Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Hivi umeelewa kilichoandikwa au kinachojadiliwa?! Umeambiwa huko hospitali binafsi huwa hawalipi mkopo?!
Naelewa...
Kama hakufuata taratibu za kuacha kazi ni shida, na kama hajalipa deni ni shida pia
 
Kuna mambo huwa anaongea haya-make hata sense.
 
Kwa akili hizi mbilikimo utaendelea kuwa zumbukuku mpaka unaingia kaburin
Ndio maana nikakwambia inategemea na nafasi, sasa mtu keshakuwa experienced Dr na hiyo experience kapewa na serikari jumlisha na elimu yake iligharamiwa na serikali halafu asepe tu.

It’s not hard to train a teacher or replacing one uitaji kumuwekea ‘restrictive covenant’ kwenye mkataba wake. But a doctor is another story it takes time and money to train one and they become more valuable with years of experience.

Halafu experienced Dr asepe tu kirahisi rahisi bila ya ridhaa ya mwajiri wake ilo kwakweli hapana atapike hela za serikali; kwanza sio kitendo cha kiungwana wala kizalendo.
 
Huu ni upumbavu, Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake.....kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu...........what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mkopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.
Ukapimwe akiliii
 

Kwakuwa tunapenda kuiga mabeberu nimeweka standard framework ya mkataba wa ajira NHS uchukue mfanyakazi wao bila ya ruhusa yao au kuwalipa compensation halafu uone watakachokufanya.

Kwa haraka wale wabishi wapitie page 6 or 8 waone madhara ya kuongea na mtaalamu wao bila ya ruhusa yao au kuchukua mfanyakazi mwenye mkataba nae bila ya idhini yao au kuwalipa fidia.

It costs lots of money to train medical professionals and giving them experience; that’s why they are valuable to any employer.

Sisi watanzania tunatabia ya kuchukulia vitu rahisi sana, serikali yetu imekuwa ya kibepari zaidi kuliko wananchi wanaopiga kelele kudai free market.
Acha kutetea ujinga kwa sababu tu kinacholalamikiwa unadhani hakikuhusu! Nani alitarajia ujinga kama huo unaweza kufanywa kwa madaktari as if mtu akifanya sekta binafsi atakaotibu huko sio Watanzania. Na kama madaktari yanawakuta hayo basi hata wewe au watu wako wa karibu yanaweza kuwakuta kwenye sekta zao ingawaje hapa unaoona bora kutetea ujinga kwa sababu haukuhusu! Hata hiyo link uliyowek kuhalalisha utetezi wako haihusiani kabisa na alichosema Mheshimiwa Rais
 
Naelewa...
Kama hakufuata taratibu za kuacha kazi ni shida, na kama hajalipa deni ni shida pia
Ndo alivyosema hakufuata taratibu?! Ina maana hujaona kwamba anacholamimikia ni hao madaktari kwenda kufanya kazi hospitali binafsi as if huko wanaoitibiwa sio Watanzania!!
 
Ndo alivyosema hakufuata taratibu?! Ina maana hujaona kwamba anacholamimikia ni hao madaktari kwenda kufanya kazi hospitali binafsi as if huko wanaoitibiwa sio Watanzania!!
Wewe unazijua taratibu?
 
Kule hawatibu watu ?

Wanadaiwa ?, Wamelipa hawajalipa ?, kuliko kufungia hospital / mtu anayetibu watu pia ni rahisi sana kwenye mkataba wa mkopo waseme kwa miaka kadhaa lazima ufanye kazi ya serikali sehemu yoyote utakayopelekwa (hapo mtu anakuwa anabanwa kwa mkataba) sio aina hii ya sheria / maamuzi kutoka kwenye kinywa cha mtu
Hawawezi kuweka hiyo clause ya lazima wafanye kazi serikalini kwanza kwa kuwa serikali haina uwezo wa kuajiri.
Kwa kifupi mzee akili yake imepatwa na 'changamoto ya upumuaji'
 
Wewe unazijua taratibu?
Issue sio kuzijua au kutozijua; issue ni kwamba ana-mind kuona madaktari waliopewa mkopo 100% wanakataa kufanya kazi hospitali za serikali na kwenda hospitali binafsi kwa ajili ya kufuata maslahi! Cha kujiuliza ni kwamba, sasa ikiwa tumeruhusu hospitali binafsi kujengwa; sasa tunatarajiwa wao watoe wapi madaktari ikiwa madaktari waliopewa mkopo ni serikali inakuwa nongwa kwenda huko!!
 
Miaka mitano iliyopita alilalamikiwa sana kwa kugandamiza na kuua sekta binafsi. Malalamiko haya akayajibu katika hotuba yake ya kufungua bunge baada ya ushindi wake wa kishindo mwaka jana kuwa serikali yake itasaidia kukuza sekta binafsi.

Lakini leo Mungu ajuaye ya moyoni mwa mtu amemuweka wazi jinsi alivyo na chuki kwa sekta binafsi. Yaani mtu kwenda kutafuta ugali wake na watoto tena wa halali anawindwa kama mwizi!!!!. Kwa kweli leo ile chuki imejidhihirisha waziwazi
 
Hapa inabidi kuangalia kipi ni kipi. Uzalendo ni kitu kizuri, lakini uzalendo ni kwa kila mtu, na si kwa watu wachache tu. Sis binadamu siku zote tunataka zaidi na bora, kwa hiyi daktari kuhama kwa ajili ya maslahi siyo kukosa uzalendo. Huyu daktari kahamia hospitali binafsi lakini anatibu Watanzania.

Katika hili la uzalendo pia inabidi tuangalie. Kama hakuna sheria inayowalazimisha waliyopata mikopo kuitumikia serkali, basi huyu daktari asilazimishwe, maana hata huo mkopo anaulipa. Sasa kama anaulipa kwa ni alazimishwe kutumikia hospitali ya serkali wakati huo mkataba haukuwepo?

Miaka ya nyumba 60s/70s kulikuwa na sheria ambayo mwanafunzi akisomeshwa anatakiwa aifanyie serkali miaka mitano. Kama serkali inataka hivyo, inatakiwa iiweke hii kama mojawapo ya masharti ya mkopo. Bila hii kuwepo, huwezi kumlazimisha mtu kuitumikia serkali. Tuepuke kutunga sheria kwa midomo yetu. Tuweke hivi vitu wazi na siyo kila kukicha matamko yanatoka ambayo ni sawa na sheria.
Miaka ya 70 hiyo sheria ilikuwepo kwa sababu serikali ilikuwa na uwezo wa kuajiri, hii ya CCM mpya JPM imekata pumzi na imeishiwa ubunifu, hivyo haiwezi kutunga hiyo sheria.
 
Acha kutetea ujinga kwa sababu tu kinacholalamikiwa unadhani hakikuhusu! Nani alitarajia ujinga kama huo unaweza kufanywa kwa madaktari as if mtu akifanya sekta binafsi atakaotibu huko sio Watanzania. Na kama madaktari yanawakuta hayo basi hata wewe au watu wako wa karibu yanaweza kuwakuta kwenye sekta zao ingawaje hapa unaoona bora kutetea ujinga kwa sababu haukuhusu! Hata hiyo link uliyowek kuhalalisha utetezi wako haihusiani kabisa na alichosema Mheshimiwa Rais
9B39B0DC-1EA4-4DDA-B01D-57BA8F1E1139.jpeg


Huyo ni government employer kama wizara ya afya kwetu, kwanini unadhani ata huko kwao awachukulii poa watu kuondoka kiholela?

Jioni njema, time for my evening walk.
 
Back
Top Bottom