Mtume Muhamadi alishaitawala kwa haki Madina huku yeye akiwa ndiye waumini wachache ktk huo mji, hili ni swala la kitaifa. Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, hiyo sumu itageuka maziwa na asali kwa uwezo wa Allah, Mungu wa wote na mwenye kurehemu fadhila nyinginyingi kubwa na ndogo, haswa kama aliyefanya uteuzi huo aliufanya kwa kuzingatia vigezo vya kufanikisha majukumu husika, ulitaka balozi wa Vatican awe Ramadhani na Saudia awe John ? Hata hii nchi ingekuwa ni kampuni yako binafsi ungefanya hivyo. Vipi kuhusu misimamo ya nchi, mtu binafsi na nchi anakokwenda ? Nadhani kuna mengi yanayozingatiwa hapo. Halafu hao wote wanaweza wakawa ni waumini wa dini moja tu eidha waislamu au wakristo au wote hawana hata dini, wazazi wao tu waliwapatia hayo majina na wenyewe hata hawayataki.