Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Uzi kama huu ni bora upite kimya kimya tu. Pengine kauli na matendo kama hayai ndiyo ilikuwa ni sababu kuu ya kuwalaumu wapinzani kuwa wanacheleweshea maendeleo.
 
Inaweza kuwa hii hapa
 
Attachments

  • images-5.jpeg
    images-5.jpeg
    7.1 KB · Views: 1
Aiseeee. Mbona mkubwa wako anajidai kwa kauli zake za hii nchi ni tajiri! Mkuu wakati wanaomba kuchaguliwa kipindi cha kampeni si husikika wakisema tunaongea yaliyoandikwa kwenye ilani ya chama chao? Kuhusu mapato nakupinga, kwan kila siku yanakusanywa, tena wanakusanya na mapato kwa watu ambao kwa akil ya kawaida hustahili kuwaomba kodi. Alafu hizo hela tunazotoa kwenye kodi zetu ndo hizo mtu anaenda nazo chato, ndo hizo mtu anafanyia miradi ambayo inatuumiza, miradi ambayo watesi wake waliipga posp coz walitambua watu lzm waumie. Ko lengo la jamaa n kutuumiza kwa mgongo wa mkopo kipind tunasoma? Alafu mkopo ile ni biashara ya kinyonyaji, sitaki tuingie huko mana huko ndo wanatunyonya waz waz. Moreover mkopo hatukupewa bureeee. Alafu mkopo unalipwa, so hasara iko wapi?
Hivi zisingekuwepo hizo hospital za private serikali ingeweza kuhudumia watu vzr kweli?
Na mshukuru hizo hospital zinasaidia kupumguza idadi ya unemployed doctors na manesi wengi.

Muwe mnajua na kushukuru nyinyi nyang'au
Wewe ndio ujue kushukuru sio serikali umepata faida za uwekezaji wa merit goods serikali yako iliyokufanyia ili uwe msaada kwenye jamii, sasa hivi unaleta ngebe.

Yaani serikali iwasomeshe madokta tena wengi wao wasingeweza fanikiwa ndoto zao bila ya ivyo, iwaajiri, iwape experience ya kutibu, wawe watu wenye thamani; halafu waanze kuvimba.

Hao private waache kupenda kuvuna wasipopanda.

Mtu kama wewe ilifaa unyimwe mkopo wa elimu ya juu ubaki unapambana na nyoka mashambani.

Umesomeshwa bure sasa hivi unaanza kuitukana serikali.
 
Siamini kama kasema hivyo! Na kama ni kweli basi inaogopesha, lile swala la kufuata sheria bila shuruti limeishia wapi?!
Wasilipolipa mikopo basi tutamuelewa, AU SABABU YA KUPEWA GRANTS???!!! Na kama ni hivyo basi wawekeane mkataba wakimaliza kulipa hizo GRANTS WAWE HURU...
 
"Ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda".

Jiwe lina roho mbaya sasa unataka kuifungia hiyo hospital binafsi kwa kosa lipi..huyu mzee mshenzi sana yaani.

Anazidi kutuaminishia ili uonekane mzalendo ukubali umaskini,,,yaanimtu umlipe kidogo na kuna mahalianalipwa vizuriunataka ang'ang'anie anapolipwa kidogo kisa uzalendo na waiati huo huo akija mwenyekiti wa UV CCM ana uwezowa kumnyanyasa anavyotaka huu ni upumbavu wa hali ya juu.
 
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

Rais Magufuli amenukuliwa akisema
“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”
Ongeza maslahi uone kama wataenda private,uzalendo siyo kuumia kwa sababu ya mtu mmoja mbinafsi ambaye anajali sana maeneo ya kwake kuliko maslahi mapana ya taifa uzalendo ni kuwezeshana kila mtu aridhike na kile anachokifanya.
 
Siamini kama kasema hivyo! Na kama ni kweli basi inaogopesha, lile swala la kufuata sheria bila shuruti limeishia wapi?!
Wasilipolipa mikopo basi tutamuelewa, AU SABABU YA KUPEWA GRANTS???!!! Na kama ni hivyo basi wawekeane mkataba wakimaliza kulipa hizo GRANTS WAWE HURU...
Ile sio grant mkuu ni mkopo tena ambao unalipwa by hook or by crook
 
Wewe ndio ujue kushukuru sio serikali umepata faida za uwekezaji wa merit goods serikali yako iliyokufanyia ili uwe msaada kwenye jamii, sasa hivi unaleta ngebe.

Yaani serikali iwasomeshe madokta tena wengi wao wasingeweza fanikiwa ndoto zao bila ya ivyo, iwaajiri, iwape experience ya kutibu, wawe watu wenye thamani; halafu waanze kuvimba.

Hao private waache kupenda kuvuna wasipopanda.

Mtu kama wewe ilifaa unyimwe mkopo wa elimu ya juu ubaki unapambana na nyoka mashambani.

Umesomeshwa bure sasa hivi unaanza kuitukana serikali.
Kwahiyo ukikosea ww kama serikali nisikwambie, na hili ndilo linalofanywa na viongoz ngazi ya juu, wanaona mtu anakoenda si salama wanakausha? Hii nchi yetu sote kila mmoja anatakiwa kujivunia nchi yetu, ukiiharibu nam naona ntakuwa mjinga sana lazima nikukemeee
Serikali. Kwanini serikali.
Badala ya kujiulizia wapi tunakwama mnataka ndo mharibu kabisaaaa, haya umefungia hiyo hospital kwahiyo wale waliokuwa wameajiriwa kufanya kaz kwenye hiyo hospital utawaajiri ww? Mambo mengine yakukurupuka sanaaaaa
 
Ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda".

Jiwe lina roho mbaya sasa unataka kuifungia hiyo hospital binafsi kwa kosa lipi..huyu mzee mshenzi sana yaani.

Anazidi kutuaminishia ili uonekane mzalendo ukubali umaskini,,,yaanimtu umlipe kidogo na kuna mahalianalipwa vizuriunataka ang'ang'anie anapolipwa kidogo kisa uzalendo na waiati huo huo akija mwenyekiti wa UV CCM ana uwezowa kumnyanyasa anavyotaka huu ni upumbavu wa hali ya juu.
 
Hii nchi tunakoelekea ni kubaya zaidi.

Huyu mwalimu wa science tena kipindi kile walimu wa science shule za vijijini walikuwa wachache sana ila aliamua kuacha wanafunzi na kugombea ubunge. Masilai ya ualimu aliona ni kidogo. Ubunge wenyewe aligombea awamu mbili bila kufanikiwa.

Hayati Benjamini william Mkapa ndyo akampa support baada ya kuitenga chato ndipo Rais JPM alifanikiwa kuwa mbunge.

Leo hii daktari wa serikali kaacha kuwa mtumishi wa serikali na kaenda kufungua hospitali binafsi ambayo imeongeza huduma katika jamii ila Rais Magufuli kwa Roho ya kwanini anataka awaingize matatani.

Nakumbuka Rais mstaaf J. Kikwete aliwahi kuzungumza juu ya katiba inavyompa Rais nguvu kubwa na hivyo inahitaji busara sana kuendesha nchi kama Tanzania.

Kusema ukweli hii busara magufuli hana kabisa. Na waliopo karibu naye wanashindwa kmweleza ukweli ilimradi vibarua vyao visiote nyasi au wanasubiri aboronge ili akiondoka wamsengenye.
 
Back
Top Bottom