Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Hapo yatajazana kuulizia nyongeza ya mshahara, hii kada sjui Kwa nn tu, ina member wenye low IQ sana. Bora ukauze maembe kuliko kuwa mwalimu.

Wewe nawe unajiona una IQ kubwa kumbe hata kwenye kisoda tu haijai! Kwa hiyo unataka waulizie kuhusu maisha yako wewe na familia yako kama mnakula walau milo mitatu kwa siku, au?

Ujuaji mwingi kumbe kiazi tu! Ungekuwa unaelewa maana ya Working Class usingeandika huu ugoro wako. Unategemea Mfanyakazi anaye endesha maisha yake kwa kutegemea mshahara aombe nini kutoka kwa Mwajiri wake zaidi ya hiyo nyongeza ya mshahara, kupandishwa madaraja, mazingira bora ya kufanyia kazi, mafao yao kutoka kwa wakati, nk?

By the way, kuna mtu amekuzuia kuuza hayo maembe yako? Na mwisho wa siku atakaye kuja kuyanunua hayo ni maskini mwenzako au ni huyo huyo mwalimu?
 
Mkuu chukua hao wanafunzi,ambapo ikama inasema kuwa kila mwalimu ahudumie watoto 45 , kwa idadi hiyo ya watoto 250 ukigawanya kwa walimu 6 unakuta kila mwalimu anapaswa kuhudumia watoto 41 ,kwa ikama inavyotaka utagundua kuwa walimu katika shule hiyo wamezidi na wanapaswa kupungua ili ikama ya idadi ya watoto 45 izingatiwe.

Kwa huo mfano ulioutoa ngoja na Mimi nikupe wa kwangu,hapa ninapofundisha Mimi shule yangu ina watoto 320 na idadi ya walimu 24, ikiangalia ikama na idadi ya vipindi unakuta kila mwalimu anahudumia watoto 13, na kwa mwalimu mwenyewe vipindi vingi kwa shule hii ni vipindi 12 ,wakati ikama inataka kila mwalimu awe na vipindi 24 kwa mwezi,huoni hapa kuwa kuna ziada ya walimu zaidi ya 5-9?

Sent using Jamii Forums mobile app
Taja hiyo shule iko wapi inaitwaje unajua nyie kwa propaganda za kupotosha hamjambo
 
Mkuu chukua hao wanafunzi,ambapo ikama inasema kuwa kila mwalimu ahudumie watoto 45 , kwa idadi hiyo ya watoto 250 ukigawanya kwa walimu 6 unakuta kila mwalimu anapaswa kuhudumia watoto 41 ,kwa ikama inavyotaka utagundua kuwa walimu katika shule hiyo wamezidi na wanapaswa kupungua ili ikama ya idadi ya watoto 45 izingatiwe.

Kwa huo mfano ulioutoa ngoja na Mimi nikupe wa kwangu,hapa ninapofundisha Mimi shule yangu ina watoto 320 na idadi ya walimu 24, ikiangalia ikama na idadi ya vipindi unakuta kila mwalimu anahudumia watoto 13, na kwa mwalimu mwenyewe vipindi vingi kwa shule hii ni vipindi 12 ,wakati ikama inataka kila mwalimu awe na vipindi 24 kwa mwezi,huoni hapa kuwa kuna ziada ya walimu zaidi ya 5-9?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna shule inao walimu 4 na wanafunzi zaidi ya 800 Lakini ukienda hapo ukimuliza mwalimu changamoto za shuleni hapo atakwambia mambo ya madawati, nyumba za walimu na blah blah kama hizo

Kitu nilichogundua walimu awapendani na hii kitu serikali wanaitumia ipasavyo...umoja kati ya walimu ni sifuri hata walio kituo kimoja.
 
Hao waalimu unaowakashfu hapa ndio waliokufanya Leo ujione mjanja nyuma ya keyboard.

Wengine hao waalimu ni baba, mama na ndugu zetu na hata tunaosoma huu ujumbe wako ni waalimu. Wewe katika elimu yako kuna shule hukufundishwa na hawa waalimu unaowaita mialimu?

Nyie nyumbu pingapinga Fc ndo mnafanya wananchi wanaichukia chadema maana mkisikia Magufuli anafanya hata jambo la kawaida tu lazima mpinge.

Sent using Jamii Forums mobile app

Uko sahihi kabisa. Hii nchi ina baadhi ya Watanzania wajinga sana. Hata umchukie Magufuli kiasi gani, mwisho wa siku yeye ndiye Rais wa Tanzania! Kumchukia hakuwezi kuleta tija yoyote ile kwenye maisha yetu ya kawaida ya kila siku, zaidi tu ya kuongeza msongo wa mawazo.

Wafanyakazi tunataka unafuu wa maisha. Huo ndiyo ukweli. Leo hii wasipomualika Magufuli ili atie neno, ni nani mwenye hiyo nguvu ya kuboresha stahiki za Wafanyakazi kama siyo Rais?

Mimi kama Mfanyakazi wa Nchi hii, naunga mkono hao CWT kumualika Rais! Nina imani walau mwaka huu atatekeleza baadhi ya ahadi zake. Simuungi mkono kwenye baadhi ya uonevu anaowafanyia Wafanyakazi! Lakini hakuna namna, maisha lazima yaendelee.
 
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
M
Kuna shule inao walimu 4 na wanafunzi zaidi ya 800 Lakini ukienda hapo ukimuliza mwalimu changamoto za shuleni hapo atakwambia mambo ya madawati, nyumba za walimu na blah blah kama hizo

Kitu nilichogundua walimu awapendani na hii kitu serikali wanaitumia ipasavyo...umoja kati ya walimu ni sifuri hata walio kituo kimoja.
Mkuu uko sahihi, hata jpm, majaliwa, jenista Ni walimu.lakini wamewatupa sana walimu awamu hii
 
Ccm Hoyee Ccm Hoyee
Chama Cha Walimu Zii 😏🙄🤣😃
 
Salaam Wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania-CWT.

Mkutano huo utafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, huku watu wote wakitakiwa kuzingatia na kuchukua tahadhari za kujikinga na Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Tayari, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru, Mkoa wa Dodoma, imetangaza kuwa itashughulika na watu watakaojihusisha na vitendo vya rushwa katika Uchaguzi huo.

Nitawaletea Updates kwa kila kitakachojiri.

Karibuni.

===
UPDATES:

Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako, Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa mingine na viongozi wengine wengi.

Tayari M.h Rais Magufuli ameshawasili katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambaye tayari kwa ajili ya kuja kufungua Mkutano huu wa Chama cha Waalimu Tanzania ambapo amefika na kuwasalimia na kuwapungia mkono Waalimu wote waliohudhuria.

Wimbo wa Taifa unaimbwa kabla ya Rais kuketi na kufungua mkutano huu.

Kabla ya kukaribishwa Mh. Rais kuzungumza Mkutano huu umeanza kwa maombi kutoka kwa Sheikh na Mchungaji Davidi kalinga ambao wameanza kwa maombi kwa kumshukuru Mungu kisha kuomba amani na furaha katika mkutano huu pamoja na kumuombea Rais na viongozi wengine.

Mshereheshaji wa tukio hili ameanza kwa kuzingatia itifaki na kuwatambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano huu na kisha ameanza kusoma risala iliyoandaliwa.

Risala hii imeanza kwa kumshukuru Rais kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi mkutano huo kisha kumpongeza rais kwa miradi mbalimbali ambayo Rais ameitekeleza katika kipindi hiki cha miaka mitano pamoja na kuweza kulipa malimbikizo mbalimbali ya mishahara ya waalimu zaidi ya Bilioni 12.5.

Aidha, risala hiyo imebainisha changamoto ambazo waalimu wanakumbana nazo ikiwamo ukosefu wa nyumba za waalimu na pia rasala hiyo imemuomba rais kuwapandisha cheo waalimu kundi la waalimu walioajiriwa mwaka 2013/ 2014 wapandishwe cheo katika bajeti ya ya mwaka 2020/2021.
Moja ya kada ambayo ina watu wengi wa hali ya chini wasiotambua haki zao
 
Walimu wanasifia hadi kero daah....wanasema hamna haja ya nyongeza ya mshahara kwani aliyofanya magufuli Ni zaidi ya kuongeza mishahara Kweli kuliko kuwa Mwalimu Ni bora ukauze maembe
ha ha nimecheka sana
 
Mbona waalimu hawapigi makofi? Hawapendi juhudi za JPM au?
 
Back
Top Bottom