Madawa kibao mahospitalini mpaka maArvs tunayopewa kwa msaada yanatoka kwa mabeberu. Wakitaka kutumaliza kwanini wahangaike na barakoa?Kuanzia Dream liner, Bombadia, mpaka zile VX na Helicopter anazotumia Magufuli zimetengenezwa na mabeberu na zikisumbia tu ni mabeberu hao hao wanaitwa kuzirekebisha. Sijui ni kwanini Magufuli hazilitii mashaka na badala yake anapotosha watanzania kuhusu Barakoa na Chanjo?
Farao ana matatizo makubwa kichwani.
Hao wasaidizi ndio walitumia nguvu nyingi kuhakikisha anakuwa mtawala bila ridhaa ya wenyenchi wananchi.Anasema watu wanakufa kwa mipango ya Mungu. Anajivua lawama kwamba hata watu wafe wangapi yeye hahusiki, hana uwezo wala jukumu la kuzuia hilo.
Ana uwezo mdogo sana wa kufikiri na anawapa kazi sana wasaidizi wake. Nahisi wameamua wamuache tu!
Moshi Meya Juma Rabia tume muweka kwenye listAisee. Iv ni wap kule watu walivuliwa barakoa
Huo ni ukosefu wa maarifa@britannica,
..labda anaamini kwa dhati kabisa kwamba "mabeberu" wanaweza kupandikiza covid-19 kwenye barakoa na kuzileta Tanzania ili watuuwe.
Mkuu unashindwa kuelewa jambo dogo sana..., Hii Sentensi ya kwamba Serikali haina Dini ina manufaa sana hususan kwa nchi ambayo ina waumini wa dini mbalimbali... (usiangalie nchi gani inafanya nini au nani alifanya nini) bali angalia kwa jicho la kuunganisha watu...Muulize Mhe. Butiku kama unashida ya kupata ushahidi. Pia nitajie sheria yoyote inayozuia Rais kuongelea mambo ya sera au jamii ndani ya kanisa. Pia sijaongea kuwa Nyerere alikuwa mzee wa kanisa kijijini. Hilo umesema wewe. Na ibada hiyo haikufanyika Butiama, bali Musoma mjini. Nipatie ushahidi wa kitaalamu unaozuia Rais kuongea kanisani.
Nilichoongelea mimi ni mahusiano ya kanisa na siasa. Kasome kozi ya Pilitics and Religion utaelewa. Hata katiba yetu haijakataza Rais kuongea kanisani au sheria yoyote ile. Ingekuwa hivyo Rais asingekuwa anatumia Biblia au Kuruani kuapa mbele ya jumuia. Bunge lisingeanza kwa Sala. Uwezi tenganisha hivi vitu. Hata siasa imeanza kwa mfumo wa kidini. Ndo maana ukisoma maandiko Neno la Mungu linasema Viongozi wa nchi (Kisiasa) uwekwa na MUNGU mwenyewe. Japo tunapiga kura lakini Mungu ni Mwamuzi. Karibu nchi zote duniani washauri wa watawala wengi ni viongozi wa dini.
Huo ni ukosefu wa maarifa
We jamaa nimekupenda bure. Nilichojifunza kwa watanzania ni uhuru mwingi wa kupitiliza afu kila mtu anadhani yeye anajua kuliko wengine.mhe.rais ni kiongozi wetu na amesema wazi kwamba yeye anataarifa nyingi kuliko sisi wote.anavyombo vingi vya kumpa taarifa ata kutoka kwenye mataifa mengine. Wewe ni nani mpaka unamdaharau mhe rais .Shida yenu hampendi kuambiwa ukweli, barakoa ziliingizwa nyingi sana kipindi cha mwaka jana, na baada ya serikali kugundua hilo walianza kuzuia baadhi ya barakoa zinaonekana zina walakini, na ndio maana kuna kipindi surgical mask zilikuwa adimu hadi mahospitalini kiasi kwamba madaktari walianza kulalamika. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, MSD walifanya dharura ya kujenga kiwanda cha kuzalisha barakoa za mahospitalini (surgical mask) amabapo kimeanza full production mwezi wa tisa mwaka jana.
Kuhusu dawa za asili nadhani wewe una tatizo kichwani na pengine unachanganya uchawi na dawa za asili. Aliyekuambia dawa za asili nazo si sayansi ni nani? Tofauti ya dawa za asili na hizi za kawaidi ni matumizi ya kemikali. Halafu hata hizo dawa za asili nazo ni sayansi pia, kwani wanachofanya NIMR ni nini kama siyo sayansi?
Halafu kosa ni lipi kwa yeye Rais kutaja dawa ili wananchi wazitumie wapone? Yeye kataja zile ambazo serikali imethibitisha zinafanya kazi, na wananchi wana haki ya kuzijua ili wazitumie wapone, sasa ulitaka afiche ili kiwe nini? Au mleta mada una dawa yako ambayo imeshindwa kuthibitishwa ubora wake hivyo unaona wivu kutajwa dawa zingine?
Pia viongozi wa dini kama binadamu wengine wanachambwa kama kawaida pale wanapokosea. Aliyekuambia kiongozi wa dini hakosolewi basi alikudanganya sana. Unzuri wa Magufuli anakupa za uso hapo hapo hajali wewe ni nani. Ni lazima tuambiane ukweli ili tuweze kubadilika.
Kingine, anachofanya Magufuli si mahubiri, mahubiri ya Kanisa katoliki yanafanywa kabla ya kutoa sadaka baada tu ya somo la Injili ambapo huwa ni katikati ya ibada au misa. Muda anaosimama Magufuli ni muda wa matangazo ambapo misa au ibada inakuwa imeisha. So usichanganye hivyo vitu, kanisa katoliki lina utaratibu wake, na ibada au misa zina miongozo yake ya kufuata.
Umeamua kutokuelewa tul, mbona Rais anaeleweka vizuri tu. Anatoa tahadhari ya barakoa za nje. Rais ana taarifa nyingi tumwamini!Kupitia hii Video nimeona mkangamyiko, alimkataza Spika kuvaa Barakoa
Walivyo sema serikali haina dini, ilikuwa kuwa tofauti na kidogo na nchi za Mataifa ya nje ambayo yalitutawala. Kwani yote yaliongozwa kwa mfumo wa dini, si tu dini bali dhehebu. Mfano Sweden, Ujerumani wao walikuwa Waromani baada ya Mageuzi ya Martin Luther watawala wa nchi hizo waliamua nchi zao ziwe za Kirutheri. Nyerere aliposhika madaraka akasema serikali haina dini. Hii ilimaanisha zaidi kutokuwa na kanisa au kutokuwa na imani ya Uislamu itakayo ongoza Taifa. Hii ndo maana ya serikali haina dini. Ila serikali inaamini Mungu yupo na watu wake wanadini.Mkuu unashindwa kuelewa jambo dogo sana..., Hii Sentensi ya kwamba Serikali haina Dini ina manufaa sana hususan kwa nchi ambayo ina waumini wa dini mbalimbali... (usiangalie nchi gani inafanya nini au nani alifanya nini) bali angalia kwa jicho la kuunganisha watu...
Kila mtu akiwa na freedom ya kuamini / Kuabudu kwa nafasi yake na kiongozi kufanya hayo kama personal issue na sio issue ya kitaifa kunaondoa ile nadharia kwamba nchi/ fulani anapendelea dini yake..., Binadamu tunatafuta sababu ndogo tu ya kupigana..., ukishaweka mwanya wa sisi na wao unakuwa haujengi..., Imani yako huenda isiwe sawa na yangu (ni vigumu kuongelea kodi zetu tujenge msikiti, kanisa, hekalu au tutoe sadaka kwa mizimu) hilo haliwahusu wote..., ila mambo yanayohusu wote ni ya wote..., hivyo mtu akizungumza na taifa / kuhusu taifa ni vema akaongea / akaongelea audience yote ila kama ni issue inayohusu labda walevi anaweza kuiongelea Bar..., wengine wanaenda kanisani kupata neno sio kusikiliza Siasa....
Kwani kura zina uhusiano gani na barakoa?Nabado atapagawa sana,wao si waliiba Kura zetu
Mkuu ulimchanja Biden hiyo chanjo wewe. Anaweza kupiga hata juice tu ili RAIA waumini.Barakoa zina corona,chanjo ina madhara makubwa ikiwemo kuwafanya wanawake wagumba na wanaume mazezeta, social distance ni njia ya kutuletea hofu na kufanya tusizaliane hakuna corona ni magonjwa ya kawaida ya changamoto ya kupumua(serikali).
Wataam wa afya na vyombo vya dini 'corona ipo tuchukue tahadhari za kuvaa barakoa,social distance na kufwata ushauri wa wataalam wa afya'.
Hivi hii chanjo aliyo chanjwa biden,Obama,prince Philip,Queen Elizabeth, Putin na viongozi wengine wakubwa ndiyo iyo tunaambiwa si salama?. Tujaribu kuwaza tu hyprocratic politicians kama yule anaye vaa tai ya taifa,yule prof wa jalalani ni kweli hawajapigwa chanjo hadi muda huu?.
Umeulizwa swali badala ya kujibu unamwambia Kiranga amtafute Mzee Butiku amuulize?Muulize Mhe. Butiku kama unashida ya kupata ushahidi. Pia nitajie sheria yoyote inayozuia Rais kuongelea mambo ya sera au jamii ndani ya kanisa. Pia sijaongea kuwa Nyerere alikuwa mzee wa kanisa kijijini. Hilo umesema wewe. Na ibada hiyo haikufanyika Butiama, bali Musoma mjini. Nipatie ushahidi wa kitaalamu unaozuia Rais kuongea kanisani.
Nilichoongelea mimi ni mahusiano ya kanisa na siasa. Kasome kozi ya Pilitics and Religion utaelewa. Hata katiba yetu haijakataza Rais kuongea kanisani au sheria yoyote ile. Ingekuwa hivyo Rais asingekuwa anatumia Biblia au Kuruani kuapa mbele ya jumuia. Bunge lisingeanza kwa Sala. Uwezi tenganisha hivi vitu.
Hata siasa imeanza kwa mfumo wa kidini. Ndo maana ukisoma maandiko Neno la Mungu linasema Viongozi wa nchi (Kisiasa) uwekwa na MUNGU mwenyewe. Japo tunapiga kura lakini Mungu ni Mwamuzi. Karibu nchi zote duniani washauri wa watawala wengi ni viongozi wa dini.
No relation,naamin Tu huu ni mwanzo wa malipo Kwa waliyo tutendea