Mwitikio wa andiko langu wiki lililopita katika mtandao huu wa JF ulinipa hamasa kuendelea kuandika zaidi jinsi Rais Magufuli anavyoendelea kulipotezea mwelekeo taifa. Wiki hii naona nigusie kwa undani jinsi Magufuli anavyoharibu uhusiano mzuri sana uliokuwepo kati ya Tanzania na wadau mbalimbali wa maendeleo. Awali ya yote naomba mnisamehe, kiswahili changu si kizuri kama ambavyoningependa kiwe, ila anendela kujifunza;
Sio siri kwamba Tanzania ilijulikana kama kipenzi cha wadau wa maendeleo(darling of development partners); Ukiangalia twakimu za misaada iliyokuwa inaletwa na wahisani katika nchi za Africa, Tanzania ilikua haikosi katika 10 bora katika nchi za Africa. Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Marekani, China, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani nchi zote hizi zilikua zinawekeza kwa nguvu kubwa katika maendeleo ya watanzania.
Magufuli alipoingia madarakani, mambo yakaanza kubadilika, mwanzoni walikua wanamvumilia sababu alionekana kama ni kiongozi mpya mwenye ‘zeal’ ya kupigana na rushwa ila siku zilivyokuwa zinazidi wakaona hali inazidi kuwa mbaya hususani katika utawala wa sheria, demokrasia na haki za binadamu.
Magufuli alipotangaza kuzuia wasichana wa kike kutoendelea na masomo yao kisa ya mimba alipiga msumari mkali katika mahusiano na hawa watu. Na hii ndio sababu husikii hawa development partners hawainvest kwenye sekta ya elimu, maana wakitoa msaada au wakiwakopa Tanzania, watanekana na wao wapo complicit kwenye hilo katazo. Athari zake tunaziona kwa jinsi hali ya elimu inavyozidi kuporomoka siku baada ya siku, madarasa hayatoshi, walimu hawashugulikiwi madai yao vizuri maana mzigo wa kuiinua hii sekta nyeti kwa Taifa limebaki tu kwa serikali.
Benki ya dunia
Katika wahisani ambao sikutegemea (hata Magufuli mwenyewe hakutegemea) wangeweza kuigomea serikali ni Benki ya dunia maana ndio ilikua taasisi iliyobaki ambayo ilikua inaipa serikali kiburi pamoja na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za kiraia.
Kwa msiofahamu wahisani wanachangia asilimia 40% ya bajeti ya Tanzania na Benki ya dunia inachakia takribani asilimia 10%(kubwa kuliko mdau yeyote) na hivyo kuifanya kuwa Tanzania’s biggest partner in development.
Benki ya dunia ilianza kuichoka serikali walipofanya marekebisho kwenye sheria ya twakimu ya mwaka 2018 ambayo inazuia taasisi yeyote kuto-desseminate statistics bila kupata verification kutoka NBS. Kazi kubwa za Benki ya Dunia ikiwemo repoti na miradi zinategema takwimu halisi, hii sheria mpya iliweka vikwazo vilivyoifanya WB kutofanya kazi zao freely and professionally
Tulisikia mwaka jana mwezi wa 11 jinsi benki ya dunia livyositisha mkopo wa $300million wa elimu (takribani billion 700tsh) kwa sababu ya sera ya serikali ya kutoruhusu hawa watoto kurudi shuleni. Magufuli anathamini na anajua mchango wa benki ya dunia katika maendeleo ya nchi na ndio maana alikubali kukutana na WB Regional Vice President wanegotiate kuhusu huu mkopo. Katika maongezi yao (japo hayajawekwa wazi) walikubaliana kuandaa program ambayo italipiwa na serikali itakayowawezesha watoto wa kike wenye mimba kupata elimu, kama mnakumbuka wakati ule nchi ilibujikwa katika sakata la ushoga lililoanzishwa na makonda, waliliongelea na Magufuli alimuhaidi kuwa amna mtu atakae kamatwa kwa ushoga na atamkataza Mkuu wa Mkoa kuongelea kuhusu swala hilo tena, tatu, alikubali kuendelea kuwa na maongezi juu ya ile sheria ya takwimu.
Cha kushangaza, siku chache tu baada ya kukubaliana nao, Magufuli wakati wa uzinduzi wa Library ya UDSM, akawakashifu kwa kuwapongeza waChina kwa kuwaambia kuwa, “misaada yenu hayana masharti, sio kama mashirika mengine”. Huyo makamu wa Rais alisikitiswa na kauli hii maana ilionyesha kuwa serikali haikuwa na commitment katika makubaliano hayo.
Ni kwa sababu hiyo mpaka leo hii mkopo haujatolewa na sidhani kama utaolewa. Sio hiyo tu, Benki ya Dunia imei-demote ofisi yake ya Tanzania. Benki ya Dunia inakuaga na Country Director- wa sasa ni ndugu Bella Bird lakini kuanzia June 2019, amabapo mda wake utaisha nchi itaanza kuwa na country manager.
Kuwa na country manager inamaanisha kuwa na portfolio ya nchi itapunguzwa. Miradi yote inayohusiana na P4R – Program for results, kwenye elimu, maji, umeme, yote inafutwa, maana huwezi kupata results without credible statistics.
Pamoja na balozi Mahiga na Prof Kabudi kwenda Brussels kuipigia magoti umoja wa ulaya bado wameendelea kusitisha msaada wao nchini.
Yamkini inabidi tutafute mbinu za kujitegemea lakini tupende tusipende bado tunawahitaji hawa wadau wa maendeleo. Hata Europe yenyewe iliendelea kwa kusaidiwa na Marekani through the Marshall Plan policy iliplay a big part in the reconstruction of Europe baada ya vita ya pili ya dunia.
Serikali ifanye nini
Kwanza wathibiti matamko ya Rais; Kuwaita mabeberu hadharani, kutangaza kwamba nchi ipo katika vita ya uchumi na kusema kwamba misaada yao inamasharti. Ushawahi kuona wapi jirani yako anakuja kukusaidia alafu unaanza kumtukana, unadhani ataendelea kukusaidia?? Sio lazima akubaliane nao ila awaheshimu, kiufuppi ajifunze lugha za kidiplomasia zaidi
Pili, na hii itakua ngumu kwake, aruhusu watoto wenye mimba waendelee na masomo yao, hii itabuild confidence kubwa sana kwa hawa wahisani. But we all know this is never going to happen maana Rais alishasema na ninanamnukuu, “katika utawala wangu watoto wenye mimba hawatarudi shuleni, siwezi somesha wazazi”. Kwa mtu mwenye ego kubwa kama Rais wetu, hawezi reverse such a statement, it will possibly be the biggest political miracle in our country’s history.
Tatu, Asisgn into law mswada wa vyama vya siasa. Hii itakua ushindi kwakwe in both the internal and external politics.. kwanini; 1. Itanesha kwamba kama Rais anaheshimu demokrasia ya vyama vingi, pili itabuild trust kwa wananchi kuwa rais kumbe anauwezo wa kutosign sheria mbaya hata iliyopitishwa na wabunge wa vyama vyake (hatausishwa na hii sheria kabisa), tatu, He will for once be on the positive side of the coverage of the international media. Tutaona makala mabali mbali za nje zitakavyomsifu jinsi kwa huo uwamuzi… But this is also never going to happen maana ukweli unajulika kuwa yeye ndio muasisi mkuu wa hiyo sheria.
Najua wengi mtasema kuwa “hatuitaji misaada yao” “serikali ina pesa” ila ukweli msioujua ni kuwa the government is sooooooooooo broke, na ndio maana unaona kuna msisitizo mkubwa hivi karibuni wa kulipa kodi na kufanya ulipaji kodi kuwa rahisi kwa watanzania.
Kama mnadhani tunaweza kuendelea bila ushirikiano na wadau wa maendeleo angalieni hali ya Zimbabwe wanaoenda nunua mkate na begi limejaa noti… Serikali ibadilishe mwelekeo, kabla mwelekeo haujatubadilisha… kuweni na siku njema