Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Rais Magufuli afungua mkutano Mkuu wa Chama cha Waalimu, Corona imeisha, Shule za Msingi kufunguliwa karibuni

Shehe kakosea kusali
Aiseh ubinadamu upo
Kataja majina matatu benjamini, Edward ndio baadae akapatia jina la John Pombe Magufuri
Maisha yanaendelea hapa viwanjani
Shehe ubwabwa katika ubora wake
 
Woote mnaopinga JPM kualikwa je mlipenda nani ndio aalikwe ?

Walimu wamechagua upande wao mapema, mlijitahidi kumfitinisha magufuli na walimu mwisho wa siku walimu wameamua kwenda na JPM
 
aisee sijui walimpitishaje no issue tokea aanze kuzungumza
 
Woote mnaopinga JPM kualikwa je mlipenda nani ndio aalikwe ?

Walimu wamechagua upande wao mapema, mlijitahidi kumfitinisha magufuli na walimu mwisho wa siku walimu wameamua kwenda na JPM
Hihihihi hiki ulichokisema ni unafiki na inaonekana hawa walimu ni makada wa CCM
 
Kuitenganisha Serikali na Chama Cha Walimu Tanzania ni sawa na kutaka Kutenganisha Ndoa ya Wawili waliokula Viapo halali Kanisani / Msikitini.
 
Mkuu Kwani ni fani ngapi watu wamesoma na hawana ajira,watu wa sheria,community deve'nt, international rela.nk ije kuwa hao walimu,?

Mkuu Serikali imesema hakuna nafasi za ualimu kwa walimu kwa sasa ,je unawataka iwaajiri wapi ikiwa hakuna nafasi?

Tuache lawama ambazo haziwezi kubadili ukweli wa mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
Waisimamishe kwa muda ili watu wadonee zenye tija.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kabisa. Hii nchi ina baadhi ya Watanzania wajinga sana. Hata umchukie Magufuli kiasi gani, mwisho wa siku yeye ndiye Rais wa Tanzania! Kumchukia hakuwezi kuleta tija yoyote ile kwenye maisha yetu ya kawaida ya kila siku, zaidi tu ya kuongeza msongo wa mawazo.

Wafanyakazi tunataka unafuu wa maisha. Huo ndiyo ukweli. Leo hii wasipomualika Magufuli ili atie neno, ni nani mwenye hiyo nguvu ya kuboresha stahiki za Wafanyakazi kama siyo Rais?

Mimi kama Mfanyakazi wa Nchi hii, naunga mkono hao CWT kumualika Rais! Nina imani walau mwaka huu atatekeleza baadhi ya ahadi zake. Simuungi mkono kwenye baadhi ya uonevu anaowafanyia Wafanyakazi! Lakini hakuna namna, maisha lazima yaendelee.
Kwa akili yako timamu unategemea kutakuwa na jipya leo?kualikwa kwa JPM na even asingealikwa there is no difference
 
Wewe nawe unajiona una IQ kubwa kumbe hata kwenye kisoda tu haijai! Kwa hiyo unataka waulizie kuhusu maisha yako wewe na familia yako kama mnakula walau milo mitatu kwa siku, au?

Ujuaji mwingi kumbe kiazi tu! Ungekuwa unaelewa maana ya Working Class usingeandika huu ugoro wako. Unategemea Mfanyakazi anaye endesha maisha yake kwa kutegemea mshahara aombe nini kutoka kwa Mwajiri wake zaidi ya hiyo nyongeza ya mshahara, kupandishwa madaraja, mazingira bora ya kufanyia kazi, mafao yao kutoka kwa wakati, nk?

By the way, kuna mtu amekuzuia kuuza hayo maembe yako? Na mwisho wa siku atakaye kuja kuyanunua hayo ni maskini mwenzako au ni huyo huyo mwalimu?
Mkuu kuna binadamu kwenye ubongo wao kuna maji machafu.
 
Hao waalimu unaowakashfu hapa ndio waliokufanya Leo ujione mjanja nyuma ya keyboard.

Wengine hao waalimu ni baba, mama na ndugu zetu na hata tunaosoma huu ujumbe wako ni waalimu. Wewe katika elimu yako kuna shule hukufundishwa na hawa waalimu unaowaita mialimu?

Nyie nyumbu pingapinga Fc ndo mnafanya wananchi wanaichukia chadema maana mkisikia Magufuli anafanya hata jambo la kawaida tu lazima mpinge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Je, kama kajifunza mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom