Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Naona pisi kali zimehamia pande za halmashauri, wenye nyavu zao jamani......naona vijana wajasiriamali wa kupaka rangi kucha, kope na nyusi za kichina, wigi, na makorokoro mengine wakienda kula shavu pande hizo.
 
Mataga utataga
Tuliishawaambia ccm sio chama cha siasa,hamuelewi.

Sijui huwa mnatuona wambea au wazushi!!!!wewe unemwona mtu kavaa tishirt la kijani anapiga makelele na ujinga wako unadhani kakosa kazi kweli kweli mpaka kaamua afanye hiyo!

Chiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Toka 2010
Kiutaratibu ilikua wanapandisha vyeo kwa aliyekua Muhasibu wa halmashauri (DT)/Mchumi wa halmashauri/Afisa mipango wa halmashauri/Afisa utumishi wa halmashauri (DHRO) au mwanasheria wa halmashauri

Ila toka 2015 tukaanza kudemka
 
Kwanza kwa nini DED awe ccm??? Hawa wanatakiwa kuwa Watumishi wa serikali!! Uzoefu wa kutosha unatakiwa mpaka mtu iwe Mkurugenzi. Kama Mkuu alitaka wajifunze basi angewaweka maassistants!

Ila hii tabia ya kutuambia kuwa mfanyakazi wa serikali asiwe na chama na hapo hapo unawanyima promotion kwa kuleta makada wa ccm kuwapa nafasi ambazo wao walistahili, na watakaofundishwa na hawa walionyimwa promotion to those positions ni kuwadhalilisha hawa senior staff na kuua kabisa motivation yao ya Kazi!!
 
Kiutaratibu ilikua wanapandisha vyeo kwa aliyekua Muhasibu wa halmashauri (DT)/Mchumi wa halmashauri/Afisa mipango wa halmashauri/Afisa utumishi wa halmashauri (DHRO) au mwanasheria wa halmashauri

Ila toka 2015 tukaanza kudemka
Dada_huyu_ameteuliwa_kuwa_Mkurugenzi_wa_Halmashauri_ya_Wilaya_ya_Kigoma._Katiba_yetu_inampa_ma...jpg
 
Try to be constructive katika hoja yako.

Ni kwa vipi utumishi wa umma wanajisiwa na ni vipi watumishi wa umma wavunjwa moyo?
Nitazungumzia kuvunjwa moyo. Mtumishi wa umma anatakiwa kuwa na uhakika kuwa akitimiza wajibu wake vizuri na kwa weledi ataweza kupanda cheo hadi kufikia uongozi wa juu wa kiutendaji ( ukurugenzi, uafisa tawala wa mkoa au wilaya na ukatibu mkuu).

Na mojawapo wa vipimo vya utumishi wake ni jinsi anavyofuata na kusimamia miongozo ya utumishi wa umma kama waraka wa utumishi wa umma. Mtumishi huyu anapoona nafasi hizo sasa zimekuwa za makada na sio za watu kama yeye ni lazima akate tamaa.

Mbaya zaidi anajikuta anatumia muda mwingi kumuelekeza namna ya kufanya kazi maana anajua mambo yakiharibika ni yeye ndio atawajibika. Aidha, mara nyingi hawa makada wanakuwa wabishi katika kufuata taratibu za utumishi kwa dhana kuwa ni kupoteza wakati. K.m. taratibu za ununuzi zinachukua muda kwa sababu ya checks and balances lakini kwa wale wasiojua wanaona ni ucheleweshaji na ni njia ya kula hela ya serikali.

Kitu kingine cha kukumbuka ni kuwa ni wajibu wa watendaji wa umma kuwawekea mipaka ya kiutendaji viongozi wa kisiasa maana wao ndio "accounting officer". Ni vigumu kufanya hivi ikiwa wote ni wanasiasa maana kila mmoja anakuwa na lengo la kujijenga kisiasa.

Huu sio utaratibu mzuri. Watendaji walitakiwa kuwa watumishi wa umma ambao wanajibika kwa serikali na sio chama tawala. Lakini haya yanajitokeza kwa sababu lengo ni ushindi wa kisiasa kwa namna yeyote ile. Wote tunajua mtu muhimu ni yule anayehesabu kura na sio yule anayepiga kura.

Amandla...
 
Mimi naamini huko wilayani kuna Watumishi waandamizi wanaofaha sana,Kulinganga na hii JD.Hata baadhi ya wakuu wa idara waandamizi wangefaha, kuliko kuleta watu wasio na uzoefu wala taaluma.Kwani lazima ateuwe fresh???ona sasa, Hii itakuja kuharibu na kuvuruga kila kitu
 
Tatizo siyo Rais Samia, ni washauri, wanaopendekeza na wanaomzunguka.
Ni lazima kuwe na succession plan nzuri kwa watumishi wa serikali...
Umesema vizuri kwamba wanaopendekeza,kwa hiyo kupendekeza Siyo kuteua,kweli kama kuna wanaopendekeza???Kwa nini asikae ofisini apitie mafaili ajiridhishe kwamba kilichopendekezwa kinafaa? Ndiyo maana unakuta mtu apangwa Halmashauri 2,angesoma hata ilo angeliona.
 
Back
Top Bottom