Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Raisi Magufuli amefanya kosa kubwa sana kuagiza kwamba magari yaliyotaifishwa kuhusiana na kesi za uhujumu uchumi yagaiwe kwa taasisi za Serikali kwa sababu mbili kubwa zifuatazo;
Ningemshauri Rais Magufuli kwamba haya magari yapigwe mnada na fedha zitakazopatikana ziingizwe kwenye shughuli zinazohusiana na kupambana na uhujumu uchumi nchini, ili wakamate magari mengi hata zaidi!
- Haya magari mengi ni ya zamani sana, zaidi ya miaka 10, na mengi yalinunuliwa kama used vehicles. Wamiliki binafsi huwa wana namna yao ya kuya-maintain kwa gharama za chini, na kuyaingiza serikali kutasababisha gharama kubwa za matengenezo na maintanance ambayo mwisho wa siku itakuwa ni hasara kwa taifa. Watu wa uhasibu wakipiga hesabu za "depreciation" za haya magari wanaweza kukuta ni scrap tu. Gharama ya ku-maintain gari "scrap" ni kubwa sana afadhali kununua gari jipya
- Kuna sera ya serikali ya manunuzi kwamba taasisi za serikali hazipaswi "kununua" (acquisition) magari au vitu ambavo ni second hand. Kwa hiyo japo magari haya yanatolewa bure kwa hizi taasisi za serikali, kimsingi hili linakiuka sera ya taasisi za serikali kutoingiza kwenye leja zao za umiliki wa mali vitu magari ambayo ni "used".
Ningemshauri Rais Magufuli kwamba haya magari yapigwe mnada na fedha zitakazopatikana ziingizwe kwenye shughuli zinazohusiana na kupambana na uhujumu uchumi nchini, ili wakamate magari mengi hata zaidi!