Rais Magufuli amekosea sana kuagiza magari ya kesi za Uhujumu Uchumi yapewe Taasisi za Serikali

Rais Magufuli amekosea sana kuagiza magari ya kesi za Uhujumu Uchumi yapewe Taasisi za Serikali

Kuna maeneo hayana magari kabisa ya huduma kwa wananchi, sasa bora nini? Wapate magali yaliyotumika na kuyatumia au wawe bila magari watumie baiskeli?
Tatizo lenu kila jambo mnadhani ni siasa tu!! Ki uhalisia hayo magari kuyatunza ni gharama sana, sasa uwe na gari(chombo cha fundi) kila leo ni gereji, mnatumia mafungu mengine kugharamikia gari, si bora mbaki na baiskeri tu!! Gharama za services za gari kwa mwaka unapata gari jipya, hizo ni akili au matope?!!! Hayo magari mengi ni scrap!! Wewe kuna fuso hapo kuzirejesha tu kwenye hali yake ni karibu na thamani ya jipya!!!!
 
Pale kiongozi anapokuwa yeye ndio kila kitu.
Umeniwahi ,unaweza sema huyu ndugu sijui hana kazi za kufanya kama rais au inakuaje,nilishangaa sana jana hapo ndio unaweza jiuliza wenye hayo majukumu huwa wanafanya nini sasa
Si ajabu huwa tunasikia maneno ya rais ametoa bilioni kadhaa mara ametuletea hiki au kile sijui maono ya rais yaani ni shida tupu,aliyesemaga tuna fulani wa ajabu sana hakukosea
Si hayo tu kudhihirisha kushindwa kwa mfumo wa kiutawala wa ccm ni pale kila ziara ya rais utasikia matatizo ni yale yale,akitoka msibani kwa rais alilazimika kutatua kero ya vyoo vya stendi,wakiambiwa tubadilishe mfumo wa kiutendaji hawaelewi
 
Hapo sikuungi mkono sana mtoa mada,hayo magari sio yote yaliochoka jinsi unavyoeleza wewe,ingawa najua kuna baadhi yaliyochoka kabisa,hayo yanaweza kupigwa mnada.Unajua kuwa kuna taasisi za serikali ambazo hazina magari kabisa! na kama yapo yamechoka kuliko hata hayo ya wahalifu?sasa kipi ni bora,kuendelea kugharamia lililopo kwenye taasisi ambalo ni choka mbaya au kuchuku haya yenye nafuu ili yapige kazi? Kwasababu gharama ya gari mpya,nikiwa na maana ya 0KM unaweza kununua hizo used 3.Cha kufanya hapo ni kwenda kukagua yale yenye nafuu,yafanyiwe maintanance kubwa,baada ya hapo serikali iendelee kujikusanya kununua hayo mapya,kuliko hilo wazo lako la kuyapiga mnada halafu hela ziende kwenye kufuatilia magari mengine ya wahujumu uchumi,wakati kuna mipango mingi ya maendeleo inakwama kwa kukosa magari..
 
Kuna maeneo hayana magari kabisa ya huduma kwa wananchi, sasa bora nini? Wapate magali yaliyotumika na kuyatumia au wawe bila magari watumie baiskeli?
Unataka kusema nchii hii hii ambayo tunaambiwa tunanunua ndege kwa cash, tunajenga sgr kwa fedha zetu, umeme wa Nyerere kwa hela zetu halafu kuna idara/taasisi za serikali hazina magari!!!!!!!.
 
Ila yapo yalotaifishwaga kimya kimya awamu ya mkapa na yapo kwenye mataasisi ya serikali na yanapiga kazi tu
Raisi Magufuli amefanya kosa kubwa sana kuagiza kwamba magari yaliyotaifishwa kuhusiana na kesi za uhujumu uchumi yagaiwe kwa taasisi za Serikali kwa sababu mbili kubwa zifuatazo;
  1. Haya magari mengi ni ya zamani sana, zaidi ya miaka 10, na mengi yalinunuliwa kama used vehicles. Wamiliki binafsi huwa wana namna yao ya kuya-maintain kwa gharama za chini, na kuyaingiza serikali kutasababisha gharama kubwa za matengenezo na maintanance ambayo mwisho wa siku itakuwa ni hasara kwa taifa. Watu wa uhasibu wakipiga hesabu za "depreciation" za haya magari wanaweza kukuta ni scrap tu. Gharama ya ku-maintain gari "scrap" ni kubwa sana afadhali kununua gari jipya
  2. Kuna sera ya serikali ya manunuzi kwamba taasisi za serikali hazipaswi "kununua" (acquisition) magari au vitu ambavo ni second hand. Kwa hiyo japo magari haya yanatolewa bure kwa hizi taasisi za serikali, kimsingi hili linakiuka sera ya taasisi za serikali kutoingiza kwenye leja zao za umiliki wa mali vitu magari ambayo ni "used".
Nini kifanyike basi?

Ningemshauri Rais Magufuli kwamba haya magari yapigwe mnada na fedha zitakazopatikana ziingizwe kwenye shughuli zinazohusiana na kupambana na uhujumu uchumi nchini, ili wakamate magari mengi hata zaidi!
 
Aliyeyapanda na kuyasaga yeye alikataa nusu faida, huyu yeye kakataa nusu faida na kuamua kuanza kuchuma hasara.
Wahenga walisema kusuka na kunyoa, zote ni style za nywele.
Magu angesema yauzwe vitengo, husika wangejiuzia kwa bei ya kutupwa!

Everyday is Saturday............................ 😎
 
Wanapeleka mikosi tuu magari ya kupora watu hayo ajali za ajabu ajabu hazitoisha kamwe kwa watumiaji hayo magari kweli Nchi zetu ni maskini wapo busy na magari machakavu aisee nimeshangaa sana
 
Bwana wee, hebu mara nyingine tutumie busara ya elimu katika kuamua mambo. Wewe umeambiwa hapo juu kuna mtu ameona RAV4 a mwaka 1996. Sasa unafikiri katika masuala ya asset za serikali ukiambiwa wahasibu wafanye evaluation ya hiyo gari watakuambia thamani yake ni kiasi gani?

Kama hujui mambo ya gharama za mainatance za magari katika serikali basi acha tunaoelewa haya mambo tuongee. Jiulize swali, ikiwa taasisi za serikali zinaruhusiwa kisheria kupiga mnada gari za zamani baada ya kufikia depreciation ya kiasi fulani, kwa nini basi taasisi hizo hizo leo zipewe RAV4 ya mwaka 1996?

Mimi nikiwa mkurugenzi katika taasisi ya serikali itakayopewa RAV4 ya 1996, kesho yake tu baada ya kukabidhiwa nitatoa idhini ipigwe mnada wa hadhara, kulingana na kanuni za assets za taasisi za serikali
Achana na mshamba huyo.

Kazi kusifusifu kama mbuzi alokatwa kichwa.

Hizo gari ni takataka.

Wazipeleke mikoani wakinga wakazinunue.
 
Uko sahihi kabisa iwapo tu ungeweza kutamka maneno hayo hayo bila kuyamung'unya hata chembe, kama ungekuwa upo pamoja naye hapo ulipo. Ila kama umetamka hivyo kwa sababu upo kwenye mtandao na yeye hayupo, basi mara nyingine inabidi labda uyapunguze makali kidogo. Si kwa Rais tu bali pia kwa watu wengine akiwemo hata bosi wako ofisini kwako hapo ulipo
MKuu, mbona unaji-contradict?

Nikiwa nae nisimung'unye, nisipokuwa naye nimung'unye!
 
Back
Top Bottom