mkaruka ataja rinu
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 3,527
- 2,469
March 16, 2020
Kilosa, Morogoro
Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli akiwa wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro akifanya ukaguzi wa daraja muhimu kwa taifa la Kiyegeya lililobomoka Machi 2, 2020 kufuatia mvua nyingi alionesha kutoridhishwa na utendaji wa safu za wateule wake hasa Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano injinia Isack Kamwelwe (Mbunge wa jimbo la Katavi) kupitia CCM. Injinia Kamwelwe alipata kuwa meneja mkoa wa TANROAD na pia ofisa ngazi za juu TANROAD makao makuu kabla ya kujiingiza ktk siasa kupitia CCM.
Mh. Rais kuonesha mapungufu ya watendaji wake hakusita kumungunya maneno kiasi cha kusema ana hisia kuwa wateule wake wanahujumu juhudi na kufananisha kadhia hiyo na "Economic Sabotage" uhujumu wa uchumi wa nchi, maana daraja hilo si tu linaunganisha Tanzania bali pia na nchi za maziwa makuu za Burundi, Rwanda, DR Congo zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.
Rais Magufuli akawaomba msamaha wananchi wa Kilosa na Tanzania kwa madhila makubwa yanayowakabili ikiwemo daraja lingine la wilaya hiyo kubomoka na hivyo wananchi kupata changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kufika ktk hospitali kubwa kutokana na daraja lao kutofanyiwa matengenezo baada ya daraja lao pia kusombwa na mafuriko.
Katika safari yake toka Dar es Salaam mpaka Kilosa alisimama mara kadhaa na kusikia vilio vingi vya wananchi wa mikoa ya Pwani na Morogoro juu ya utendaji hafifu wa wateule wake ktk sekta za afya, elimu na miundo mbinu ya barabara. Wananchi walionesha matamanio yao kuhusu sekta mbalimbali hayapewi vipaumbele na watendaji wa serikali waliopo maeneo yao.
Wasaidizi wa Rais wengi wao wanamuangusha sana,kila jambo hadi Rais aseme asiposema wanabakia wanarumbana tu hakuna kinachoendelea. Wananchi wa kule Mwanza wanaoishi maeneo ya barabara kutoka Mkuyuni-Mahina-Kanyerere-Nyangulugulu hadi Mwatex ni kama wanaishi uhamishoni maana barabara wanayotumia si barabara bali ni maandaki. Mbunge wa Nyamagana yupo, DC wa Nyamagana yupo, RC wa Mwanza yupo, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mwanza yupo, Waziri yupo lakini watendaji hao walifikia hatua ya kuwatishia wananchi waliotaka kumwambia Mheshimiwa Rais kuhusu kero ya barabara hiyo alipokuwa maeneo ya Iseni pale Butimba Mwanza wasiseme. Rais unayajua hayo? Unahujumiwa