Pole kwa yaliyokukuta ndugu, naona jiwe la gizani limekupata! Ila kuna vitu tunapaswa kujua, Magu ni mzalendo kupindukia:
SERIKALI inakupa full sponsorship ya exceptional, unique Medical Courses mfano areas of specialization kama NEUROSURGERY, KIDNEY TRANSPLANT , HEART SURGERY kwa gharama kubwa kama Mtumishi wao unamaliza masomo baada ya masomo unaamua kuhamia hospital binafsi bila kujali pesa nyingi za walipa kodi zilizowekezwa kwako
Yaani kwenye public kupata huduma yako gharama ni chini
Huko kwenye private hospital kupata huduma yako gharama ni kubwa kweli na ndio wanapopata pesa ya kukuongezea huo mfano.
Kwa ufupi huyo mwenye private hospital anakuwa amekufanya bidhaa anakupandisha bei kwenye hospital yake dhidi ya watanzania ambao pesa zao ndio zimekusomesha
Kwa ufupi huyo mwenye private hospital anakuwa ameigeuza public ASSET kuwa private asset kwa maslahi yake BINAFSI bila kujali UWEZO wa watanzania.
Hivyo naunga mkono maelezo na maelekezo ya Mhe Rais
Kama huyo mwenye private hospital asomeshe specialist wake kisha aweke gharama kubwa kuonana na wagonjwa badala mtindo wa sasa unamchukua specialist aliyesomeshwa na SERIKALI kisha unaweka gharama kubwa kuonana na wagonjwa ambao ndio hao hao wamemsomesha huyo specialist kwa gharama kubwa kupitia kodi zao akiwa Mtumishi wa SERIKALI