priniples ulizonazo pekee ni ubinafsi
Hapana, sina ubinafsi.
Ningekuwa na ubinafsi, ningekuwa ni kati ya watetezi wazuri sana wa Magufuli. Kwani, kwa kuangalia ubinafsi tu, Magufuli kainufaisha sana familia yangu.
Mimi nipo tofauti na ubinafsi, kwa kuwa, licha ya ukweli kwamba Magufuli kaifaidisha sana familia yangu, bado naweza kumkosoa pale ninapoona ameharibu.
Kwa kuangalia principles kama za kutoweka mbele ukabila, kutofanya mzaha wakuwatoa watu kwenye message muhimu ya sera za serikali, na kadhalika.
Kwa hivyo, naweza kuonesha kwamba, mimi najenga hoja ambazo hazikuchochewa na ubinafsi.
Siku moja nilikuwa naongea na binamu yangu, yupo Geneva Switzerland. Baba yake waziri serikalini, Nikawa nataka kujua habari fulani za serikali, huwa nasoma magazeti, halafu natumia pia mitandao ya familia kuhakiki habari.
Nikamuuliza, mbona serikali ya Tanzania inaachia fursa fulani? Imekuwaje hapo? Mzee wako anasemaje?
Akaniambia Kiranga, wewe si uko Marekani? Nikamwambia ndiyo.Akaniuliza, familia yako huko Marekani iko poa? Nikamwambia ndiyo. Akaniuliza una vibali vy kufanya kazi, unafanya kazi nzuri uliyosomea? Nikamwambia ndiyo. Akaniambia una biashara zako zinaenda vizuri, una nyumba umepangisha watu wanakulipa kodi poa? Nikamwambia ndiyo.
Akaniambia, sasa sikiliza.
Nakuomba sana, sana tu, sahau siasa za Tanzania. Sahau habari za Tanzania. Kama unaweza, tafuta kijana sharp mdogo katika familia, umsaidie aje Marekani umuondoe Tanzania. Siasa za Tanzania ukiziendekeza, zitakuumiza kichwa.
Nikamwambia sawa cousin, lakini wewe ni rahisi sana kusema hivyo, umeondoka Tanzania ukiwa na miakamitano, umesoma na kuishi ulaya maisha yako yote. Sisi wengine Marekani tumekuja kusoma chuo kikuu, kwa hivyo kusahau mizizi yetu Tanzania si kitu rahisi kama unavyosema wewe. Nitajaribu kufanya unachoshauri, lakini sifikiri kwamba nitaweza.
Sasa, ningekuwa na chembe ya ubinafsi, ningesema mimi niko Marekani, waache hawa Watanzania wapigane na hali yao huko.
Lakini, ukweli kwamba, hata baada ya kuwa Marekani, mambo yangu si mabaya, bado ninaona ni muhimu angalau kuchangia kimawazo, hapo inaonekana wazi kwamba sina ubinafsi. Kuna watu wangapi walio nje hata kujadiliana na watu wa Tanzania wanaona udhia tu?
Hao ndio wabinafsi.
Mimi ninayejaribu kumpigia mbuzi gitaa huwezi kunilaumu kwamba nina ubinafsi.
I have the exact opposite problem it seems.
I am too altruistic, even with my time alone.
Kwa sababu inaonekana clearly nampigia mbuzi gitaa, halafu bado naweka imani kwamba inawezekana akaelewa melody akaanza kucheza.
Wakati sina hata hakika kwamba masikio ya mbuzi yanasikia muziki!
Sasa hapo utasemaje nina ubinafsi?