Rais Magufuli afungua Kiwanda cha Kukoboa Mpunga Morogoro. Amlaumu Mbunge Abood kwa kuua ajira Mjini Morogoro

Rais Magufuli afungua Kiwanda cha Kukoboa Mpunga Morogoro. Amlaumu Mbunge Abood kwa kuua ajira Mjini Morogoro

Huku kwetu tunasema ameenda kuzindua "mashine ya kukoboa", sio kiwanda. Ukisema kiwanda utafanya ionekane ni kitu kukubwa sana.
Issue ya viwanda ishabuma hiyo.Watazindua hata karakana ya kukarabati baiskeli waite kiwanda!Kuchamba kwingi!
 
Mbona kiwanda cha tumbaku kimetelekezwa na kiwanda cha mazava vimetelekezwa.vyote vinazoa ajira ya watu 7,000.myonge myongeni haki yake mpeni.
 
Rais Magufuli amefungua kiwanda cha kukoboa mpunga Kihonda Morogoro.

Rais Magufuli amempongeza mwekezaji wa Kiwanda hicho na kumlaumu mbunge wa Morogoro mjini mh Abood kwa kupewa viwanda viwili na Serikali na yeye badala ya kuviendeleza akavitumia kukopea benki na kununua mabasi.

Rais Magufuli amewataka wawekezaji kuitendea haki nchi hii.

Maendeleo hayana vyama?
Mashine za kukoboa mpunga tunaziita viwanda?! Ndio maana tumeweza kujenga “viwanda “ 8,000 ndani ya miaka mitano.
 
Kupatwa kwa Tanzania kunashuhudiwa kwa kiasi cha kutosha kabisa
 
Rais Magufuli amefungua kiwanda cha kukoboa mpunga Kihonda Morogoro.

Rais Magufuli amempongeza mwekezaji wa Kiwanda hicho na kumlaumu mbunge wa Morogoro mjini mh Abood kwa kupewa viwanda viwili na Serikali na yeye badala ya kuviendeleza akavitumia kukopea benki na kununua mabasi.

Rais Magufuli amewataka wawekezaji kuitendea haki nchi hii.

Maendeleo hayana vyama?
Sijui siku ile Radio na TV za Abood zilitangaza nini kwenye taarifa ya habari maana 75% ya hotuba ilikuwa masimango kwake 😅 🤣
 
Mnatekeleza ilani ya ccm huku rais anamshutumu mbunge wa ccm aliyechaguliwa miezi michache iliyopita kuwa anaua ajira! Ifahamike huyo mbunge ana zaidi ya miaka 10 kwenye hilo jimbo,kama sio utapeli wa mchana kweupe ni nini?
Kwani ni jukumu la mbunge kuajiri,hata hivyo yeye mkuu mbona kasimamisha ajira?.
Na juzi aliwambia Magereza wasahau ajira labda wawape ajira hizo wafungwa.
 
Kwani ni jukumu la mbunge kuajiri,hata hivyo yeye mkuu mbona kasimamisha ajira?.
Na juzi aliwambia Magereza wasahau ajira labda wawape ajira hizo wafungwa.

Seems you get me wrong.
 
LAKINI SI YEYE ALIMPITISHA DODOMA , HAYA HATA KAMA HAKUMTAKA ALIMSHUHUDIA AKIFANYA DHULUMA KWA KUHAKIIKISHA ANATUMIA MABAVU DHIDI YA YULE MAMA WA CHADEMA ......KAMA KWELI ALIKUWA HAMTAKI SI ANGEACHA UCHAGUZI UWE HAKI HAKI ..
 
Leo Nimekuja Hapa Ningekuta Hajaandika Kibao Cha Soko
Ningechukua Kibao Mimi Mwenyewe Nikaandika
"Soko Kuu La Kingaru Morogoro "
Halafu Ningekipandisha Kibao Pale Juu, Halafu Viongozi Wote Wangepoteza Kazi. Mimi Siogopi Ningemkufuza Kazi, RC,RAS,DED, Mpaka Mtendaji Wa Kijiji

Wanaotafuta Kazi Ni Wengi Sana, Hawa Watendaji Maneno Mengi Vitendo Hakuna.

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
2021 Morogoro
 
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji2][emoji1][emoji8][emoji2][emoji1787][emoji23][emoji16][emoji16][emoji28][emoji1][emoji2]
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom