Kikarara78
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,495
- 903
Boss Nyani Ngabu Umoja wa Vijana na TASAF vinaingilianaje hapo ??? !!! Mpaka Mh. Mkapa ameshangaa nae. Aliambiwa nauli ilitoka kwenye pesa za TASAF ??? !!! Kiki ... Kiki ... !!!
Aisee ... Kamanda ... anasema ... LAZIMA tuwe ... Wazalendo, na sio tena MOYO wa KIZALENDO.
Kweli Dunia inazunguka kwa kasi sana aisee.
Aisee ... Kamanda ... anasema ... LAZIMA tuwe ... Wazalendo, na sio tena MOYO wa KIZALENDO.
Kweli Dunia inazunguka kwa kasi sana aisee.
Rais Magufuli leo kasema, kama Makonda alizitumia fedha za TASAF, basi na azirudishe.
Vilisikika vicheko hafifu na vya chinichini baada ya Rais kusema hivyo.
Kamera nazo zikamwonyesha Makonda, aliyekuwa kakaa mbele pamoja na viongozi wengine, akitabasamu kana kwamba hana wasiwasi wowote. Yaani hakuna baya litalomtokea [sababu yaweza kuwa ni kwa sababu hakuzitumia kabisa hizo hela, au, alizitumia lakini anajua kuwa Rais hatomfanya chochote, n.k.]
Kamera pia ziliwaonyesha marais wastaafu wote watatu.
Kwa kuwasoma lugha yao ya mwili, ni kama vile walikuwa ‘embarrassed’ na alichokisema rais.
Ni kweli Rais Magufuli alimaanisha alichokisema au kasema vile ili kuonyesha tu kuwa ‘hampendelei’ Makonda?
Binafsi naona kama vile kasema tu ili kuonyesha ‘hampendelei’ jamaa huku kiuhalisia hakuna lolote atalomfanya maana jamaa ana madhambi mengi na makubwa kuliko hilo la kutumia fedha za TASAF.
Bofya video umsikie Rais alivyosema kuhusu Makonda. Kuanzia dakika ya kwanza hadi ya pili.