Tafakuri
Ukiona Mzazi wako anapenda kutengeneza tatizo kisha analitatua yeye mwenyewe, tena kwa kujifanya kwamba tatizo hilo limemuuma na anawajibika kulitatua yeye kwa sababu ana upendo sana, watoto mnatakiwa kuwa makini sana na vyanzo vya matatizo yenu katika familia.
Mosi, kama ikitokea kwamba tatizo lolote yeye hakulisababisha lazima Mtoto utawajibishwa tu tena bila huruma. Pili, Mzazi wenu akiwa ana tabia hizo mjue ni mpenda sifa kwelikweli. Tatu, ataendelea kutumia njia hiyohiyo ya kuanzisha matatizo na kuyatatua endapo watoto mtapiga kelele nyingi. Mkinyamaza mjue kwamba itakula kwenu na mtaumia kwelikweli.
Suluhisho Mzazi wenu akikosea mwambieni mapema kwamba, hili tatizo chanzo chake ni hiki, lakini kamwe hawezi kukiri kwamba yeye ndo kasababisha. Akijirudi ni kushukuru maana katambua alipokosea japo hataki kukiri kosa.
#LeaveUrLegacy
Simon Ngusa Jilala