Rais Magufuli amkaanga vikali Waziri Kamwelwe, atishia kumuweka ndani kwa Uhujumu Uchumi

Rais Magufuli amkaanga vikali Waziri Kamwelwe, atishia kumuweka ndani kwa Uhujumu Uchumi

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
March 16, 2020

Kilosa, Morogoro



Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli akiwa wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro akifanya ukaguzi wa daraja muhimu kwa taifa la Kiyegeya lililobomoka Machi 2, 2020 kufuatia mvua nyingi alionesha kutoridhishwa na utendaji wa safu za wateule wake hasa Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano injinia Isack Kamwelwe (Mbunge wa jimbo la Katavi) kupitia CCM. Injinia Kamwelwe alipata kuwa meneja mkoa wa TANROAD na pia ofisa ngazi za juu TANROAD makao makuu kabla ya kujiingiza ktk siasa kupitia CCM.

Mh. Rais kuonesha mapungufu ya watendaji wake hakusita kumungunya maneno kiasi cha kusema ana hisia kuwa wateule wake wanahujumu juhudi na kufananisha kadhia hiyo na "Economic Sabotage" uhujumu wa uchumi wa nchi, maana daraja hilo si tu linaunganisha Tanzania bali pia na nchi za maziwa makuu za Burundi, Rwanda, DR Congo zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

Rais Magufuli akawaomba msamaha wananchi wa Kilosa na Tanzania kwa madhila makubwa yanayowakabili ikiwemo daraja lingine la wilaya hiyo kubomoka na hivyo wananchi kupata changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kufika ktk hospitali kubwa kutokana na daraja lao kutofanyiwa matengenezo baada ya daraja lao pia kusombwa na mafuriko.

Katika safari yake toka Dar es Salaam mpaka Kilosa alisimama mara kadhaa na kusikia vilio vingi vya wananchi wa mikoa ya Pwani na Morogoro juu ya utendaji hafifu wa wateule wake ktk sekta za afya, elimu na miundo mbinu ya barabara. Wananchi walionesha matamanio yao kuhusu sekta mbalimbali hayapewi vipaumbele na watendaji wa serikali waliopo maeneo yao.
 
Hii iliyompata Engineer Isack Kamwelwe leo inapaswa aandike barua ya kujiuzulu ili kuwajibika kama waziri bila kusuburi alazimishwe kama Kangi Lugola.

Itakuwa jambo la kiungwana akikubali kama kiongozi kuwajibika kwa kujiuzulu kuliko kuendelea kukaa ofisini aking'ang'ania nafasi hiyo ya kisiasa iliyomletea mtafaruku mkubwa na bosi wake leo hii.
 
Kamwere hawezi kuwachia ngazi kwa hiari yake, ref kuzama kwa kivuko cha mv Ukara watu waliotoa maoni yao kuwa ajiuzuru Kamwere akajitokeza kuwa hao wanao msema hivyo atawakamata awashitaki.
Hii iliyompata Engineer Isack Kamwelwe leo inapaswa aandike barua ya kujiuzulu ili kuwajibika kama waziri bila kusuburi alazimishwe kama Kangi Lugola.

Itakuwa jambo la kiungwana akikubali kama kiongozi kuwajibika kwa kujiuzulu kuliko kuendelea kukaa ofisini aking'ang'ania nafasi hiyo ya kisiasa iliyomletea mtafaruku mkubwa na bosi wake leo hii.

In God we Trust
 
Nilitaka kushangaa we Bagamoyo uandike namna hii kuhusu JPM ...….. ….... …. nimeona source baada ya kumaliza. Thanks.

Unajua habari kama hii lazima uiandike kama ilivyo kwanza, halafu ktk comments baadaye tunaweka post inayojitegemea yenye comments zetu binafsi.

Hii ni kuzingatia kanuni bora za uandishi na viwango bora vya kupashana habari husika hapa Jamiiforums.

Namna hii tunawavutia wanaLumumba wasiwe wanasita au kukaa pembeni bila ku comment kuhusu habari inayohusu Taifa letu. Hasahasa pale watendaji wa serikali ya CCM Mpya wanapoonesha kukosa ubunifu wa kutatua Kero za wananchi au taifa.
 
Kiukweli huo ni uhujumu haswa


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom