March 16, 2020
Kilosa, Morogoro
Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli akiwa wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro akifanya ukaguzi wa daraja muhimu kwa taifa la Kiyegeya lililobomoka Machi 2, 2020 kufuatia mvua nyingi alionesha kutoridhishwa na utendaji wa safu za wateule wake hasa Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano injinia Isack Kamwelwe (Mbunge wa jimbo la Katavi) kupitia CCM. Injinia Kamwelwe alipata kuwa meneja mkoa wa TANROAD na pia ofisa ngazi za juu TANROAD makao makuu kabla ya kujiingiza ktk siasa kupitia CCM.
Mh. Rais kuonesha mapungufu ya watendaji wake hakusita kumungunya maneno kiasi cha kusema ana hisia kuwa wateule wake wanahujumu juhudi na kufananisha kadhia hiyo na "Economic Sabotage" uhujumu wa uchumi wa nchi, maana daraja hilo si tu linaunganisha Tanzania bali pia na nchi za maziwa makuu za Burundi, Rwanda, DR Congo zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.
Rais Magufuli akawaomba msamaha wananchi wa Kilosa na Tanzania kwa madhila makubwa yanayowakabili ikiwemo daraja lingine la wilaya hiyo kubomoka na hivyo wananchi kupata changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kufika ktk hospitali kubwa kutokana na daraja lao kutofanyiwa matengenezo baada ya daraja lao pia kusombwa na mafuriko.
Katika safari yake toka Dar es Salaam mpaka Kilosa alisimama mara kadhaa na kusikia vilio vingi vya wananchi wa mikoa ya Pwani na Morogoro juu ya utendaji hafifu wa wateule wake ktk sekta za afya, elimu na miundo mbinu ya barabara. Wananchi walionesha matamanio yao kuhusu sekta mbalimbali hayapewi vipaumbele na watendaji wa serikali waliopo maeneo yao.
For sure kabisa, hapa kwa mara ya pili au ya kwanza nakubaliana na Magufuli....
Ni ngumu sana kuamini kuwa daraja kama hili limekatika two weeks ago lakini halijajengwa na sisi ni nchi....!!
Kwa kiongozi makini alitakiwa kujua kuwa daraja hilo ni kiungo muhimu zaidi ya 98% ya eneo lote la nchi yetu achilia mbali nchi jirani hizi; DRC, Zambia, Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda....
Lakini cha ajabu siku 14 nothing has been serious done...!!
Tatizo ni nini? Fedha hakuna? Kuogopa kufanya maamuzi? Kukwamisha tu mambo or what??
USHAURI KWA MZEE KAMWELWE;
Nimekutazama na kukuona jinsi ulivyokuwa mnajibizana na mwanaCCM mwenzako. Nikakuona umekuwa mdogo kama piriton na sijui kama hukumwaga maji chini.....
Binafsi nimekuhurumia sana na kwa hakika kuna kitu kinakusumbua lakini ulishindwa kukisema mbele ya Rais wako....
Sasa basi, kama msamaha wako ulikubaliwa, nakushauri ukirudi ofisini ama nyumbani kwako, kaa chini kwa utulivu, andika barua ya kujiuzuru kwa heshima.....
Wewe ni Mzee, umeshakua, inatosha. Tawala za kiimla huwa zinapiga kotekote. Dikteta huweza hata kugeukia hata wenzake na "kuwala vichwa vyao" iwapo akiona unamharibia kufikia matamanio yake....
Usisubiri ufukuzwe ama "uliwe kichwa" na jamaa yenu huyo. Unaweza kupotelea kusikojulikana, shauri lako.....
Lakini kikubwa zaidi, nadhani, you are not fit for that job no matter whether you're an engineer or whatever. Kipimo cha ukomo wa uwezo wako, kilikuwa ni daraja hilo. You have failed Mzee.....!!
Waachie wengine kazi hiyo, pumzika kula pesheni yako kwa Amani.....!!!