Katiba yetu ni mbovu. Mbovu kweli kweli.
Katiba yetu inampa mamlaka mtawala ya kufanya chochote, kwa yoyote, muda wowote tena pasipo kuhojiwa ama kuwajibishwa na yeyote ama taasisi yoyote. Hii ni hatari Sana.
Kama katiba yetu ingekuwa bora JPM alipaswa kuwajibishwa kwa kueneza chuki, ubaguzi, uminyaji wa demokrasia na ukiukwaji wa sheria mbali mbali za kiutawala na sheria za kazi.
Iko mifano mingi unayoweza kuitoa lkn mmojawapo ni huu wa Tabora, ambapo ameagiza daktari aliyeacha kazi serikalini afuatiliwe kisha afungiwe na na Hospitali aliyokwenda ifungiwe.
Shime watanzania tudai katiba mpya ili kila kiongozi awe na mipaka ya kiuongozi. Na aogope kusema na kutenda atakacho.
Mfano huyu mwekezaji na daktari wanakwenda kupoteza haki zao za kujipatia kipato kupitia mitaji na elimu zao kisa tu kuna mtu mmoja hajafurahi.
Katiba bora ndiyo silaha pekee dhidi ya uwonevu.