Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amepania kurejesha kwa nguvu mfumo wa chama kimoja nchini


Wacha kulia nyau, wewe ndiye ulimpa madaraka? Kwanza pengine hata kura hukupiga then unakuja kulialia hapa kama nyau. Leta facts usiandike majungu. Ningekubali hoja yako kwamba mambo anayofanya JPM yaani kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo itauwa upinzani ningekuelewa.
 
Naomba kuuliza tu,hivi daktari na mlinzi wa magufuli nao ni watanzania ?any way sijui kwa nini nauliza hili swali
 

Ole ,
Wewe ni Nyang'au tu!
Tunajua Policcm,NEC na UWT ndio waliompa madaraka JPM! Hili unalijua ma JPM anajua hivo. Mstahafu Mkapa katika kitabu chake:My LIfe, My Purpose ameweka wazi kuwa FEDHA YA EPA ILIMWINGIZA KWENYE URAIS Mgombea wa CCM…! Sasa unataka FACTS gani we nyang`au?
 
THE SEAL,
Wazungu hawakutaka kabisa Marekani ipate rais mweusi lakini Mungu aliposema ndiyo hakuna aliyeweza kumzuia Obama.

Kuna siku ambayo CCM itaishiwa mbinu zote na upinzani kuingia madarakani. Ninamuomba Mungu aniweke hai nilishuhudie hili.
That day is not far, 2020 will not end with a ccm president, take that to the bank my sister, you cant kill people, ruin the economy, pump 37 bullets on an opposition mp and you think you will live long, NO WAY,
 
kama mwenyekiti wa CCM Hilo ni jukumu lake muhimu
 

Mystery,
Achana na huyo mnafiki mkubwa Bw. Pascal Njaa…!Naona anajitahidi kutetea upuuzi wa CCM ili JPM amkumbuke angalau hata u~DC!
 
Huyu jamaa Siasa kwake ni mtihani mkubwa kwake hasa siasa za ushindani ndiyo hazitaki kabisa.Nikirejea yale aliyo mfanyia mshindani wake kwenye chama kipindi cha kugombea uteuzi wa kuwania Ubunge huko kwao .
 
Mzalendo 2015
Tatizo lako wewe ulikuwa mfaidika mkubwa wa awamu ya BWM na JK hivyo ule mlo wako umekatwa kwa sababu Chuma kiko Ikulu. Endelea kuwewesekaweweseka tu lakini unafahamu kifo cha mende unacho. Unaongelea BMW aliyeuza viwanda vyote alivyoanzisha Mchonga na mashirika yote ambayo mchonga aliyaacha. JPM Jembe na mtakoma ubishi, hakitoki kitu hapa. Hapa kazi tu!
 
Eeenh, napinga mlinganisho huo.
Yule ,Mama' wa 'Nobel' mbona siku hizi hasikiki, au kwa vile mlimpa ulaji kajisahau?
Yupi huyo? Tanzania haijawahi kuchaguliwa kwa Nobel prize najua ni Prof. Mathai tu RIP.
 
Kama JPM anatekeleza ipasavyo ilani ya CCM, ambapo kama unavyodai wewe kila mtu anaona, ni kwanini basi anaogopa mno kupambanishwa na vyama vya upinzani??

Angeruhusu uchaguzi ulio huru na hao wananchi unaosema wanaona hayo maendeleo, wapige kura kwa kumpa ushindi wa kishindo

Siyo kuihadaa dunia kuwa tunafanya chaguzi, wakati in real sense, tunachofanya ni UCHAFUZI!
 
Ulimpima kwa meter gauge gani kuona hiyo hofu?
Jamaa hana hofu, yeye ni kazi tu 24/7.
Mwenye hofu ni Chadema
 
Ulimpima kwa meter gauge gani kuona hiyo hofu?
Jamaa hana hofu, yeye ni kazi tu 24/7.
Mwenye hofu ni Chadema
Hivi ni kwanini nyinyi maccm tunapousema ukweli kuwa Magu anauogopa sana upinzani, mnakana kuwa siyo kweli??

Sasa mbona tunapowauliza maswali ya msingi, kuwa iweje aendeshe uchaguzi huu wa serikali za mitaa kwa uhuni wa kiwango hiki, mnakosa majibu!
 
Hakuna jambo hata moja analofanya JPM linaloweza kuua upinzani isipokuwa ukandamizaji wa demokrasia. Hivi umejiuliza kwa nini atoe maagizo kwa watendaji wa kata ambao ni wasimamizi wa uchaguzi waharibu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwaengua wagombea wote wa upinzani!!?
Anatambua nguvu ya upinzani. Hapo alipo yeye ni zao la upinzani. Sema tu mtu mwenyewe inawezekana hata maana ya neno "demokrasia" atakuwa haelewi. Sababu kubwa ni kuwa vyuo vya uongozi wa umma nchini ni kizungumkuti.
Anaweza kuwa anaamini 'demokrasia' ni barabara ya lami, flyover, ndege, sgr au stiegler's gorge!!! Kwamba demokrasia ni pamoja na Uhuru na haki za kiraia, kwake ni kiza kinene.
Nasema hivi kwa sababu sioni ni kwa sababu zipi za msingi kwamba Rais mwenye PhD katika karne ya 21 atamani kutawala kwa mfumo wa Chama kimoja!!! Yalipofanywa na akina Idd Amin au Bokasa, tulielewa ni 'inferiority complex', maana wale walikuwa ni darasa la nne la zamani!!!
 
Naomba kuuliza tu,hivi daktari na mlinzi wa magufuli nao ni watanzania ?any way sijui kwa nini nauliza hili swali
Hao ni wa kutoka nchi jirani, kwa yule Best friend wake, anayefahamika kwa initials za PK

Huyu jamaa amefikia hatua ya kutowaamini kabisa watanzania!
 
Kwanza nakupa hongera kwa kupenda kuchukuwa mawazo ya upande mmoja nakuyafanya ndio sahihi bila ya kuyabalance.Pili ningependa kukuweka sawa hakuna Rais ameeonekana au kusikika akiwapa maelekezo watendaji wake kuhusiana na uchaguzi, ninavyojua ni pale Rais anapokuwa ziarani na kutaka kujua kero za wananchi halafu mhusika hayupo hapo utakuta lipo chini ya vyama pinzani sasa huoni hizo ni dharau Rais atawezaje kuwasaidia wananchi wakati wawakilishi wao hawapo na ndio maana anakuwa anatoa kauli za kuwataka wananchi kuchagua viongozi wanaofaa sasa hapo ni kosa. Kuhusu fomu kumbuka vyama pinzani vilishasusia kabla hata ujazaji fomu kuanza huoni kuwa walikuwa na lengo la kususa kabla ya kujaza fomu?hapo walishaona mambo mazuri yanayofanyika wakaona watumie mbinu hizo ili ionekane wanaonewa kwa kuwaweka wagombea wasiowapa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu na pia kila chama kina mwanasheria wake na ilikuwa unavyojaza fomu unatakiwa ugongewe mhuri na katubu wake hilo nalo utalizungumziaje. Wagombea wa ccm waliweza kujaza fomu vizuri ni kutoka na kupewa maelekezo mazuri na wanasheria wao. Pia kumbuka vyombo vya ulinzi na usala vipo kwa ajili ya usalama wa wananchi wake na sio ccm pekee, hao wengine wanavunja sheria na ndio maana unaona kama wanaonewa. Hivyo nakushauri uwe unajitahidi kutafuta taarifa vizuri na kuzilinganisha la sivyo baadae utakuja kujilaumu na muda utakuwa umeshapita.
 
Hao ni wa kutoka nchi jirani, kwa yule Best friend wake, anayefahamika kwa initials za PK

Huyu jamaa amefikia hatua ya kutowaamini kabisa watanzania!
Sasa siku akimkorofisha PK ndo maisha yake yameishia hapo
 
Kwa rais kujua shida za wananchi wake lazima afanye ziara,sasa hiyo representation tunayoambiwa niya nini na tunawakilishwa kwa nani?Je hiyo ya wapinzani kutokujumuika kwenye ziara za rais imeanza tangu 1992 au wakati huu wa Magufuli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…