Leo niseme bila kupepesa macho miongoni mwa maeneo ambayo mheshimiwa wetu ameweza kutendea haki ni hili la kuwa refa/muamuzi katika jambo hili la mfuko mpya wa mafao hasa kanuni yake iliyotungwa na wazir juu ya kikokotoo.......
Kwa kweli hili lilikuwa lina watesa sana watumishi hasa wanaostaafu hivi karibuni kwangu niliamini kwa muda nitakao enda kustaafu hii kanuni itakuwa imeshafanyiwa mabadiliko mengi sana..........
Mheshimiwa ameamuru kikokotoo cha zamani kiendelee kutumika kama kawaida mpaka 2023 huku akiweka angalizo lifuatalo:-
(1)Ndani ya kipindi hiki cha mpito yafanyike mazungumzo ili ni kikokoto kipi ambacho ni best kitumike......
(2)kama mifuko itakuwa imara na kwakuwa ni yawafanyakazi basi hata kama inauwezekano ikalipa kwa mkupuo hata kwa asilimia 70% ifanye tu
(3)Raisi katoa angalizo na ndiyo wengi tuliokuwa tunalilalamikia hii mifuko ipunguze matumi na mipango isiyo na tija na hivi vitu ndiyo vilivyokuwa vinamaliza pesa za wanachama.....
(4)Raisi amesema atashangaa mpaka inafika 2023 hawajaja na kikokoto tena kilicho bora....
(5)Raisi kasema kustaafu ni heshima isiwe ni kero kwa mfanyakazi.....
HITIMISHO
Wapo watu wanasema ni muda tu je 2023 itakuwa je!!!! Imani yangu naamini vyovyote itakavyokuwa hayatajirudia madudu kama yale tena.....
Kikubwa yeye mwenyewe kaliona lilivyo la hovyo na teyari kaisha litolea maangalizo hapo si zani kama kuna mtu ataenda kumfanya raisi aonekane muongo naamini siyo kwa utawala huu....
Imani yangu mwanzo ni mzuri sasa mheshimiwa geukia na mshahara maana wewe ndiyo umekuwa chama cha wafanyakazi kwani hata hao TUCTA waliganda na 40% yani umewazidi kufikiri hata wao....
Sent using
Jamii Forums mobile app