Rais Magufuli amkaanga vikali Waziri Kamwelwe, atishia kumuweka ndani kwa Uhujumu Uchumi

Rais Magufuli amkaanga vikali Waziri Kamwelwe, atishia kumuweka ndani kwa Uhujumu Uchumi

Ila mkumbuke mvua hizi si za kawaida hii hali ya mvua hizi niclimate change in africa sehemu nyingine mf rufiji hawajashuhudia mafuriko haya kwa zaidi ya miaka 30

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli unayosema ila jitihada ilitakiwa ifanyike sana
Wangepiga kazi usiku na mchana kuhakikisha panapitika ila wamefanya uzembe sana Mkuu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
March 30, 2018

Katibu Uenezi wa CCM, Ndg. Humphrey Polepole akikagua ujenzi wa barabara ya Ifakara - Kidatu mkoani Morogoro ambayo ni ya urefu wa kilometa 67 inayofadhiliwa na EU, Shirika Maendeleo la Uingereza na nchi ya Marekani huku mkandarasi wa ujenzi ni kampuni ya Reynolds Construction toka Nigeria.

2017
Wahisani waliotoa fedha wa kwa ajili ya barabara hiyo ya Ifakara - Kidatu na ujenzi wa daraja ni EU, Shirika la Maendeleo la Uingereza na USAID na mkandarasi wa ujenzi wa barabara ni kampuni ya Reynolds Construction toka Nigeria.

March 16, 2020

Kilosa, Morogoro

Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli akiwa wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro akifanya ukaguzi wa daraja muhimu kwa taifa la Kiyegeya lililobomoka Machi 2, 2020 kufuatia mvua nyingi alionesha kutoridhishwa na utendaji wa safu za wateule wake hasa Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano injinia Isack Kamwelwe (Mbunge wa jimbo la Katavi) kupitia CCM. Injinia Kamwelwe alipata kuwa meneja mkoa wa TANROAD na pia ofisa ngazi za juu TANROAD makao makuu kabla ya kujiingiza ktk siasa kupitia CCM.

Mh. Rais kuonesha mapungufu ya watendaji wake hakusita kumungunya maneno kiasi cha kusema ana hisia kuwa wateule wake wanahujumu juhudi na kufananisha kadhia hiyo na "Economic Sabotage" uhujumu wa uchumi wa nchi, maana daraja hilo si tu linaunganisha Tanzania bali pia na nchi za maziwa makuu za Burundi, Rwanda, DR Congo zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

Rais Magufuli akawaomba msamaha wananchi wa Kilosa na Tanzania kwa madhila makubwa yanayowakabili ikiwemo daraja lingine la wilaya hiyo kubomoka na hivyo wananchi kupata changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kufika ktk hospitali kubwa kutokana na daraja lao kutofanyiwa matengenezo baada ya daraja lao pia kusombwa na mafuriko.

Katika safari yake toka Dar es Salaam mpaka Kilosa alisimama mara kadhaa na kusikia vilio vingi vya wananchi wa mikoa ya Pwani na Morogoro juu ya utendaji hafifu wa wateule wake ktk sekta za afya, elimu na miundo mbinu ya barabara. Wananchi walionesha matamanio yao kuhusu sekta mbalimbali hayapewi vipaumbele na watendaji wa serikali waliopo maeneo yao.

Sasa waziri asikofanya vizuri na wewe ndio mmemchagua kama
Raisi. Wananchi hawataki malalamiko na TV bali suluhisho
 
March 21, 2020

Barabara ya mchepuko Kiyegeya yakamilika

Makalavati ya zege kwa ajili ya ujenzi SGR Reli yaliyonunuliwa kwa dharura na serikali toka kampuni ya Yapi Merkezi yakamilisha ukarabati barabara ya mchepuko daraja la Kiyegeya barabara ya Morogoro - Dodoma.

Source : Azam TV
 
''Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.'' Maagizo ya JPM kuhusu ujenzi wa daraja hili waziri alipewa siku saba kuponyesha kibarua chake, chezea JPM wewe! Ama kweli Tanzania tumepata rais mambo ya kubembelezana ya enzi zile yamekwisha. Good job and salute to Mr. President, kama Watanzania hatutatoboa wakati wa JPM basi tusahau.
 
March 22, 2020
Rufiji, Pwani
Tanzania

Barabara iendayo mradi wa umeme Stiegler's Gorge
Mbunge wa Rufiji mkoani Pwani Mh. Mohamed Mchengerwa akielezea hali ya barabara jimboni kwake kama ilivyo katika video inayotoka Kibiti kwena Ikwiriri, Mkongo, Ngororo, Mloka mpaka katika mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere HydroPower Project ilivyo na kukwamisha uwezekano wa ndoto ya nchi mradi kukamilika ktk muda uliopangwa:

Source : Millard ayo
 
Hapa ndipo uwaziri ulipoota mabawa
March 16, 2020

Kilosa, Morogoro

Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli akiwa wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro akifanya ukaguzi wa daraja muhimu kwa taifa la Kiyegeya lililobomoka Machi 2, 2020 kufuatia mvua nyingi alionesha kutoridhishwa na utendaji wa safu za wateule wake hasa Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano injinia Isack Kamwelwe (Mbunge wa jimbo la Katavi) kupitia CCM. Injinia Kamwelwe alipata kuwa meneja mkoa wa TANROAD na pia ofisa ngazi za juu TANROAD makao makuu kabla ya kujiingiza ktk siasa kupitia CCM.

Mh. Rais kuonesha mapungufu ya watendaji wake hakusita kumungunya maneno kiasi cha kusema ana hisia kuwa wateule wake wanahujumu juhudi na kufananisha kadhia hiyo na "Economic Sabotage" uhujumu wa uchumi wa nchi, maana daraja hilo si tu linaunganisha Tanzania bali pia na nchi za maziwa makuu za Burundi, Rwanda, DR Congo zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

Rais Magufuli akawaomba msamaha wananchi wa Kilosa na Tanzania kwa madhila makubwa yanayowakabili ikiwemo daraja lingine la wilaya hiyo kubomoka na hivyo wananchi kupata changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kufika ktk hospitali kubwa kutokana na daraja lao kutofanyiwa matengenezo baada ya daraja lao pia kusombwa na mafuriko.

Katika safari yake toka Dar es Salaam mpaka Kilosa alisimama mara kadhaa na kusikia vilio vingi vya wananchi wa mikoa ya Pwani na Morogoro juu ya utendaji hafifu wa wateule wake ktk sekta za afya, elimu na miundo mbinu ya barabara. Wananchi walionesha matamanio yao kuhusu sekta mbalimbali hayapewi vipaumbele na watendaji wa serikali waliopo maeneo yao.

lipo
 
Back
Top Bottom