Shida yenu hampendi kuambiwa ukweli, barakoa ziliingizwa nyingi sana kipindi cha mwaka jana, na baada ya serikali kugundua hilo walianza kuzuia baadhi ya barakoa zinaonekana zina walakini, na ndio maana kuna kipindi surgical mask zilikuwa adimu hadi mahospitalini kiasi kwamba madaktari walianza kulalamika. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, MSD walifanya dharura ya kujenga kiwanda cha kuzalisha barakoa za mahospitalini (surgical mask) amabapo kimeanza full production mwezi wa tisa mwaka jana.
Kuhusu dawa za asili nadhani wewe una tatizo kichwani na pengine unachanganya uchawi na dawa za asili. Aliyekuambia dawa za asili nazo si sayansi ni nani? Tofauti ya dawa za asili na hizi za kawaidi ni matumizi ya kemikali. Halafu hata hizo dawa za asili nazo ni sayansi pia, kwani wanachofanya NIMR ni nini kama siyo sayansi?
Halafu kosa ni lipi kwa yeye Rais kutaja dawa ili wananchi wazitumie wapone? Yeye kataja zile ambazo serikali imethibitisha zinafanya kazi, na wananchi wana haki ya kuzijua ili wazitumie wapone, sasa ulitaka afiche ili kiwe nini? Au mleta mada una dawa yako ambayo imeshindwa kuthibitishwa ubora wake hivyo unaona wivu kutajwa dawa zingine?
Pia viongozi wa dini kama binadamu wengine wanachambwa kama kawaida pale wanapokosea. Aliyekuambia kiongozi wa dini hakosolewi basi alikudanganya sana. Unzuri wa Magufuli anakupa za uso hapo hapo hajali wewe ni nani. Ni lazima tuambiane ukweli ili tuweze kubadilika.
Kingine, anachofanya Magufuli si mahubiri, mahubiri ya Kanisa katoliki yanafanywa kabla ya kutoa sadaka baada tu ya somo la Injili ambapo huwa ni katikati ya ibada au misa. Muda anaosimama Magufuli ni muda wa matangazo ambapo misa au ibada inakuwa imeisha. So usichanganye hivyo vitu, kanisa katoliki lina utaratibu wake, na ibada au misa zina miongozo yake ya kufuata.