Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Kuanzia Dream liner, Bombadia, mpaka zile VX na Helicopter anazotumia Magufuli zimetengenezwa na mabeberu na zikisumbia tu ni mabeberu hao hao wanaitwa kuzirekebisha. Sijui ni kwanini Magufuli hazilitii mashaka na badala yake anapotosha watanzania kuhusu Barakoa na Chanjo?

Farao ana matatizo makubwa kichwani.
Madawa kibao mahospitalini mpaka maArvs tunayopewa kwa msaada yanatoka kwa mabeberu. Wakitaka kutumaliza kwanini wahangaike na barakoa?

Mambo mengine hayahitaji kwenda darasa la pili kujua safari hii tumempata Rais wa ajabu sana...
 
Anasema watu wanakufa kwa mipango ya Mungu. Anajivua lawama kwamba hata watu wafe wangapi yeye hahusiki, hana uwezo wala jukumu la kuzuia hilo.

Ana uwezo mdogo sana wa kufikiri na anawapa kazi sana wasaidizi wake. Nahisi wameamua wamuache tu!
Hao wasaidizi ndio walitumia nguvu nyingi kuhakikisha anakuwa mtawala bila ridhaa ya wenyenchi wananchi.
 
Muulize Mhe. Butiku kama unashida ya kupata ushahidi. Pia nitajie sheria yoyote inayozuia Rais kuongelea mambo ya sera au jamii ndani ya kanisa. Pia sijaongea kuwa Nyerere alikuwa mzee wa kanisa kijijini. Hilo umesema wewe. Na ibada hiyo haikufanyika Butiama, bali Musoma mjini. Nipatie ushahidi wa kitaalamu unaozuia Rais kuongea kanisani.
Nilichoongelea mimi ni mahusiano ya kanisa na siasa. Kasome kozi ya Pilitics and Religion utaelewa. Hata katiba yetu haijakataza Rais kuongea kanisani au sheria yoyote ile. Ingekuwa hivyo Rais asingekuwa anatumia Biblia au Kuruani kuapa mbele ya jumuia. Bunge lisingeanza kwa Sala. Uwezi tenganisha hivi vitu. Hata siasa imeanza kwa mfumo wa kidini. Ndo maana ukisoma maandiko Neno la Mungu linasema Viongozi wa nchi (Kisiasa) uwekwa na MUNGU mwenyewe. Japo tunapiga kura lakini Mungu ni Mwamuzi. Karibu nchi zote duniani washauri wa watawala wengi ni viongozi wa dini.
Mkuu unashindwa kuelewa jambo dogo sana..., Hii Sentensi ya kwamba Serikali haina Dini ina manufaa sana hususan kwa nchi ambayo ina waumini wa dini mbalimbali... (usiangalie nchi gani inafanya nini au nani alifanya nini) bali angalia kwa jicho la kuunganisha watu...

Kila mtu akiwa na freedom ya kuamini / Kuabudu kwa nafasi yake na kiongozi kufanya hayo kama personal issue na sio issue ya kitaifa kunaondoa ile nadharia kwamba nchi/ fulani anapendelea dini yake..., Binadamu tunatafuta sababu ndogo tu ya kupigana..., ukishaweka mwanya wa sisi na wao unakuwa haujengi..., Imani yako huenda isiwe sawa na yangu (ni vigumu kuongelea kodi zetu tujenge msikiti, kanisa, hekalu au tutoe sadaka kwa mizimu) hilo haliwahusu wote..., ila mambo yanayohusu wote ni ya wote..., hivyo mtu akizungumza na taifa / kuhusu taifa ni vema akaongea / akaongelea audience yote ila kama ni issue inayohusu labda walevi anaweza kuiongelea Bar..., wengine wanaenda kanisani kupata neno sio kusikiliza Siasa....
 
Huo ni ukosefu wa maarifa

..bila shaka ana matatizo na barakoa.

..but where does he get his information from?

..Na ana tabia mbaya ya kusema UONGO, na kupotosha kauli za wenzake, na kuwakejeli.
 
Shida yenu hampendi kuambiwa ukweli, barakoa ziliingizwa nyingi sana kipindi cha mwaka jana, na baada ya serikali kugundua hilo walianza kuzuia baadhi ya barakoa zinaonekana zina walakini, na ndio maana kuna kipindi surgical mask zilikuwa adimu hadi mahospitalini kiasi kwamba madaktari walianza kulalamika. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, MSD walifanya dharura ya kujenga kiwanda cha kuzalisha barakoa za mahospitalini (surgical mask) amabapo kimeanza full production mwezi wa tisa mwaka jana.

Kuhusu dawa za asili nadhani wewe una tatizo kichwani na pengine unachanganya uchawi na dawa za asili. Aliyekuambia dawa za asili nazo si sayansi ni nani? Tofauti ya dawa za asili na hizi za kawaidi ni matumizi ya kemikali. Halafu hata hizo dawa za asili nazo ni sayansi pia, kwani wanachofanya NIMR ni nini kama siyo sayansi?

Halafu kosa ni lipi kwa yeye Rais kutaja dawa ili wananchi wazitumie wapone? Yeye kataja zile ambazo serikali imethibitisha zinafanya kazi, na wananchi wana haki ya kuzijua ili wazitumie wapone, sasa ulitaka afiche ili kiwe nini? Au mleta mada una dawa yako ambayo imeshindwa kuthibitishwa ubora wake hivyo unaona wivu kutajwa dawa zingine?

Pia viongozi wa dini kama binadamu wengine wanachambwa kama kawaida pale wanapokosea. Aliyekuambia kiongozi wa dini hakosolewi basi alikudanganya sana. Unzuri wa Magufuli anakupa za uso hapo hapo hajali wewe ni nani. Ni lazima tuambiane ukweli ili tuweze kubadilika.

Kingine, anachofanya Magufuli si mahubiri, mahubiri ya Kanisa katoliki yanafanywa kabla ya kutoa sadaka baada tu ya somo la Injili ambapo huwa ni katikati ya ibada au misa. Muda anaosimama Magufuli ni muda wa matangazo ambapo misa au ibada inakuwa imeisha. So usichanganye hivyo vitu, kanisa katoliki lina utaratibu wake, na ibada au misa zina miongozo yake ya kufuata.
We jamaa nimekupenda bure. Nilichojifunza kwa watanzania ni uhuru mwingi wa kupitiliza afu kila mtu anadhani yeye anajua kuliko wengine.mhe.rais ni kiongozi wetu na amesema wazi kwamba yeye anataarifa nyingi kuliko sisi wote.anavyombo vingi vya kumpa taarifa ata kutoka kwenye mataifa mengine. Wewe ni nani mpaka unamdaharau mhe rais .

Lakin pia nimepitia michango ya watu humu kuna mtu anasema ata bila aibu eti malikia wa Uingereza na marais wengine wamechanjwa hiyo chanjo ya pfizer na nyinginezo wakati taarifa zilionesha kwamba hao watu hawakuchanjwa walifanya udanganyifu wa kukusanya vyombo vya habari na kujifanya wanachanjwa wakati sindano zikioneshwa kwa siri kwamba zimefungwa kwenye ncha.

Lakini pia hizi chanjo zinamadhara kwa watu weusi wa marekani japo hawasemi wanaficha.kunawatu wamechanjwa a wamekufa.south africa wamekataa chanjo kwasababu wanasayansi wamevundua kwamba sio effective kwa kirusi kipya kilichoundergo mutation,mara kimeshakuwa covid 21 watanzania wanajifanya wao ni wanasayansi kuliko mhe rais ambaye walau ana phd ya sayansi.

Pia chanjo hizo za europe zimetengenezwa kwa genetic engenering madhara yake yanakuwa kwenye gene maana yake watu wasipokuwa makin waafrica wa miaka ijayo hawatakuwa waafrica wa leo. Madhara ya genetics ni ya vizazi na vizazi watu hawaweze kuelewa ilo.

China na urus wametengenez chanjo ila wakubwa wa dunia wako wanapigana vikumbo kutoidhinisha izo chanjo na wanataka ziundergo review process wakati zao hizo hazijapitia hizo process.Mkila mkashiba mnaanza madharau.

WATANZANIA WENZANGU tujitafakari wakati wa kutoa maoni.
 
Kweli anajipinga mwenyewe kwa kila kitu ,ukisikiliza hotubayake leo kanisani katumia neno la kiingereza katika hotuba aliyo kuwa anaitoa kwa lugha ya kiswahili "Msini Quote vibaya" hapo kwa kujifanya anakienzi kiswahili ni zaidi ya uzandiki
 
Unamtafsiri Rais nje ya muktadha (out of context), sijajua Kama Ni kwa makusudi ili upotoshe au ni kwa ukosefu wa uelewa!

Alivyosema kufa tutakufa tu alikuwa anakumbusha ukweli wa maisha ambao haukanushiki. Si kwamba corona ndio ndio sababu pekee ya kifo, hata bila corona watu hufa! Akatsja mfano wa kanisa nk! na huo ndio ukweli.

Alikuwa anakemea hofu, na kushauri kumtegemea Mungu zaidi ya kutegemea barakoa, japo alisema serikali haijazuia barakoa.
 
Mtoa mada nadhani umetumia Uhuru wako wakutoa Maoni. Lakini ni lazima ujue kuongoza nchi sio kama kuongoza kilabu cha pombe.

Mnaweza mkamlaumu sana Ndugu Rais kwa maamuzi anayoyachukua hii ni kutokana na kuvimbiwa kwa Uhuru aliotupatia kwa kuzurura zurura bila kufungiwa ndani.

Sidhani kama mngekuwa mmefungiwa ndani nadhani mngepata Akili nakujua Madhara Yake.

Hii kitu tusijitoe ufahamu hakuna mtanzania Ambaye hajapata corona tumeishi nayo hata kabla haijagundulika. Hivyo kujidai sasa hivi tunatoapovu ni kujitoa ufahamu.

Kifo kipo siku zote utajikinga na barakoa huku malaria ukimwi sukari pressure Ajali zinaondoa uhai wa watu kila Leo. Hivyo kuitikuza corona kwamba ndio chanzo cha kifo ni ujinga wakupindukia.

Tuache kutishana Rais kama Rais ndiye kiongozi MKUU wa nchi. Hatuna makambale kila MTU anasharubu. Tuheshimu Viongozi wetu.
 
Mkuu unashindwa kuelewa jambo dogo sana..., Hii Sentensi ya kwamba Serikali haina Dini ina manufaa sana hususan kwa nchi ambayo ina waumini wa dini mbalimbali... (usiangalie nchi gani inafanya nini au nani alifanya nini) bali angalia kwa jicho la kuunganisha watu...

Kila mtu akiwa na freedom ya kuamini / Kuabudu kwa nafasi yake na kiongozi kufanya hayo kama personal issue na sio issue ya kitaifa kunaondoa ile nadharia kwamba nchi/ fulani anapendelea dini yake..., Binadamu tunatafuta sababu ndogo tu ya kupigana..., ukishaweka mwanya wa sisi na wao unakuwa haujengi..., Imani yako huenda isiwe sawa na yangu (ni vigumu kuongelea kodi zetu tujenge msikiti, kanisa, hekalu au tutoe sadaka kwa mizimu) hilo haliwahusu wote..., ila mambo yanayohusu wote ni ya wote..., hivyo mtu akizungumza na taifa / kuhusu taifa ni vema akaongea / akaongelea audience yote ila kama ni issue inayohusu labda walevi anaweza kuiongelea Bar..., wengine wanaenda kanisani kupata neno sio kusikiliza Siasa....
Walivyo sema serikali haina dini, ilikuwa kuwa tofauti na kidogo na nchi za Mataifa ya nje ambayo yalitutawala. Kwani yote yaliongozwa kwa mfumo wa dini, si tu dini bali dhehebu. Mfano Sweden, Ujerumani wao walikuwa Waromani baada ya Mageuzi ya Martin Luther watawala wa nchi hizo waliamua nchi zao ziwe za Kirutheri. Nyerere aliposhika madaraka akasema serikali haina dini. Hii ilimaanisha zaidi kutokuwa na kanisa au kutokuwa na imani ya Uislamu itakayo ongoza Taifa. Hii ndo maana ya serikali haina dini. Ila serikali inaamini Mungu yupo na watu wake wanadini.
Rais hajaongelea dini. Ameongelea mambo ya kitaifa kwa ujumla yanayowagusa wananchi wake. Ndo maana hata kanisa au uslamu wanaongelea mambo ya jamii. Mfano makanisa kadhaa yametoa waraka juu ya tahadhari za Covid 19. Uwezi tenganisha policy na kanisa. Serikali inakataza kutenda maovu, pia dini inakataza kutenda maovu. Ndini ipo kuboresha au kujenga imani ya mtu kwa Mungu wake lakini ipo pia kujenga maisha ya kijamii na huduma mbalimbali. Ndo maana dini au madhehebu yanatoa huduma za kijamii ambazo utolewa na serikali. Nenda kokote duniani uwezi tenganisha. Dini uwafunza watu maisha ya ujasiriamali, afya, elimu, na mazingira haya yote ufanywa chini ya sera za serikali.
Rais alichoongelea ni tahadhari ya kiafya kwa ujumla, hakubagua wala kuonesha maswala ya kidini. Rais ni wa wote, anapo pata nafasi ataongelea maswala ya kitaifa. Si rais wa kwanza kuhudhuria ibada. Marais wengi ufanya hivyo na ndiyo maana wakati wa sherehe za Idd kwa waislamu ualika viongozi wa kitaifa awe Rais, Makamu, hata Waziri Mkuu kuhutubia. Ili limekuwepo toka uhuru na uwa haijarishi Rais ni Mwislamu au lah! Kipindi hicho Rais uweza kutoa sadaka kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima mfano Mbuzi, mafuta ya kula, sukari na kadharika. Kwa wakristo pia wakati wa Krismas au Pasaka ualika viongozi wa kitaifa. Limekuwepo miaka yote.
Tuache chuki, hata kama tutaweka chuki yeye tayari ni Rais haito saidia. Kikubwa ni nchi yetu sote tusikae kufatilia vitu vidogovidogo visivyo jenga jamii. Tuwe wabunifu tujenge Taifa letu. Hapo ulipo jiulize umefanya nini kwa jamii. Siyo kukashifu kupinga. Hivi hata tukifa Mungu akakuuliza nilikuweka duniani nini ulifanya jibu hakuna. Tukosoe kwa kuwa na mawazo mbadala yatakayo leta ufanisi kwa jamii. Je rais kuongea vile kaathiri imani ya mtu?
Umeeongelea Kuhusu issue za kitaifa pale kaongelea issue za Taifa. Unaposema issue ikihusu ulevi ikaongelewa bar unanishitua kidogo. Mfano baba akiwa na mtoto mlevi atamchukua wakaongelee bar. Kama hatahitaji mkanya mtoto juu ya ulevi. Wazazi wengi hata akikosea mtoto mmoja. Mfano ni mlevi mara nyingi mzazi uweka kikao cha familia ili kuweka funzo kwa watoto wote. Corona ni issue ya Taifa na kimataifa, kilichoongelewa pale ilikuwa kwa manufaa ya Taifa.
Ubarikiwe,
Wasalaam Walykum!
 
Barakoa zina corona,chanjo ina madhara makubwa ikiwemo kuwafanya wanawake wagumba na wanaume mazezeta, social distance ni njia ya kutuletea hofu na kufanya tusizaliane hakuna corona ni magonjwa ya kawaida ya changamoto ya kupumua(serikali).

Wataam wa afya na vyombo vya dini 'corona ipo tuchukue tahadhari za kuvaa barakoa,social distance na kufwata ushauri wa wataalam wa afya'.

Hivi hii chanjo aliyo chanjwa biden,Obama,prince Philip,Queen Elizabeth, Putin na viongozi wengine wakubwa ndiyo iyo tunaambiwa si salama?. Tujaribu kuwaza tu hyprocratic politicians kama yule anaye vaa tai ya taifa,yule prof wa jalalani ni kweli hawajapigwa chanjo hadi muda huu?.
Mkuu ulimchanja Biden hiyo chanjo wewe. Anaweza kupiga hata juice tu ili RAIA waumini.
 
Muulize Mhe. Butiku kama unashida ya kupata ushahidi. Pia nitajie sheria yoyote inayozuia Rais kuongelea mambo ya sera au jamii ndani ya kanisa. Pia sijaongea kuwa Nyerere alikuwa mzee wa kanisa kijijini. Hilo umesema wewe. Na ibada hiyo haikufanyika Butiama, bali Musoma mjini. Nipatie ushahidi wa kitaalamu unaozuia Rais kuongea kanisani.

Nilichoongelea mimi ni mahusiano ya kanisa na siasa. Kasome kozi ya Pilitics and Religion utaelewa. Hata katiba yetu haijakataza Rais kuongea kanisani au sheria yoyote ile. Ingekuwa hivyo Rais asingekuwa anatumia Biblia au Kuruani kuapa mbele ya jumuia. Bunge lisingeanza kwa Sala. Uwezi tenganisha hivi vitu.

Hata siasa imeanza kwa mfumo wa kidini. Ndo maana ukisoma maandiko Neno la Mungu linasema Viongozi wa nchi (Kisiasa) uwekwa na MUNGU mwenyewe. Japo tunapiga kura lakini Mungu ni Mwamuzi. Karibu nchi zote duniani washauri wa watawala wengi ni viongozi wa dini.
Umeulizwa swali badala ya kujibu unamwambia Kiranga amtafute Mzee Butiku amuulize?
Inaelekea hiyo story yako ni fiction.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Naomba kufahamishwa yafuatayo;

Je barakoa za kutengeneza kienyeji za materials ya vitenge , vitambaa n.k ni salama kutumika kiafya?

Ninavyofahamu ni kuwa zile barakoa imported zimezingatia viwango fulani ambavyo ni rafiki kwa matumizi ya puani na mdomoni ktk kutumika,

Sasa Je hizi za kushonwa kienyeji zinazingatia viwango gani?

Je chemistry ya materials ya vitenge na vitambaa ni rafiki kwa matumizi ya puani na mdomoni?
 
Back
Top Bottom