Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Hao wawakilishi wa wafanyakazi ni wajinga
Badala waombe mishahara mikubwa ili wafanyakazi watatue matatizo yao ya sasa eti kikokotoo ambapo hujui lini utakufa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna mmoja alijaribu kuzungumzia hayo Rais akamrekebisha kwa kumuambia a-focus kwenye kikotoo na mafao..Nafikiri walijikita kwenye hilo zaidi.
 
Mshahara unatosha. Kama haukutoshi kopa ufanye ujasiriamali, nchi ikiwa na maendeleo kodi utakusanywa na vipato pamoja na mshahara vitaongezeka, so tujenge kwanza nchi. Wewe unataka serikali iongeze mishahara wakati tunakusanya bil 1300 kwa mwezi, mishara bili 578 kila mwezi, mifuko ya hifadhi bil 135 kila mwezi, loan repayment bil 300 kila mwezi, bado kuna wazabuni, miradi ya maendeleo, tuacheni kulalamika mishahara ikiongezeka serikali ita shutdown completely, itaongezwa tu endapo mazingira yataruhusu

Asante
 
Mh, Rais John Pombe Magufuri ametigua kitendawili hicho baada ya kusema kila mfuko uendelee na kanuni yake ya kikokotoo kwa wastaafu mpaka mwaka 2023. Pia ametoa maelekezo yafuatayo kwa mifuko ya hifadhi ya jamii

1). Kuhakikisha hakuna wastaafu hewa kwenye daftari la wastaafu.

2). Mifuko ya jamii kupunguza matumizi yasiyo na tija. Mfano kuchapisha kalenda na kujenga vitega uchumi visivyo leta faida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alikuwa anaongea kama nchi yake binafsi. pole yake sasa hivi atakuwa anaukaribisha mwaka mpya kwa mawazo sana ya kutumbuliwa.

Alipata kama brain freeze hivi maskini wakati mkulu anatoa hitimisho la kustakabali wa pensheni.
Leadership is an art, inabidi usikilize sana na kuongea kidogo.
 
MNYONGE MNYONGENI ILA HAKI YAKE MPENI,RAISI LEO TUMPONGEZE

MFANYAKAZI AKISTAAFU,AKIACHA AU KUACHISHWA KAZI,APEWE CHAKE AKAFE NACHO,SIO KUMUWEKEA MAKANUNI YA OVYO OVYO
 
Mwaka 2012 Sister Irene +(Dau) wa SSRA alikazania sana jambo hili kama leo alivyoshupalia lakini wenzie macho yao yote yalikuwa kwenye mwaka 2015 na mwisho wa siku ikaahirishwa na watu wakalamba, leo hoja ikiwa ni ileile, Irene yule yule wa SSRA, Waziri huyo huyo na wenzie ni hao hao wanaosubiria 2020 kwa dukuduku lao moyoni... na leo ngoma imeahirishwa tena hadi 2023, Angalizo ni kuwa Irene anaweza kustaafu akaacha mambo yakiwa hivyo hivyo kwani interest zake ni tofauti na za wenzie
 
JPM "nimeamua kila mfuko utumie kikokotoo chake cha Awali.....kiendelee ktk hichi kipindi cha mpito hadi 2023"

"Kustaafu siyo dhambi Ni heshima Nimeamua kuwa kikotoo cha awali ambacho ni 50% kiendelee kutumika kipindi cha mpito ambacho ni hadi 2023, Ambapo wanachama wa mfuko 58,000 watastaafu katika kipindi hicho,hao hatutashindwa kuwalipa, Mimi nitakuwa naichungulia hii mifuko kweli kweli ili kuzilinda hizi fedha za hawa wanachama,Saa ingine hi mifuko inawasemea wanachama,wakati wa shida zao haikuwasemea Hadi kufikia 2023 tuje na best formula" Amesema Mhe, Rais Magufuli Dec 28,2018.
 
Mh, Rais John Pombe Magufuri ametigua kitendawili hicho baada ya kusema kila mfuko uendelee na kanuni yake ya kikokotoo kwa wastaafu mpaka mwaka 2023. Pia ametoa maelekezo yafuatayo kwa mifuko ya hifadhi ya jamii

1). Kuhakikisha hakuna wastaafu hewa kwenye daftari la wastaafu.

2). Mifuko ya jamii kupunguza matumizi yasiyo na tija. Mfano kuchapisha kalenda na kujenga vitega uchumi visivyo leta faida.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikua anapima upepo, kaona mambo magumu kaamua kutoa watu kafara... JIWE bwana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG-20181228-WA0014.jpeg

Kama heading inayosema.

............itaendelea hivi punde
 
😀 utaona humu wanavyopita na mapambio yao ya ashurukuriwe mtukufu
 
hizo zinaitwa political calculations. tuliosoma political science tunajua spin hizo!!
kabla hawatangaza walipmpelekea akabariki!
leo kageuka mpaka 2013
Means 2020 kura zake anazo toka kwa wafanyakazi
Then anamwachia msala wa 2025 - kama kigezo cha kampeni!! hehe
chezea siasa!
 
Back
Top Bottom