Tetesi: Rais Magufuli amewaita mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje

Tetesi: Rais Magufuli amewaita mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje

Tanzania hii hii inabeba tena gharama za kuwasafirisha Mabalozi hao!!! Mishahara imegoma kuongezwa
 
Nyie wakati "ujumbe mzito" umeenda Ulaya kulalamikia ukuta kwa nini msingekata gharama hizo kwa kutembelea balozi za Ulaya hapa Dar?
Mbona mlisema hawaendagi wanajificha hapo dar? Kwani safari za nje zimeruhusiwa?
 
Si aite anaotaka kuwatimua,yanini kuwasumbua wengine?
Kwa wale watakaopenya, maana kutakuwa na mchujo mkali tu, watakaopenya anataka aongee nao uso kwa uso majukumu yao ni nini huko watakoenda.
Wengi hujisahau, hawaitangazi nchi ipasavyo kama vivutio na fursa zilizopo huku.
 
Gharama zipi wakati tuna madege mawili mapya bombardier?
 
Kodi wanajitahidi kuzikusanya ila matumizi sasa
 
Hapo kuna wengine mizigo yao itawaguata hukuhuku aisee karibuni nyumbani sukari imeshuka bei kiasi
 
Kuna tetesi kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Johm Pombe Magufuli amewaita mabalozi wote wawakilishi wa Tanzaina nchi za nje kwenye mkutano utakaofanyika Ijumaa (kesho) Ikulu jijini Dar-Es-Salaam.

Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mabadiliko makubwa katika safu ya mabalozi hao pamoja na utendaji wa ujumla katika vituo vyao vya kazi. Habari zaidi zinanyetisha kwamba kabla ya mkutano huo kati ya mabalozi wote na mh. Rais, mabalozi hao watafanya mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mh. Agustine Mahiga hii leo.
Nashauri mabalozi walioko EU waondolewe warudi nyumbani, maana ni wabinafisi, wazembe na wanalugha mbovu sana. Hawana msaada kwa watanzania, ni wakorofi, si wabunifu wala wa kujituma. Wao hudhani kila mtanzania aliyenda ulaya kaenda kwa matatizo. Yaani wanachukiza sana!
 
Back
Top Bottom