani wananchi tunajua dafu hili japo kada lakini kichwani halina kitu linatoswa instantly.
 
Hii nchi jamani kweli kuna haya mambo ya kuzaliwa kwenye silver spoon hapo.

Kuna mteuliwa UDE namfahamu tokea amalize chuo ajira yake ya kwanza ni kuteuliwa uded.

Magufuli alifanya hivyo kwenye uteuzi wa Ma DAS naona mama kamuiga au kahujumiwa.

Mama embu angalia vizuri CV za hao wateule wako.

Nyingine zitakuwa zimebumbwa embu zifuatilie usibitishe ukweli
 
Nadhani wamaanisha kuwa DEDs hawa wawe sawa na maofisa watendaji wakuu CEO au?

Katiba mpya haiwezi kupatikana ila marekebisho ya katiba iliyopo.

Hata hivyo Tanzania ina uhaba mkubwa wa watu wenye sifa za kuwa CEO.

Ila kwa hawa DEDs ni lazima serikali itengeneze kitu chaitwa Municipal Charter au Council Charter yaani mkataba rasmi ambao ni lazima DEDs wasaini mbali na kula viapo.

Ufanisi wa utendaji wake wa kazi utatokana na kuzingatiwa mambo yaliyomo kwenye mkataba.
 
Hivi kweli hako kadada Form four kwetu kwa wakulima wa mpunga Kwetu Malinyi kweli tumepata hasara sura ya kitoto kweli jamani anyway macho yangu Basi kari
Hivi kweli hako katoto Kataweza hapa Malinyi kwenye mpunga wetu labda ,,, Basi karibu tyu tujipatie mke maana inaonekana hujaolewa Bint na suala inafaa kuwa mke wa maonesho,, Lakini hako ka Joanfaith hakawezi kupaisha Uchumi wetu wa Malinyi anyway nisiandike mwishowe nikakosea
 
ni vema kujifunza..
Ila km hujawai kufanya kazi hata kuwa mkuu wa kitengo au idara aombe Mungu.
Wazoefu Wanaweza kukuyumbisha akajikut anaingiza halmashauri kwenye migogoro.
Pili inawavunja moyo watu waliotumikia kwa umakini na unyenyekevu nafasi zao na wana vigezo vya uteuzi ila hawateuliwi wakikata tamaa utaumiz wengi.hawatakuwa na moyo wa kujitoa km awali
Watu wengi tunaangalia tulipoanguka siotulipojikwaa; mfano watu wengi wapo lazy..Ila hatuangalii.kwa nn wapo lazy..
Ni Sawa na kumlaumu kwa nn baba hakumpeleka mama hospital kwa tax au bodaboda katumia baiskeli au daladala wakati hiyo baiskeli tu ya kufika hospital kaiazima Ili asevu pesa ya matibabu ya mama kutokana a mavuno haba aliyoyapata msimu ulopita na hajawai kukulalamiia japo unajua na ww mtt umefanikiwa Umeanza matanuzi na maamuzi ya kujijenga ww kwanza ukiamini muda Upo utawakumbuka.
 
Mama anawakomoa mataga na sukuma gang!
.
Alisikika mamwia toka ufipa
 
Bora wangeteuliwa hata maafisa elimu kata kwenye digiri na uzoefu wanao.Hao watoto hata kuwa maafisa utumishi hawajawahi Fanya.Hii ni dharau sana
 
Ulichoandika uko sahihi tena bora wapya damu moto majority walioko serikalini husubiria mishahara na posho basi ubinifu zero, inabidi serikali ije na system nzuri ya kumonitor miradi ya maendeleo na ufanisi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma, bila hvo umaskini kuisha Tanzania haitakwisha wala
 
Saizi upigaji utakuwa mkubwa kwa sababu Hawa madada hawajawahi kufanya Kazi zozote za Halmashauri hawajui taratibu yaani watakuwa bypassed Sana japo watazoea baada ya kama mwaka hivi,sijui kwenye vikao vya madiwani na RCC watakuwa wanajieleza vipi
Hata huo upigaji ni vile serikali inaruhusu kwanini wasiweke mifumo inayozuia huo upigaji na hyo mianya yote huko serikalini?
Wenzetu wamewezaje kuzuia hyo Hali na sisi kwanini tushindwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…