Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Tafakuri

Ukiona Mzazi wako anapenda kutengeneza tatizo kisha analitatua yeye mwenyewe, tena kwa kujifanya kwamba tatizo hilo limemuuma na anawajibika kulitatua yeye kwa sababu ana upendo sana, watoto mnatakiwa kuwa makini sana na vyanzo vya matatizo yenu katika familia.

Mosi, kama ikitokea kwamba tatizo lolote yeye hakulisababisha lazima Mtoto utawajibishwa tu tena bila huruma. Pili, Mzazi wenu akiwa ana tabia hizo mjue ni mpenda sifa kwelikweli. Tatu, ataendelea kutumia njia hiyohiyo ya kuanzisha matatizo na kuyatatua endapo watoto mtapiga kelele nyingi. Mkinyamaza mjue kwamba itakula kwenu na mtaumia kwelikweli.

Suluhisho Mzazi wenu akikosea mwambieni mapema kwamba, hili tatizo chanzo chake ni hiki, lakini kamwe hawezi kukiri kwamba yeye ndo kasababisha. Akijirudi ni kushukuru maana katambua alipokosea japo hataki kukiri kosa.

#LeaveUrLegacy

Simon Ngusa Jilala
Shida ya wapinzani wa Magufuli uelewa wao unafanana. hapa hoja imebaki eti katengeneza tatizo na kutoa suluhisho. Ni hatari sana upinzani wa leo wa spoon feeding
 
Leo niseme bila kupepesa macho miongoni mwa maeneo ambayo mheshimiwa wetu ameweza kutendea haki ni hili la kuwa refa/muamuzi katika jambo hili la mfuko mpya wa mafao hasa kanuni yake iliyotungwa na wazir juu ya kikokotoo.......

Kwa kweli hili lilikuwa lina watesa sana watumishi hasa wanaostaafu hivi karibuni kwangu niliamini kwa muda nitakao enda kustaafu hii kanuni itakuwa imeshafanyiwa mabadiliko mengi sana..........

Mheshimiwa ameamuru kikokotoo cha zamani kiendelee kutumika kama kawaida mpaka 2023 huku akiweka angalizo lifuatalo:-

(1)Ndani ya kipindi hiki cha mpito yafanyike mazungumzo ili ni kikokoto kipi ambacho ni best kitumike......

(2)kama mifuko itakuwa imara na kwakuwa ni yawafanyakazi basi hata kama inauwezekano ikalipa kwa mkupuo hata kwa asilimia 70% ifanye tu

(3)Raisi katoa angalizo na ndiyo wengi tuliokuwa tunalilalamikia hii mifuko ipunguze matumi na mipango isiyo na tija na hivi vitu ndiyo vilivyokuwa vinamaliza pesa za wanachama.....

(4)Raisi amesema atashangaa mpaka inafika 2023 hawajaja na kikokoto tena kilicho bora....

(5)Raisi kasema kustaafu ni heshima isiwe ni kero kwa mfanyakazi.....

HITIMISHO
Wapo watu wanasema ni muda tu je 2023 itakuwa je!!!! Imani yangu naamini vyovyote itakavyokuwa hayatajirudia madudu kama yale tena.....

Kikubwa yeye mwenyewe kaliona lilivyo la hovyo na teyari kaisha litolea maangalizo hapo si zani kama kuna mtu ataenda kumfanya raisi aonekane muongo naamini siyo kwa utawala huu....

Imani yangu mwanzo ni mzuri sasa mheshimiwa geukia na mshahara maana wewe ndiyo umekuwa chama cha wafanyakazi kwani hata hao TUCTA waliganda na 40% yani umewazidi kufikiri hata wao....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ni muhini sana. Alichowafanyia wafanyakazi ni kma machinga. Yan katuma wakuu wa mikoa awafukoze, wapigwe na wabomolewe mabanda yao, alafu baada ya wiki akaibuka kuwatetea.

Leo wafanyakaz wamekuwa affected psychologicaly. Ndyo anakuja kujisemesha. Siku zote alkuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Suala la mafao sawa lina walakini lakini, hivi suala la machinga kupigwa, kufukuzwa kwenye maeneo yao, mgambo kuwanyang'anya mama lishe vyakula vyao limeanzia awamu ya tano? Unapozidisha chuki huzaa dhambi!!!!
 
Usifanye mchezo yani baada ya kusikia Tundu Lissu anataka awe moinzani wa kwenye nafasi yake inabidi ubadili upepo huu mbaya
 
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka 3 hakuna ongezeko la mishahara na maslahi yenu yanazidi kukandamizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau , naombeni mnieleweshe Kama FAO LA KUJITOA limerudi nikalambe changu nipate mtaji
 
Kama wewe ni Mtaendaji Katika awamu hii ya Serikali ya Wanyonge ukiona hoja Halali ya Serikali (iliyoamuliwa na SERIKALI) Inapingwa na wengi na ukaona wanasiasa wa upinzani wanaisimmia ....ni lazima uwe makini sana katika kuipigia chapuo na kufafanua ! uataonekana mjinga mkubwa .Pole sna Irene Isacka
 
Kwa kweli kazi nyingine sii za kufanya. Basi tuu hakuna mbadala inabidi ukomae
 
HONGERA MR. PRESIDENT KWA HILO NAFIKIRI HUWA UNASOMA THREAD ZANGU NA COMMENTS ZANGU ZA UCHUNGU ZA MAFAO KUHUSU KUJITOA UANACHAMA KWA SISI PRIVATE NINACHOSEMA GOOD ENOUGH ILE KANUNI YA 33% YA KUKOSA AJIRA NI OVYO OVYO HAISAIDII KATIKA AJIRA ZA MIKATABA MIAKA 3
Kwani silaha waliyoitumia kwenye Muswada wa Sheria ya Mafao na Kanuni mpya za Mafao imekufa? Haikuzaa matunda? Wapinzani wanamkosesha Sana raha JPM! Kanunua Korosho kisa Zitto, Karekebisha KIKOKOTOO kisa Bulaya na Mnyika (Pongezi watetezi wa Kweli wa Wanyonge wa Taifa hili)! Mwambieni huyo Mzee ajiandae kwa makombora Mazito ya Tani nyingi kuanzia mwaka kesho! Itabidi akabidhi Hadi Mahakama kwa Jeshi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale mawaziri waliotokwa povu zito Bungeni kutetea hiki kikokotoo walikuwa wanafanya vile kwa maagizo au maslahi ya nani? Walikuwa "wakiitetea" Serikali ipi? Mheshimiwa Rais fukuza haraka watu wale maana walitaka kukuchonganisha na wananchi wanyonge mno. Usikubali kukaa na na mamluki wa JK😎
Acha kudanganya watu wewe hao mawaziri walitumwa na Jiwe na inafahamika wazi. Hii si serikali ya wanyonge ni kandamizi
 
Upuuzi mtupu na kuchezeana akili kwani hadi wanaanza huu mchakato hadi wanapitisha bungeni alikuwa wapi leo anataka kuwa staring
 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuboresha daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa.
Leo Dec 28. 2018 na viongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA), vyama shiriki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF & NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Rais Magufuli amewataka wenyeviti na watendaji wakuu wa NSSF na PSSSF pamoja na watendaji na Wizara kusimamia orodha ili kusiwepo na wastaafu hewa.
Aidha Rais Magufuli ametoa wito kwa hifadhi za jamii na kuzitaka kupunguza matumizi ya hovyo ya fedha na kuwekeza sehemu ambazo hazizalishi.
Vilevile amesema kuwa uwekezaji usio na tija usifanyike na kudai kuwa haufai na kutumia fedha za wanachama bila ridhaa yao.
Hata hivyo amewataka mifuko ya hifadhi ya jamii kupunguza gharama za uendesha na amesema kuwa hakuna haja ya kushindana kwa sababu kwa sasa kuna mifuko miwili ya sekta binafsi na sekta ya umma hivyo wanachama wa Serikali wahamishiwe PSSSF na wanachama wa PSSF ambao sio watumishi wa Serikali wahamishiwe

Chanzo muungwana blog
 
Pongezi za dhati zimuendee Kamanda Esther Bulaya. Kama sio juhudi zako Esther JPM asingesema kitu. JON alikuwa sehemu ya ule upuuzi wa mwanzo, sasa kwa jinsi anavopenda sifa amewakana wenzake. Doh wonders shall never end!!!!
 
Nashangaa wanaosema Rais ni mtetezi wa wanyonge na watumishi kwa ujumla! Kwaalichokifanya Leo ni muendelezo wa kukanyaga taasisi nyingine ambazo amekua akizipa maelekezo yeye mwenyewe na baadae kuja kuyapinga yeye mwenyewe....Hii Sheria ni serikali yake ndoiliyoipeleka Bungeni kupitia Waziri wake ambae kimsingi Rais anshiriki kwenye Cabinet...Anyway ata Bunge lilivopitisha muswada yeye aliusaini kwa mbwembwe kua sheria Leo inamaana ata wabunge wake na Spika wake aliemfanya msukule wake anawapinga Kweupee....Rais kama kweli ni mtetezi wa watumishi basi aombe Radhi watumishi kwa kuvuruga miundo ya utumishi hasa madaraja huwezi amini ila ndo ukweli Leo 2081 Wanaotakiwa kupandishwa madaraja ni watumishi wa 2014 lakini bado yuko 2012 je haoni kavuruga kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Anajua bongo mazuzu ni wengi kuliko werevu,na hao mazuzu ndo mtaji wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom