Jiwe amesoma Chemistry lakini hajaelimika. Sikutegemea Mwanasayansi kama yeye aje na argument ya uharo namna hii.
Kwanza kabisa NIMR ndiyo chombo cha juu nchini kinachotambulika kisheria katika utafiti wa magonjwa. Yeye kama Rais alitumia vigezo gani kujua ugonjwa upo au haupo?
Kwa mujibu wa Sheria na protocol za NIMR, wakiona dalili ya ugonjwa kutokana na Epidemiology report inayotayarishwa na idara ya kinga ya wizara watafanya utafiti kwa kuchukua sampuli. Na wakijiridhisha watatoa taarifa kwa ajili ya kutahadharisha wananchi.
Jiwe anasema eti ugonjwa haukuwapo wakati yeye ni mbumbumbu kwenye sayansi ya binadamu na magonjwa.
Watumishi wa Afya waliogopa sana kusema ukweli kwa kuwa wagonjwa wa zika walikuwapo. Na uwoga huo ukaendelea hadi kwenye dengue. Ugonjwa wa homa ya Dengue umeua watu zaidi ya 2000 tangu ulipoingia katikati ya 2018 hadi June 2019.
Watumishi wa afya wameamua kukaa kimya na kazi wamemuachia Waziri na Rais ndiyo wawajibike.