Rais Magufuli amkaanga vikali Waziri Kamwelwe, atishia kumuweka ndani kwa Uhujumu Uchumi

Udhalilishaji tu ,unamfanya waziri kama muhudumu wa baa.This is character assassination. Just respect them ,you don't have to shout public.
Hata wahudumu wa bar ni binadamu. Waheshimiwe pia.
 
Udhalilishaji tu ,unamfanya waziri kama muhudumu wa baa.This is character assassination. Just respect them ,you don't have to shout public.
Hapana, that was a correct approach by mr President, nchi hii ina watu wamepewa mamlaka lkn wanafanya vitu na maamuzi ya hovyo huwezi amini, na unakuta ni wasomi kweli. binafsi nadhani hamna namna nyingine zaidi ya kuwakosoa hadharani ili na wengine wabadilike, nb: nilikuwa muhanga wa daraja hilo kama msafiri.
 
Kosa lake nini?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa viongozi wetu nao wakati mwingine kuna mambo mengine wanajitakia, hawajui kuwasoma viongozi wao. Mimi ningekuwa waziri kwenye Serikali ya JPM, ningekuwa mwangalifu sana na PM, kuliko hata Rais mwenyewe. Mimi ninaona kam PM ni mkali pengine kumzidi hata Mkuu wa Kaya, lakini sidhani kama wote wameshaliona hilo. Ningesikitika mno kumkosa Kamwele, kazi nzuri anayofanya. Mara nyingi mimi maamuzi ya JPM huwa yananipa amani sana isipokuwa tu pale anapokuwa ametumbua watu kama akina Kamwele. Kwa sababu kuna mtu mwingine kweli sababu ya kutumbuliwa inakuwa ipo na ipo valid lakini bado mnamumiss, case kama ilivyokuwa ya Simbachawene kabla hajarudi tena kwa mara ya pili. From my heart, Kamwele angetoka ningekosa amani kabisa
 
Ila jiwe anadhalilisha sana watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye akikosolewa hadharani unajua ambacho huwa anafanya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maamuzi gani ya wasomi,nikikwambia hilo daraja liliombewa pesa tangu 2015 na likapuuzwa na huo hao wanaowafokea utasemaje.Mtu hawezi kubadilika kwa kufokewa wewe mtu anabadilika kwa kuonywa kwa kutumia mifumo imara ya uongozi na malezi ya makuzi imara.Unaweza kumfokea mtu akawa na nidhamu ya uoga tu .Tujenge culture ya uwajibikaji .Mimi nikiona mtu ananifkea mbele za watu najua asilimia 100 ajiamini hata kidogo ni mwoga au ameadhirika kisaikologia .Iwe kazini au mahusiano ni ugonjwa
 
Maigizo tu. Hivi watu hawawezi kukarabati daraja au kipande cha barabara bila hizi drama na macamera. Mbona hatusikii haya nchi nyingine na mambo yanakwenda.
 
Haya mambo ndio tunaambia watu humu mara kwa mara. Waziri au kiongozi yoyote hahitaji kutoka ofisini kwenda site kufokea watu mbele ya macamera ya wandishi wa habari. Yule Prof. Ndalichako alijikuta anajiaibisha kwa English mbovu baada ya kukurupuka kwenda kufokea wachina huku kafuatana na waandishi wa habari kutafuta kiki, kiki zikamtokea puani.
'Chains of command' zinafahamika! Mifumo ya kiutawala na managementi pia inajuliakana! Mbona kama viongozi siku hizi wanatumia sana approach ya micromanagement?
 
Hii movie ya leo wote wawili, Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Kamwele wamezitendea haki nafasi walizo act.
 
Inawezekana Mheshimiwa akagoma kutukarantini watanzania dhidi ya corona kwa kisingizia cha economic sabotage, sababu ideally ni lazime tule movement ban kwa takribani siku hizo hizo 14, hakuna kitu kitatembea kwenye hizo barabara kwa kipindi hicho.
 
Asimame pia hapo Segerea azungumze na Wale waliowapiga Wanawake. Hili aslifumbie macho wala asipite hivi.Wameliaibisha taifa.
Jiwe mwenyewe kaliingiza taifa mkenge vitu kibao aanze yeye kuachia nafasi kama kweli mzalendo au makosa akifanya mwingine ila kwake sahihi?😁😁😁
 
Mwambie na yeye awe tayari kukosolewa hadharani sio kukosoa na kukemea wengine tu ebo!!πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Bagamoyo,
Vilio vya wananch ni sahihi kabisa na hata mimi naamini kwamba kwa jinsi mambo yalivyo,juhudi za Rais kuwaletea Watanzania maendeleo zinahujumiwa.Hili tumelisema mara nyingi huko nyuma,na kwa vile kalishuhudia yeye mwenyewe,labda sasa atakuwa makini zaidi katika kupokea ushauri wa washauri wake katika teuzi mbali mbali,kwa kuwa inawezekana nao wanamhujumu.
 
Kile kiyoyozi cha kwenye V8 unafikir mchezo nn kupita na ving'ora kuna raha yake bwana anaanzaje kujiuzulu kirahis

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…