Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Rais Magufuli afanya Mabadiliko ya teuzi, amteua Mhandisi Mwita kuwa RC Njombe

Wale Wataalamu wa Nyota... hivi huu ndo Mwezi Mchanga, au ni Upepo wa Kusi?! Hoyaa Mshana Jr, hivi huku kwenye mambo ya Mwezi Mchanga huna utalaamu nako?!

Kule Uswahilini kwetu nasikia kuna kitu kinaitwa kipaipai! Nasikia watalaamu wa kipaipai huwa wanafunga kikaratasi kwenye mti!! Sasa ngoja pepo la kusi lianze kupeperusha kikaratasi huku na huko constantly!!!

Ndo hapo unakuta jamaa mmekaa mnapiga nae stori, mara anainuka huyoo, mbele kidogo mara anasimama na kurudi alikotoka kabla hajabadili tena njia kueelekea upande mwingine... ni mwendo wa kufuata mwelekeo wa kikaratasi hadi Kusi lipite!!

Halafu hata sijui nilitaka kusema nini hasa hapo... cjui na mimi ndo Pepo la Kusi lenyewe!!!

Ila tuache masihara... Watanzania tuweke siasa pembeni tukisake hicho kikaratasi kwa udi na uvumba kabla hamjasikia Bashite kateuliwa kuwa RPC Kanda Maalumu ya Kinondoni!!

Nimecheka Sana......halafu kwa nguvu
 
Aachwe afanye kazi yake Raisi wa nchi, wewe fanya zako! Unajua je mteuliwa wa kwanza kakiri hatapaweza? Ni bora kukubali kuwa huwezi kuliko kukimbilia cheo usichokuwa na uzoefu nacho halafu ukachafuke. Mimi namsifu!
 
Kabla ya juzi mkuu wa mkoa wa Njombe alikuwa Ole Sendeka, juzi akawa Jumanne Fikha, leo Mwita Rubya!

Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais, kwa sasa aachane na haya mambo ya kutumbua na kuteuateua, afanye mambo mengine. Hayana faida yoyote kwa sisi wananchi, tumeshayachoka.
Hivi Jumanne Fikha alikuwa ameshaapishwa?? Au ni juu kwa juu??
 
Nimecheka Sana......halafu kwa nguvu
Hapo ulipokuwa hawakukutimua lakini kwamba unawapigia kelele?! All in all, itakuwa nimepatia kuhusu Pepo la Kusi kutaka kutuharibia mpendwa wetu, si eti!?
 
Back
Top Bottom