Tetesi: Rais Magufuli amewaita mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje

Tanzania hii hii inabeba tena gharama za kuwasafirisha Mabalozi hao!!! Mishahara imegoma kuongezwa
 
Nyie wakati "ujumbe mzito" umeenda Ulaya kulalamikia ukuta kwa nini msingekata gharama hizo kwa kutembelea balozi za Ulaya hapa Dar?
Mbona mlisema hawaendagi wanajificha hapo dar? Kwani safari za nje zimeruhusiwa?
 
Vipi Lizaboni Olesendeka Moendazoe Na msindai wamo ktk Orodha?
 
Si aite anaotaka kuwatimua,yanini kuwasumbua wengine?
Kwa wale watakaopenya, maana kutakuwa na mchujo mkali tu, watakaopenya anataka aongee nao uso kwa uso majukumu yao ni nini huko watakoenda.
Wengi hujisahau, hawaitangazi nchi ipasavyo kama vivutio na fursa zilizopo huku.
 
Gharama zipi wakati tuna madege mawili mapya bombardier?
 
Kodi wanajitahidi kuzikusanya ila matumizi sasa
 
Hapo kuna wengine mizigo yao itawaguata hukuhuku aisee karibuni nyumbani sukari imeshuka bei kiasi
 
Nashauri mabalozi walioko EU waondolewe warudi nyumbani, maana ni wabinafisi, wazembe na wanalugha mbovu sana. Hawana msaada kwa watanzania, ni wakorofi, si wabunifu wala wa kujituma. Wao hudhani kila mtanzania aliyenda ulaya kaenda kwa matatizo. Yaani wanachukiza sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…