Bwana wee, hebu mara nyingine tutumie busara ya elimu katika kuamua mambo. Wewe umeambiwa hapo juu kuna mtu ameona RAV4 a mwaka 1996. Sasa unafikiri katika masuala ya asset za serikali ukiambiwa wahasibu wafanye evaluation ya hiyo gari watakuambia thamani yake ni kiasi gani?
Kama hujui mambo ya gharama za mainatance za magari katika serikali basi acha tunaoelewa haya mambo tuongee. Jiulize swali, ikiwa taasisi za serikali zinaruhusiwa kisheria kupiga mnada gari za zamani baada ya kufikia depreciation ya kiasi fulani, kwa nini basi taasisi hizo hizo leo zipewe RAV4 ya mwaka 1996?
Mimi nikiwa mkurugenzi katika taasisi ya serikali itakayopewa RAV4 ya 1996, kesho yake tu baada ya kukabidhiwa nitatoa idhini ipigwe mnada wa hadhara, kulingana na kanuni za assets za taasisi za serikali