Rais Magufuli alitaka kuiua CHADEMA, lakini alishindwa! Hakuna wa kuinunua wala kuiua CHADEMA

Rais Magufuli alitaka kuiua CHADEMA, lakini alishindwa! Hakuna wa kuinunua wala kuiua CHADEMA

Apo ulipo bado unaamini ile chadema ya miaka iyo ndo yasasa? Imeshakatwa mkia kitambo.

Chadema imebaki mtandaoni, Mtaani watu wameshaanza kuisahau
Watu wa mitandaoni watakuwa wanaishi sayari nyingine, au siyo...
 
Magufuli kashindwa lakini mama ameweza tena bei chee kabisa, miezi 8 Mbowe aliyokaa jela ilitosha ku-sarender na kufutiwa mashtaka ingawa alikuwa na kesi ya kujibu, ndio mana alipochiwa tu break ya kwanza Ikulu, na sasaivi kila wiki Ikulu, chadema sasa naifananisha na TLP ya Mrema na Mbowe ni Mrema mwenyewe.

Ndio mana Mbowe juzi amediriki kusema chadema anataka kuifumua na kuisuka upya ili kina msingwa, tundu lissu, na Heche wasioamini kwenye udalali wataachwa nje

Watanzania bado wana safari ndefu sana kuiondoa ccm madarakani, baada Maalim seif watanzania walikuwa wanatupa jicho lao kwa chadema kama chama kikuu cha upinzani lakini sasa kinachotokea watanzania wengi hawaamini macho yao., Mbowe ambaye akiitwa mwamba sasa amekuwa kama pamba, ajenda ya katiba mpya hanayo tena, ni Ikulu na Ikulu na yeye.,
Utateseka sana
 
Segerea muli-sarender baada ya miezi 8 tu, sasa Mbowe amefika mwenyekiti wa chama chenu, Tundu Lissu hana mdomo huko aliko, kina msingwa haamini macho yake jamaa alivyowasaliti na chama chao
Bado sana, Jiwe alikuwa na imani kama yako
 
sasa ACT ndio angalau watanzania wanaweza elekea huko Chadema wamekubaliana bei ili Mbowe aachwe huru miezi 8 jela mwamba alikuwa hoi ikabidi aangushe majeshi, sasa saa 24 anashinda Ikulu
Kajiunge huko sasa, unateseka sana
 
Chadema wamejiua wenyewe kwa kutokusimamia wanachikiamini, JPM anahusikaje hapo? Ikiwa miaka nenda rudi mlimshambulia mzee Lowasa kwa kumsingizia mambo kibao kisha kaja kwenu mkampokea bila kujiuliza, ikiwa miaka nenda rudi mlipiga vita utoroshwaji wa maliasili zetu kaja JPM kukomesha haya mambo mkaanza kumpinga. Mungu hapendi mtu mwenye ndimi mbili.
Lowasa alichafuliwa na mfumo siyo Lowasa kama Lowasa ingekuwa Lowasa ndiye aliyehusika moja kwa moja na Richmond angekuwa sasa jela ila ule ulikuwa mchezo wawenyewe na wenyewe waliendelea kubaki madarakani mpaka wanamaliza.
 
TUKI wanatakiwa wabadili ule msemo wa banyiani mbaya.... iwe shetani mbaya kiatu chake dawa. Tuendelee kupokea nishani .
 
Mwenendo wa sasa ndo unaiua Chadema....ni muda tu.
 
Magufuli kashindwa lakini mama ameweza tena bei chee kabisa, miezi 8 Mbowe aliyokaa jela ilitosha ku-sarender na kufutiwa mashtaka ingawa alikuwa na kesi ya kujibu, ndio mana alipochiwa tu break ya kwanza Ikulu, na sasaivi kila wiki Ikulu, chadema sasa naifananisha na TLP ya Mrema na Mbowe ni Mrema mwenyewe.

Ndio mana Mbowe juzi amediriki kusema chadema anataka kuifumua na kuisuka upya ili kina msingwa, tundu lissu, na Heche wasioamini kwenye udalali wataachwa nje

Watanzania bado wana safari ndefu sana kuiondoa ccm madarakani, baada Maalim seif watanzania walikuwa wanatupa jicho lao kwa chadema kama chama kikuu cha upinzani lakini sasa kinachotokea watanzania wengi hawaamini macho yao., Mbowe ambaye akiitwa mwamba sasa amekuwa kama pamba, ajenda ya katiba mpya hanayo tena, ni Ikulu na Ikulu na yeye.,
Hivi wenzetu huwa mnatoa wapi muda wa kuandika ujinga mkubwa na mrefu kama huu!!??
Mnalipwa!!???
Mmejitoa akili au ndio mmezaliwa hivyo na uwezo mdogo wa kupambanua mambo!!???
 
sasa ACT ndio angalau watanzania wanaweza elekea huko Chadema wamekubaliana bei ili Mbowe aachwe huru miezi 8 jela mwamba alikuwa hoi ikabidi aangushe majeshi, sasa saa 24 anashinda Ikulu
Kama CHADEMA wamefika bei,maana yake Mh. Rais ameshindwa kuwashawishi kwa hoja mpaka awanunue!!??
Maana yake ni kuwa Mh. Rais uwezo wake ni mdogo kiasi hicho!!??
Maana yake mnamtukana Mh. Rais kuwa hawezi kujenga hoja mpaka atumie ushawishi wa pesa!!???
Umeelewa hayo mnayomtuhumu nayo Mbowe na CHADEMA kununuliwa yanamvua mama "credibility" aliyokuwa nayo!!???
 
We tu ndo hupati fungu, CHADEMA inanunulika, rejea uchaguzi wa 2015 yule mgombea aliinunua tena bei sawa na bure. Inwwezekana vipi mwizi uliyempiga vita ukamuachia mamlaka ya kuendesha akaunti yako?
Unafanya nini hapa Jukwaani!!?
Tafadhali, nenda kaendelee na kufanya majukumu yako kuliko kuja kuandika upupu na kuonyesha hadharani jinsi uwezo wako wa kufikiri ulivyo mdogo.
 
Naona kuna kundi kubwa limeandaliwa humu JF kupinga na kubeza Mazungumzo yanayoendelea baina ya Rais Samia na Mbowe.

Kundi hili ndio lile Kundi lililokuwa linashabikia kuwa Mbowe ni gaidi. Baada ya kupata aibu kwa kelele zile sasa wanaandika habari za uongo na uzushi dhidi ya Mbowe na CHADEMA.

Kifupi wanajitekenya na kujichekesha kwani Wanachama na Wafuasi wa CHADEMA wana akili kubwa. Endeleeni kupuyanga umbea lakini usiku mtalala.

CHADEMA haifi, kama alishindwa Magufuli kuinunua CHADEMA nyinyi Mavuvuzeni hamuiwezi CHADEMA

CHADEMA BEI YAKE NI KAMA BEI YA KUINUNUA KLABU YA CHELSEA
Kila atakayejaribu kuleta uchawi kwa Chadema atakufa
 
Back
Top Bottom