Rais Magufuli amnyooshea kidole Mwele Malecela asema alitumiwa na mabeberu kutangaza ugonjwa 'hewa' wa Zika

Rais Magufuli amnyooshea kidole Mwele Malecela asema alitumiwa na mabeberu kutangaza ugonjwa 'hewa' wa Zika

Huwa najiuliza mengi nikona kwenye media kubwa za "mabeberu" kuwa huko kwao wazazi huwa wanagoma watoto wao kupewa chanjo za surua, polio nk,na hakuna wa kuwalazisha wakati kuku kwetu wazazi hata kupewa nafasi ya kuhoji hizo chanjo hakuna...tunaswagwa tu!
 
Hivi Tanzania mamlaka huwa zinafanyaje kazi?

Mathalani kama kuna mlipuko wa ugonjwa mkubwa kama Zika, si kwamba kabla ya kujulikana kwa wananchi Rais inabidi afahamishwe na waziri husika?

Ilikuaje Mwele kutangaza tamko kubwa kama lile pasipo kuwa na backup ya waziri wake?

Rais katoa jibu leo ya kilichojiri. #1
 
Kabisa jana nilimcheck akizungumuza nilimuhurumia anaonekana anajua ukwel ila ndo bas. Ila swala jingine kama jiwe anadai haogopi mabeberu mbona hofu nying, juz tu WHO kutamka kidogo tu watu jasho limewatoka kumbe mabeberu wanaguvu balaa. Sasa wamapambio wajipange kwan lissu ziara inaanza
Na bado wamepeka barua WHO ya kuomba USD 9.5 Million kununua dawa na vifaa vya kujikinga na Ebola
 
Hata vichaa hufanya vitu fulani. Kama kwako wewe mtu anaetumia kodi inayokusanywa kutoka kwa Watanzania wote kwenye miradi isiyokuwa na returns huku shule zikitoa elimu ya hovyo kupata kutokea ndie shujaa basi una matatizo makubwa kuliko unavyofikiri.
Hey!! Kumbe Tanzania kuna elimu ya hovyo iliyotolewa ktk miaka hii inayokaribia minne ya Magufuli? Hivi mnapimaje huo u hovyo, maana naamini walioanza std1 au form 1 2016 hata mitihani ya Taifa ya kumaliza elimu zao hawajafanya?
Au huu ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa, maabara za Sayansi na Teknohama, matundu ya vyoo na ukarabati mkubwa kwa shule kongwe ndio u hovyo wa elimu? Kweli midomo kazi yake kuongea lakini basi na macho iwe kazi yake kuona🙊🙊🙊
 
Mifumo ya kielimu yote ni ya kizungu
Siyo kweli... Kuna elimu za kiafrika hasa kwenye mambo ya dawa ambapo wazungu wamekuwa wakija kujifunza na kwenda kuuboresha na kuja na colored model.
 
Hivi Tanzania mamlaka huwa zinafanyaje kazi?

Mathalani kama kuna mlipuko wa ugonjwa mkubwa kama Zika, si kwamba kabla ya kujulikana kwa wananchi Rais inabidi afahamishwe na waziri husika?

Ilikuaje Mwele kutangaza tamko kubwa kama lile pasipo kuwa na backup ya waziri wake?
Lile tangazo lilikuwa na lengo la kuhamishia watalii wote Kenya
 
No, please, serology ilionyesha kuwa kuna antibodies against Zika virus! Means kuna infection .. au positive serology had a history of exposure to Zika, sijui kama umesoma immunobiology
Nyie ndio mkiona moshi mnasema gari limepita bila hata kuliona,kumbe kichaka kinaungua
 
Sometimes it needs to be smart or intelligent enough to understand the intelligent person.

Pia,wakati mwingine inahitaji uwe expert kumuelewa expert.
Uchaguzi wa ndani imewashinda mkuu Haya mengine yamewazidi kimo.
 
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.

Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
Vita ya kiuchumi, hivi Tanzania Vita ya kiuchumi imeanza baada Ya Magufuli kuwa Rais?
vita ya kiuchumi Tanzania inapigana na taifa gani na ktk bidhaa zipi? A fool leader deceives fool people
 
kwa sababu anazungumza mambo ambayo hampendi kusikia kwani yanawanyima fursa ya kuwatapeli watanzania.
HAPANA, SABABU UNAZIJUA KWANINI HAPENDWI, ILA UNACHOKIONA NI UNAFIKI WA NJAA MPAKA MTU ANJIITA JALALA LA MAVI
 
Back
Top Bottom