Rais Magufuli amekosea sana kuagiza magari ya kesi za Uhujumu Uchumi yapewe Taasisi za Serikali

Rais Magufuli amekosea sana kuagiza magari ya kesi za Uhujumu Uchumi yapewe Taasisi za Serikali

Kama Maeneo gani ambayo hayana magari ya huduma kwa wananchi?
Kuna maeneo hayana magari kabisa ya huduma kwa wananchi, sasa bora nini? Wapate magali yaliyotumika na kuyatumia au wawe bila magari watumie baiskeli?
 
Mawazo kama haya ndio viongozi walio chini ya Rais wanatikiwa wamshauri,lakini wao ni kuitika tu ndio mh Rais huku wakiwa wamekunja mikono mbele.
 
Raisi Magufuli amefanya kosa kubwa sana kuagiza kwamba magari yaliyotaifishwa kuhusiana na kesi za uhujumu uchumi yagaiwe kwa taasisi za Serikali kwa sababu mbili kubwa zifuatazo;
  1. Haya magari mengi ni ya zamani sana, zaidi ya miaka 10, na mengi yalinunuliwa kama used vehicles. Wamiliki binafsi huwa wana namna yao ya kuya-maintain kwa gharama za chini, na kuyaingiza serikali kutasababisha gharama kubwa za matengenezo na maintanance ambayo mwisho wa siku itakuwa ni hasara kwa taifa. Watu wa uhasibu wakipiga hesabu za "depreciation" za haya magari wanaweza kukuta ni scrap tu. Gharama ya ku-maintain gari "scrap" ni kubwa sana afadhali kununua gari jipya
  2. Kuna sera ya serikali ya manunuzi kwamba taasisi za serikali hazipaswi "kununua" (acquisition) magari au vitu ambavo ni second hand. Kwa hiyo japo magari haya yanatolewa bure kwa hizi taasisi za serikali, kimsingi hili linakiuka sera ya taasisi za serikali kutoingiza kwenye leja zao za umiliki wa mali vitu magari ambayo ni "used".
Nini kifanyike basi?

Ningemshauri Rais Magufuli kwamba haya magari yapigwe mnada na fedha zitakazopatikana ziingizwe kwenye shughuli zinazohusiana na kupambana na uhujumu uchumi nchini, ili wakamate magari mengi hata zaidi!
Safi Sana brother
 
Bwana wee, hebu mara nyingine tutumie busara ya elimu katika kuamua mambo. Wewe umeambiwa hapo juu kuna mtu ameona RAV4 a mwaka 1996. Sasa unafikiri katika masuala ya asset za serikali ukiambiwa wahasibu wafanye evaluation ya hiyo gari watakuambia thamani yake ni kiasi gani?

Kama hujui mambo ya gharama za mainatance za magari katika serikali basi acha tunaoelewa haya mambo tuongee. Jiulize swali, ikiwa taasisi za serikali zinaruhusiwa kisheria kupiga mnada gari za zamani baada ya kufikia depreciation ya kiasi fulani, kwa nini basi taasisi hizo hizo leo zipewe RAV4 ya mwaka 1996?

Mimi nikiwa mkurugenzi katika taasisi ya serikali itakayopewa RAV4 ya 1996, kesho yake tu baada ya kukabidhiwa nitatoa idhini ipigwe mnada wa hadhara, kulingana na kanuni za assets za taasisi za serikali
Hakuna mkurugenzi mwenye mamlaka ya kuamua mali ya serikali iuzwe. Mali za serikali zinauzwa kwa mchakato maalum ukiwahusu wizara ya ujenzi ( Teresa) na wizara ya fedha.
 
Hakuna mkurugenzi mwenye mamlaka ya kuamua mali ya serikali iuzwe. Mali za serikali zinauzwa kwa mchakato maalum ukiwahusu wizara ya ujenzi ( Teresa) na wizara ya fedha.
Nimekupata Mkuu. Wakati fulani huko nyuma enzi za nani sijui, Mkurugenzi wa Tacoshiri, shirika la meli la Taifa enzi hizo, George Mbowe, alifukuzwa kazi kwa kosa la kuuza meli ya serikali kwa mhindi Lord Rajpar. Watu walisema hiki ni kiini macho, mkurugenzi mamlaka ya kuuza meli ya serikali atapata wapi? Nasikia vigogo walihusika lakini ikabidi Mbowe afukuzwe kazi kupooza wananchi. Baadae akapewa mzinga wa post - Chairman wa PSRC, akatajirikia hapo kichizi!
 
Hapo sikuungi mkono sana mtoa mada,hayo magari sio yote yaliochoka jinsi unavyoeleza wewe,ingawa najua kuna baadhi yaliyochoka kabisa,hayo yanaweza kupigwa mnada.Unajua kuwa kuna taasisi za serikali ambazo hazina magari kabisa! na kama yapo yamechoka kuliko hata hayo ya wahalifu?sasa kipi ni bora,kuendelea kugharamia lililopo kwenye taasisi ambalo ni choka mbaya au kuchuku haya yenye nafuu ili yapige kazi? Kwasababu gharama ya gari mpya,nikiwa na maana ya 0KM unaweza kununua hizo used 3.Cha kufanya hapo ni kwenda kukagua yale yenye nafuu,yafanyiwe maintanance kubwa,baada ya hapo serikali iendelee kujikusanya kununua hayo mapya,kuliko hilo wazo lako la kuyapiga mnada halafu hela ziende kwenye kufuatilia magari mengine ya wahujumu uchumi,wakati kuna mipango mingi ya maendeleo inakwama kwa kukosa magari..
Tatizo ni kwamba mnanunua magari used kutoka Japan na Dubai ambao wao wanaona yamechoka lakini nyie mnaona ni mapya. Sasa hiyo mentality ya "gari jipya" ndio imewakaa vichwani. Kuna nchi duniani gari ikiwa na miaka mitatu ni chakavu inapaswa kulipa pollution tax kubwa, ndio tunauziwa huku kwa kuwa watu kama wewe mnaona jipyaaaa! Uliza Singapore wanaruhusiwa kutumia gari kwa muda gani ndio utajua maana ya gari jipya

Hatuongelei gari jipya kwa muonekano wa macho hapa. Hakuna gari jipya katika hayo magari. Piga mnada uchafu huo. Tatizo watu wachafu wanapenda vitu vikuu vikuu.
 
Kuna maeneo hayana magari kabisa ya huduma kwa wananchi, sasa bora nini? Wapate magali yaliyotumika na kuyatumia au wawe bila magari watumie baiskeli?
Si mpaka wafikiriwe kupelekewa hayo magari.
 
Raisi Magufuli amefanya kosa kubwa sana kuagiza kwamba magari yaliyotaifishwa kuhusiana na kesi za uhujumu uchumi yagaiwe kwa taasisi za Serikali kwa sababu mbili kubwa zifuatazo;
  1. Haya magari mengi ni ya zamani sana, zaidi ya miaka 10, na mengi yalinunuliwa kama used vehicles. Wamiliki binafsi huwa wana namna yao ya kuya-maintain kwa gharama za chini, na kuyaingiza serikali kutasababisha gharama kubwa za matengenezo na maintanance ambayo mwisho wa siku itakuwa ni hasara kwa taifa. Watu wa uhasibu wakipiga hesabu za "depreciation" za haya magari wanaweza kukuta ni scrap tu. Gharama ya ku-maintain gari "scrap" ni kubwa sana afadhali kununua gari jipya
  2. Kuna sera ya serikali ya manunuzi kwamba taasisi za serikali hazipaswi "kununua" (acquisition) magari au vitu ambavo ni second hand. Kwa hiyo japo magari haya yanatolewa bure kwa hizi taasisi za serikali, kimsingi hili linakiuka sera ya taasisi za serikali kutoingiza kwenye leja zao za umiliki wa mali vitu magari ambayo ni "used".
Nini kifanyike basi?

Ningemshauri Rais Magufuli kwamba haya magari yapigwe mnada na fedha zitakazopatikana ziingizwe kwenye shughuli zinazohusiana na kupambana na uhujumu uchumi nchini, ili wakamate magari mengi hata zaidi!
Mkuu pole kwa kunyang'anywa mchuma wako. Safari ijayo acha janja janja...
 
Iwanununulie kwa bajeti ipi mkuu. Why huoni jema kwenye kitu direct hivyo. Kasema kule ambako Kuna Shida hasa wananchi kupata huduma. Watu kama nyie sijui Ni Perfect kiasi gani. Lakini kisaikologia the opposite is true.
Shida si kutoa bure,shida ni kumaintain hizi used cars uelewe, utawapa service ni ghari mno.sijui hakili then huwa mnashikiwa na nani??
 
Ni kweli una mawazo mazuri ila najiuliza Range Rover ukiipeleka kwenye taasisi kila mtu atataka iwe yake ambae ni boss...Lakini pia mnada nao wangesema ooh wameuziana magari yaani Uongozi ni shidaaa.

You can’t win![emoji3]
 
Lazima watu wapige hela hapo kwenye suala la maintenance. Si vibaya hata yakipelekwa huko remote areas za nchi yakasaidie shughuli mbalimbali za kiserikali watu wapate maendeleo
 
Me Naita ni Dhulma...

Yaani mimi ninunue gari langu rafiki au Dereva wangu alifanyie madambwa ndio litaifishwe? laani itampata mtu hakika... Mwenyezi Mungu asikie kilio cha wamiliki... wasiohusika...

Tunapoelekea hadi Daladala zitashikwa Polic wakimkimbiza au wakimuona mtu wamshuku ana bangi ndani ya Daladala wanamkamata na gari lenyewe pia wanalitaifisha... hapana jamani ni dhulmati... Anayetakiwa kushikwa ni utawala aliyepokea mzigo au kupandisha hao watu kama wahamiaji haramu n.k... Ina Maana hata Mkuu mwenyewe ana hotel siku wakimshuku jambazi au mfanya biashara haramu wanavamia hotel kisha Wanamkamata na kisha kuitafisha Hotel... hii sio Sawa kabisa
 
Yaani ni uzulumaji tu, plain and simple
Haya yalikuwa yanatokea sana enzi zile za ujamaa
Hakuna chochote kilisaidia nchi
Ni upuuzi wa vi nchi vya kikomunisti njaa ambavyo haviwezi kujitegemea, badala ya kuangalia China inaweza vipi .
Vi RAV 4 ya mwaka 96 sijui vitaisadia vipi nchi
 
Back
Top Bottom