Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama Hospitali ya Rufaa mkoani Tabora kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi wafuatiliwe

kama Mtumishi wao unamaliza masomo baada ya masomo unaamua kuhamia hospital binafsi bila kujali pesa nyingi za walipa kodi zilizowekezwa kwako
Kwani huko private anatibu wasomalia?.

Siyo kila kitu anachosema jiwe mkiunge mkono. Wakati mwingine jaribu kuwa wewe achana na upenzi na ushabiki
 
Dunia nzima inatcheka kuweka kituko kama hiki ikulu. Ongea yake, uwezo wake wa kujenga hoja vinatosha kabisa kuwa sabb ya kumpeleka Milembe
Na baya zaidi, tulimkataa kwenye sanduku la kura ila vile vinavyoitwa vyombo vyetu vya ulinzi vimempachika kinyume na matakwa yetu tulio wengi!
 
Kwani huko private anatibu wasomalia?.

Siyo kila kitu anachosema jiwe mkiunge mkono. Wakati mwingine jaribu kuwa wewe achana na upenzi na ushabiki
Hata mimi mwanzoni niliwaza hivyo...private si bado wanatibu watz!? Lakini ukweli ni kwamba wananchi wa maisha ya chini hawawezi kukusogelea kupata huduma yako!

Hivyo kama kweli ulipata scholarship ya wizara afu umalize na kutokomea private wakati public wanakuhitaji mtetezi wa wanyonge hawezi kukuacha hivihivi! Hivyo tupunguze hasira na jazba! Let have a look at this issue in different perspective 😂!
 
Ndiyo maana tunajadili. Tutapata njia tu ya kumuondoa tu huyu mental case. Ni suala la muda tu.
Mental case nafikiri ni ww! Magu yupo smart kuliko unavyodhani! Eti tumuondoe, ili ukae ww!?
 
Nilitaka kuwa upande wake hadi niliposoma maneno yako haya!..
HAKUNA mwenye uwezo wala ujasiri wa kumwambia mzee kuwa "HAIWEZEKANI KWA SABABU NI KINYUME NA KATIBA/SHERIA" Mikutano ya kisiasa na shughuli nyinginezo zilipigwa marufuku kimasikhara masikhara ila ndo ilishatoka hiyo, pamoja na kwamba ilikuwa kinyume kabisa na katiba ya nchi...

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Serikali ingekuwa haijui umuhimu wake ingemsomesha bure?

Nchi inatumia tsh 700 billion kwa mwezi kulipa mishahara tu ya wafanyakazi, serikali hiyo hiyo iwatafutie vifaa tiba na majengo; ni hivi karibuni tu ndio imekuja na bima kujitua baadhi ya mzigo...
Wewe jamaa una akili matope sana, kwani nikienda kufanya kazi private natibu ng'ombe?

Au nakuwa natibu raia wa Msumbiji?

Halafu unaleta utetezi wa kijibga kabisa kwamba 7billion zinalipa mishahara kwa hiyo?

Walipokuwa wanatunga sheria ya utaratibu wa maslahi ya watumishi wa umma hawakujua hilo? Na mbona sheria yenyewe hawajaifuta?

Serikali hii inayokusanya zaidi kuliko serikali zilizopita inashindwaje kuongeza hiyo mishahara kwa miaka mitano,lakini iliyokuwa "dhaifu" ya JK, iliweza kujenga miundo mbinu, kuajiri kila mwaka sekta muhimu kama afya na elimu, kuongeza mishahara kwa mujibu wa sheria,na haikukopa kwa kiwango cha serikali hii,sasa hii inayokusanya zaidi pia inakopa zaidi, wakati huo huo miradi mingi ni kwa ufadhili wa....[emoji849][emoji849][emoji849]

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ndio ujue kushukuru sio serikali umepata faida za uwekezaji wa merit goods serikali yako iliyokufanyia ili uwe msaada kwenye jamii, sasa hivi unaleta ngebe...
Hivi serikali inasomesha bure?

Mkopo wenye riba juu na tozo lukuki unaita "bure"? Tuache utani bhana haya ni mambo serious mnooo

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Hapa Rais wangu unakosea.tuweke sawa sentensi.tunakopeshwa hizo fedha.hatupewi bure.kwa hiyo tunajisomesha.kikubwa mkopo unarejeshwa?habari ya mimi nafanya kazi wapi haikuhusu.hata wewe uliacha ualimu ukaenda bungeni.ulifuata maslahi.unalalama uraisi ni kazi ngumu.lakini huachi.kisa maslahi.huu mwaka wa ngapi huongezi mshahara.tunafanyaje?hh
Ukifuatilia sana utakuta ni lile kundi lililopata msamaha wa bunge kutolipa deni ambalo sheria iliweka wazi wahusishwe waliomaliza kuanzia 1998 na kurudi nyma
 
Amekuwa mwenda wazimu kwa kutaka tu kanuni zifuatwe? Nimeeleza kanuni husika katika Uzi Na. 25. Mimi mwenyewe nilisomeshwa na serikali mpaka shahada ya kwanza na kwa masomo ya juu zaidi nilisomeshwa na Umoja wa Mataifa. Mfadhiri wangu huyo alisisitiza nitie sahihi mkataba kwamba baada ya kuhitimu nirudi nchini kwangu na kufanya kazi nitakapopangiwa na serikali kwa kipindi kisichopungua miaka mitano. Vivyo hivyo na wenzangu waliofadhiriwa na mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali. Sasa yote hayo tuyaseme kuwa ni wenda wazimu?
HAKUNA mtu anakataa hizo kanuni, lakini je, Daktari wa Tanzania anasomeshwa kwa "ufadhili"? (Labda kama maana ya ufadhili imebadilika) lakini ninachojua gharama za elimu ya juu unakopeshwa na ni wajibu wako kulipa, haijalishi umeajiriwa na serikali, sekta binafsi au hata haja-ajiriwa kabisa, lakini ni lazima ulipe!

Sasa wewe unafananishaje hilo na ufadhili wa umoja wa mataifa?

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
So long as the government is paying for the cost of their enhacement studies ni waajiriwa, besides they need to practice even after gaining further qualification kabla ujaitwa daktari bingwa experience which again is provided by government institutes or their partners...
Lakini uzalendo ni kwa wataalam tu, wanasiasa wananunua migari ya Milioni 400, wanakula Kodi zetu watakavyo hilo halina shida lakini Daktari,mwalimu, Askari, na wengineo wao hawatakiwi kutafuta maisha mazuri coz of "uzalendo" huu ni ubinafsi tu

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Sorry to say this but rais hapa umeteleza!!

Unaposema unawasomesha hawachangii kwani hiyo mikopo si inatokana na kodi? je hizo hospitali za private hazilipi kodi?

Unaposema hela yenu wamekula wamekula kivipi? kwani hawalipi mkopo kila mwezi?

Alafu mzee baba hujui mtumishi yeyote anatafuta maslahi? sasa wewe huongezi mishahara unataka waendelee tu kukaa hapo kisa uzalendo?

Mzee huu ni mwaka 2021 na sio mwaka 1970! unapoongea jua unaongea na watu wenye akili zao kichwani!!

Huwezi ukawa mzalendo kama una njaa! HATA WEWE ULIKIMBIA CHAKI UKAENDA KWENYE SIASA!!
Huu ni ukweli tuendelee kujitafakari maamuzi yetu lakini mwisho unakaribia
 
Katiba yetu ni mbovu. Mbovu kweli kweli.

Katiba yetu inampa mamlaka mtawala ya kufanya chochote, kwa yoyote, muda wowote tena pasipo kuhojiwa ama kuwajibishwa na yeyote ama taasisi yoyote. Hii ni hatari Sana.

Kama katiba yetu ingekuwa bora JPM alipaswa kuwajibishwa kwa kueneza chuki, ubaguzi, uminyaji wa demokrasia na ukiukwaji wa sheria mbali mbali za kiutawala na sheria za kazi.

Iko mifano mingi unayoweza kuitoa lkn mmojawapo ni huu wa Tabora, ambapo ameagiza daktari aliyeacha kazi serikalini afuatiliwe kisha afungiwe na na Hospitali aliyokwenda ifungiwe.

Shime watanzania tudai katiba mpya ili kila kiongozi awe na mipaka ya kiuongozi. Na aogope kusema na kutenda atakacho.

Mfano huyu mwekezaji na daktari wanakwenda kupoteza haki zao za kujipatia kipato kupitia mitaji na elimu zao kisa tu kuna mtu mmoja hajafurahi.

Katiba bora ndiyo silaha pekee dhidi ya uwonevu.
Ni kweli ila katiba tu bado haitatosha, kumbuka kuna mengi sana viongozi wanafanya kwa utashi wao japo katiba hairuhusu. Katiba hata kama ni bora lakini na sisi watanzania kuna mahala tunakosea. Huyu mtu alipaswa ateremshwe hata jukwaani kwa nguvu ya umma mara baada ya kutamka maneno kama hayo lakini kwakuwa watanzania ni watiifu, wasaliti, waoga, wanafiki nk basi hili haliwezekani. Ndiyo katiba mpya ni muhimu sana lakini sisi watekelezaji wa matakwa ya katiba kama hatuna hofu na utii juu ya katiba hiyo mambo bado yanaweza kuwa yaleyale.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Twambie yeye alipoacha kufundisha na kwenda kugombea ubunge nafasi yake alim-replace nani?


Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Achana na watu nilichogundua watu akili zao ni mbovu kuliko neno ubovu, tena waliosoma zamani walisoma bure kwa fedha za serikali (umma) lakini wakaacha wakaenda kwenye siasa. Huko bungeni wapo wengi wameacha kazi za umma wakakimbilia huko kuzoa pesa za bure leo daktari anatafuta pa kunusuru maisha ya familia yake Mh rais anatoa kauli za ajabu na wapumbavu wachache wanamuunga mkono. Yaani ingekuwa katoa kauli hizi kwenye nchi zenye raia wanaojitambua hakika angeteremshwa jukwaani.... Hata huko private wanaotibiwa huko ni watanzania wenzetu, hata kama wanakipato cha juu ni sawa maana sote hatuwezi kulingana. Najiuliza kwani rais yupo kwa ajili ya watu maskini tu? Ndiyo maana haongezi mishahra ili watu wazidi kuwa maskini na wazidi kutawaliwa!

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Kwani akiwa huko hospitali binafsi, si anarejesha mkopo!? Ama mimi ndiye nimeingia kwenye uwanja wa mpira na shoka!!!
====
Kuna uwezekano mkubwa Rais amenukuliwa vibaya, ngoja nitafute chanzo halisi.
Ondoeni huu ujinga wa kanukuliwa vibaya mpaka sasa hospital imeshafungwa huko mnatetea upumbavu mpaka mnatia huruma

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom