Rais Magufuli amchenjia Makonda?

Rais Magufuli amchenjia Makonda?

Rais Magufuli leo kasema, kama Makonda alizitumia fedha za TASAF, basi na azirudishe.

Vilisikika vicheko hafifu na vya chinichini baada ya Rais kusema hivyo.

Kamera nazo zikamwonyesha Makonda, aliyekuwa kakaa mbele pamoja na viongozi wengine, akitabasamu kana kwamba hana wasiwasi wowote. Yaani hakuna baya litalomtokea [sababu yaweza kuwa ni kwa sababu hakuzitumia kabisa hizo hela, au, alizitumia lakini anajua kuwa Rais hatomfanya chochote, n.k.]

Kamera pia ziliwaonyesha marais wastaafu wote watatu.

Kwa kuwasoma lugha yao ya mwili, ni kama vile walikuwa ‘embarrassed’ na alichokisema rais.

Ni kweli Rais Magufuli alimaanisha alichokisema au kasema vile ili kuonyesha tu kuwa ‘hampendelei’ Makonda?

Binafsi naona kama vile kasema tu ili kuonyesha ‘hampendelei’ jamaa huku kiuhalisia hakuna lolote atalomfanya maana jamaa ana madhambi mengi na makubwa kuliko hilo la kutumia fedha za TASAF.

Bofya video umsikie Rais alivyosema kuhusu Makonda. Kuanzia dakika ya kwanza hadi ya pili.

Pesa za Tasaf, Kumbe zilikuwa zinachotwa kwa staili hiyo [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hivi hizo pesa za TASAF ni enzi ya Mkapa,Makonda alikuwa hohehahe hivyo akasaidiwa.Hizo pesa ilikuwa ni halali kwake kabisa ukilinganisha na mission za TASAF.Akipenda atarudisha tu maana kwa sasa ana uwezo.
Makonda hakuwa Masikini, Mkuu Mwenyewe amezungumza ivyo !! Hapo pesa zilitumika vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda ni hirizi ya jiwe. Tangu lini mmiliki wa hirizi akaweza kuichenjia?

Labda aokoke kwanza.
 
Nyani Ngabu,
Ni kelele tu hakuna chochote anachoweza kumfanya huyo kijana. Yeye ataishia kwa kina Lugola na Madelu tu huyo dogo ni moto wa kuotea mbali hata wamarikani wamemshindwa. Sembuse yeye?
Yaani Marekani imshindwe makonda??!!..kuwa serious mkuu
 
Baba na mwana tunaimba na kuchezaa[emoji445] ...huu wimbo nmeukumbuka mzur sana

Sent using Jamii Forums mobile app
images (7).jpeg
 
Rais Magufuli leo kasema, kama Makonda alizitumia fedha za TASAF, basi na azirudishe.

Vilisikika vicheko hafifu na vya chinichini baada ya Rais kusema hivyo.

Kamera nazo zikamwonyesha Makonda, aliyekuwa kakaa mbele pamoja na viongozi wengine, akitabasamu kana kwamba hana wasiwasi wowote. Yaani hakuna baya litalomtokea [sababu yaweza kuwa ni kwa sababu hakuzitumia kabisa hizo hela, au, alizitumia lakini anajua kuwa Rais hatomfanya chochote, n.k.]

Kamera pia ziliwaonyesha marais wastaafu wote watatu.

Kwa kuwasoma lugha yao ya mwili, ni kama vile walikuwa ‘embarrassed’ na alichokisema rais.

Ni kweli Rais Magufuli alimaanisha alichokisema au kasema vile ili kuonyesha tu kuwa ‘hampendelei’ Makonda?

Binafsi naona kama vile kasema tu ili kuonyesha ‘hampendelei’ jamaa huku kiuhalisia hakuna lolote atalomfanya maana jamaa ana madhambi mengi na makubwa kuliko hilo la kutumia fedha za TASAF.

Bofya video umsikie Rais alivyosema kuhusu Makonda. Kuanzia dakika ya kwanza hadi ya pili.

Washirikina huwa hawabadilikiani. Leta story nyingine sio hii.
 
Wakati Makonda anaongea,kabla ya Magu kuongea.Makonda alikuwa anaainisha umuhimu wa huo mfuko wa Tasaf,ndo akasema na yeye mfuko uliwahi msaidia nauli ya kwenda Dom.
Kwa hiyo arudishe kama elfu sabini hivi, au laki na kidogo kama alitumia Ndege?
 
Back
Top Bottom