Rais Magufuli amekosea sana kuagiza magari ya kesi za Uhujumu Uchumi yapewe Taasisi za Serikali

Rais Magufuli amekosea sana kuagiza magari ya kesi za Uhujumu Uchumi yapewe Taasisi za Serikali

Iwanununulie kwa bajeti ipi mkuu. Why huoni jema kwenye kitu direct hivyo. Kasema kule ambako Kuna Shida hasa wananchi kupata huduma. Watu kama nyie sijui Ni Perfect kiasi gani. Lakini kisaikologia the opposite is true.
Bwana wee, hebu mara nyingine tutumie busara ya elimu katika kuamua mambo. Wewe umeambiwa hapo juu kuna mtu ameona RAV4 a mwaka 1996. Sasa unafikiri katika masuala ya asset za serikali ukiambiwa wahasibu wafanye evaluation ya hiyo gari watakuambia thamani yake ni kiasi gani?

Kama hujui mambo ya gharama za mainatance za magari katika serikali basi acha tunaoelewa haya mambo tuongee. Jiulize swali, ikiwa taasisi za serikali zinaruhusiwa kisheria kupiga mnada gari za zamani baada ya kufikia depreciation ya kiasi fulani, kwa nini basi taasisi hizo hizo leo zipewe RAV4 ya mwaka 1996?

Mimi nikiwa mkurugenzi katika taasisi ya serikali itakayopewa RAV4 ya 1996, kesho yake tu baada ya kukabidhiwa nitatoa idhini ipigwe mnada wa hadhara, kulingana na kanuni za assets za taasisi za serikali
 
Tatizo ni wenye akili kubwa kufanyiwa maamuzi na mwenye akili ndogo tena una akili kuliko yesu wa chatle
Uoga huzaa unafiki ukifikia hapo huwezi mshauri wala kum-chalange mtukufu.

Sera ya serikali kakiri kabisa hairuhusu used cars ila ndo hivyo kumpinga ni mwiko ye keshaamua japo anaweza badili huo uamuzi hata sasa
Ubarikiwe sana mkuu.
 
Kuna maeneo hayana magari kabisa ya huduma kwa wananchi, sasa bora nini? Wapate magali yaliyotumika na kuyatumia au wawe bila magari watumie baiskeli?
Utasemaje kuna sehemu za serikali hazina magari wakati tunamuona anatembea na sanduku la pesa za serikali kila awapo ziarani.
 
Me walete kwenye taasisi yetu wanipe hyo amarok tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie mnaweza kupewa hii Probox muongeze ufanisi😀😀😀
1598431378559.png
 
wakiyauza wale maharamia watakuja kuyagomboa yote sema TEMESA nao wanazingua sana ukipeleka gari badala liludi limepona ndio wanaua kabisa wakati ukipeleka kwa fundi juma mwembeni linatoka fresh kabisa
Mkuu, kwani tatizo ni nini ikiwa watayagomboa kwa kulipa fedha zitakazoingia serikalini? Kwani wamepigwa marufuku kumiliki magari?
 
"Mimi nikiwa mkurugenzi katika taasisi ya serikali itakayopewa RAV4 ya 1996, kesho yake tu baada ya kukabidhiwa nitatoa idhini ipigwe mnada wa hadhara, kulingana na kanuni za assets za taasisi za serikali"

NUKUU YA LEO
 
Synthesizer,

Title yako ina maneno makali, ila content yako iko safi.

Hata mimi naunga mkono hoja yako kwamba yapigwe mnada halafu wao Serikali wanune magari mengine mapya kwa kutumia fedha itakaypatikana, hata kama itatosha kununua magari 10 tu. Hayo waliyokamata yakakuja kuwagharimu pesa nyingi sana kwenye upade wa matengenezo, na possibly hata maisha ya watu.

Ni kwa sababu bado yataendelea kuwa na chembe chembe za uadui kati ya waliokuwa wakiyamiliki kabla na vyombo vya serikali vitakavyokuwa vimepewa dhamana ya kutumia magari haya, hasa wale walionyang'anywa watakapokuwa wanayaona yakieendelea kuwa mikononi mwa Serikali.

Ni bora wayaone na watu binafsi ambao wameuziwa, na si watu waliopewa bure, japo ni ya Serikali
 
Ushauri mzuri ila sidhani kama atakuelewa!

Kama vichwa vya treni vilivyookotwa bandirin leo vinatumika sembuse hayo magari ambayo mmiliki anajulikana?
 
Title yako ina maneno makali, ila content yako iko safi.
MKuu sometimes ni vema to call a spade spade. Haya mambo ya kusifiana kinafiki nafiki wengine hatuna silka hiyo. Naliona hili kama kosa kubwa sana na ndio maana nikasema amekosea sana.
 
MKuu sometimes ni vema to call a spade spade. Haya mambo ya kusifiana kinafiki nafiki wengine hatuna silka hiyo. Naliona hili kama kosa kubwa sana na ndio maana nikasema amekosea sana.
Uko sahihi kabisa iwapo tu ungeweza kutamka maneno hayo hayo bila kuyamung'unya hata chembe, kama ungekuwa upo pamoja naye hapo ulipo. Ila kama umetamka hivyo kwa sababu upo kwenye mtandao na yeye hayupo, basi mara nyingine inabidi labda uyapunguze makali kidogo. Si kwa Rais tu bali pia kwa watu wengine akiwemo hata bosi wako ofisini kwako hapo ulipo
 
Back
Top Bottom