Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Hilo ndio tatizo la kuajiri watu bila kufanyishwa interview. Mimi nilikua namshauri Rais waanze kufanyishwa na interview heshima ya kazi itarudi tu.
 
Hivi we we unafahamu garama za huko private kweliii??? Hao walalahoi waliomsomesha daktari wataweza kumuduu?? Acheni utani na fedha za umaaa
Nani kakudanganya kwamba walala hoi ndo walipakondi wakuu nchini na duniani?? Fikiri sawasawa
 
NIKUKOSA UZALENDOO. MADAKTARI HAWA WAMESOMA KWA KODI ZA LALA HOI WAUZA MAHINDI NA NAMAHARAGWE, HALAFU MNAWAKIMBIA WALIOWAWEZESHAA?? KUNA LAAANA ITAFUATA JUUU YAO
hilo neno uzalendo siku hizi linatumika kuwatia watu waendelee kuwa mazuzu!!kila kitu kinasimamiwa na sheria,na sio matamko ya mtu!! hao mnaowatumikisha hadi wanastafu kisha mafao yao yanakuwa ni kama hisani kuwapatia hadi wanafariki huo ndio uzalendo?!!mtumishi ana miaka 3 toka astafu hadi leo hata nauli tu ya kumrudisha kwao bado!!!yaani mtu kuacha kazi kwa kufuata utaratibu uliopo kisheria nako kumekuwa kosa?!!ni suala la muda tu huko mbeleni (awamu ya 6) serikali itafunguliwa kesi nyingi sana za watu kudai fidia!!nje na ndani ya nchi!!
 
Hivi hizo garama za hispitali za private hao walalahoi waliomsomesha kwa kuuza mahindi na maharagwe wataweza kumudu garama zile?? Yeye daktari yule aliyeajiriwa kwenye hospitali zetu walalahoi, amalize mkataba wetu ili tunufaike tuliomsomesha, kisha akatafute hizo hospitali, ambazo kumuona daktari na lakimoja hukubado hujalipa vipimo na dawa zakee
Walipa kodi wakuu ni matajiri shutuka acha kujidanganya na kudanganywa
 
Huyu Mzee hopeless sana...

Anasema;

"....madaktari hao na hospitali zinazowarubuni watoke katika hospitali za serikali kwa kisingizio cha maslahi zifuatiliwe...."

Kauli ya "zifuatiliwe" maana yake zimefanya makosa kuwaajili madaktari hao na kwa hiyo hatua kali zichukuliwe dhidi ya hospitali hizo..!

Kauli ya namna hii toka kwa Rais Wa nchi inashangaza sana. Badala ashukuru kuwa sekta binafsi inasaidia serikali kuajiri watu wake, yeye anatoa kauli za ajabu ajabu zilizo na harufu ya u - siasa siasa tu kwa ishu serious kama ajira na maslahi ya watu...

After all madaktari mitaani wako kibao. Kwani serikali isiajiri hao?

By the way huko walikoenda hawa madaktari (hospitali binafsi) nako wameenda kuhudumia watu, Watanzania hawahawa. Sasa sijui shida iko wapi...
Ndio hivyo halafu pia zinalipa kodi Licha ya Kuwa inatoa Ajira kwa watu wengine
 
Wa Mtaani ambao hawana ajira kabisa, mbona wapo wengi

Ni Sawa na kung'ang'ania kurubuni Mke wangu wakati kama Yeye wapo wengi tu mtaani

Ifike hatua Private waweke kigezo cha kutoajiri mtu yeyote aliwahi kufanya kazi serikalini ili wasikwazane na Mamlaka z nchi
Huko nako wanataka walio experience. Not fresh from university... Kizunguzungu
 
hilo neno uzalendo siku hizi linatumika kuwatia watu waendelee kuwa mazuzu!!kila kitu kinasimamiwa na sheria,na sio matamko ya mtu!! hao mnaowatumikisha hadi wanastafu kisha mafao yao yanakuwa ni kama hisani kuwapatia hadi wanafariki huo ndio uzalendo?!!mtumishi ana miaka 3 toka astafu hadi leo hata nauli tu ya kumrudisha kwao bado!!!yaani mtu kuacha kazi kwa kufuata utaratibu uliopo kisheria nako kumekuwa kosa?!!ni suala la muda tu huko mbeleni (awamu ya 6) serikali itafunguliwa kesi nyingi sana za watu kudai fidia!!nje na ndani ya nchi!!
Na wewe tengeneza kiki uende uberigiji kamaa jamaa yenuu
 
Na yeye arudi shule akafundishe nyambaf!yee c mwalimu?
 
Restraint of trade?

Ile ilikua ni mkopo au bond?

Endapo waajiriwa wa private wanasomeshwa na wanasign bond, na bado huwezi kumzuia kuondoka baada ya masomo....ndio sembuse mkopo?

Tena ambao unalipwa back?

Anyways.
 
Wa Mtaani ambao hawana ajira kabisa, mbona wapo wengi

Ni Sawa na kung'ang'ania kurubuni Mke wangu wakati kama Yeye wapo wengi tu mtaani

Ifike hatua Private waweke kigezo cha kutoajiri mtu yeyote aliwahi kufanya kazi serikalini ili wasikwazane na Mamlaka z nchi
Nayo serikali iweke marufuku ya kuchukua watumishi kutoka sekta binafsi.

Tunaakili za jishamba sana
 
Huu ni upumbavu, Rais lazima asaidiwe na wasaidizi wake.....kauli zake za siku hizi hata chekechea anashangaa. Kuwekeana masharti mtu anatafuta maisha yake ni ujinga, ajirini wengine wapo mtaani kibao tu...........what if alijisomesha mwenyewe hakutumia huu mkopo ambao umeturudisha kwenye Ukoloni aliopambana nao Nyerere.
Kwa taarifa yako kuna watu walipiga makofi alivyotamka hivyo.
 
Jamani kwani kwenye hospitali binafsi anatibu ng'ombe? si ni hawa hawa watanzania wanyonge....mbona madaktari wamejazana mtaani mmeshindwa kuwaajiri, ubabe mwingine hauna maana...
 
Sasa ndio naelewa kwanini Kuna baadhi ya watu wakifa masela wanachimba futi zaidi ya kumi. Yani Kuna watu Mungu huwaleta duniani kuitesa jamii wanayoishi ili kuwakumbusha wanadamu uwepo wake. Akiwa mtawala mtu wa aina hiyo taifa Zima huugua.
 
Katiba yetu ni mbovu. Mbovu kweli kweli.

Katiba yetu inampa mamlaka mtawala ya kufanya chochote, kwa yoyote, muda wowote tena pasipo kuhojiwa ama kuwajibishwa na yeyote ama taasisi yoyote. Hii ni hatari Sana.

Kama katiba yetu ingekuwa bora JPM alipaswa kuwajibishwa kwa kueneza chuki, ubaguzi, uminyaji wa demokrasia na ukiukwaji wa sheria mbali mbali za kiutawala na sheria za kazi.

Iko mifano mingi unayoweza kuitoa lkn mmojawapo ni huu wa Tabora, ambapo ameagiza daktari aliyeacha kazi serikalini afuatiliwe kisha afungiwe na na Hospitali aliyokwenda ifungiwe.

Shime watanzania tudai katiba mpya ili kila kiongozi awe na mipaka ya kiuongozi. Na aogope kusema na kutenda atakacho.

Mfano huyu mwekezaji na daktari wanakwenda kupoteza haki zao za kujipatia kipato kupitia mitaji na elimu zao kisa tu kuna mtu mmoja hajafurahi.

Katiba bora ndiyo silaha pekee dhidi ya uwonevu.
 
Back
Top Bottom