Sheria iliyopitishwa na Bunge yaani kwa kimombo inaitwa Act ukitaka kuibadilisha lazima upeleke Muswada Bungeni ujadiriwe then kupitishwa kuwa sheria baada ya kusainiwa na Rais. Lakini Kanuni inatungwa na kupitishwa na Waziri ambaye pia ana mamlaka ya kuibadirisha wakati wowote. Hivyo leo kilichofanyika ni kuifuta kanuni iliyotungwa na kupitishwa na waziri na badala yake ikabaki kanuni ya awaliSheria huambatana na kanuni za jinsi ya kuitekeleza pamoja na vifungu vya adhabu kwa watakaoivunja. Swali langu, kama sheria ile aliisaini kwa maana kuwa itumike, ni sahihi kuitengua kwa tamko badala ya kuirudisha bungeni kufanyiwa amendment? Hebu fafanua hapa kidogo kwa faida ya wengine wenye shaka!