Rais Magufuli amshangaa Spika Ndugai kuvaa barakoa akiwa peke yake Bungeni

Rais Magufuli amshangaa Spika Ndugai kuvaa barakoa akiwa peke yake Bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Magufuli amesema kwa taarifa alizopewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni kwamba DSM kuna wagonjwa wanne tu wa Corona.



Corona imekwisha ndio maana hata Mabarakoa hakuna hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndio maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu - Rais Magufuli

Ndugai.jpg

Maendeleo hayana vyama!
 
wale wahudumu wanaomletea vimemo pale kila baada ya dakika kadhaa hamuwaoni??

pale alipokaa yupo kwenye chumba chake peke yake anatumia hewa yake peke yake??

Hizo shule mlienda kusomea u-praise team??
Wale wahudumu wakivaa barakoa inatosha bwashee!
 
Shotii bado hajamsoma tu jiwe kuwa si muumini wa haya matambala, wenzake akina bashite na pm wanayavaa kwa kujificha, aje ajichanganye siku ayavae siku ya kuvunja bunge muone kama hajanaswa banzi la USO Huyo andunje!
 
Jiwe mbona yeye wakati wa Corona alikimbilia kujificha Chato sasa amerudi anadanganya watanzania kwamba Tanzania imebakia wagonjwa 4 wa Corona. Ila ukweli unajulikana kabisa ugonjwa bado upo unaendelea kuua watu majuzi tumempoteza rafiki yetu Dunia Mmliki wa Magari ya Marangu Coach kwa Corona ni bora watanzania wangeambiwa ukweli waendelee kuchukua tahadhari kuliko kuwadanganya
 
Speaker ana wahudumu wengi wanamfuata na kumhudumia, ni bora avae tu, mask sidhani kama inapunguza utendaji kazi wa mtu
 
Ila huwa inashangaza kweli muda mwingine...unakuta jitu lipo ndan ya gari yake tena pekeyake...limefunga vioo halafu bado limevaa barakoa

Elimu bado wengine hawajui vema, unakuta mtu yuko peke yake ktk gari amevaa mask, nawashangaa sana
 
Back
Top Bottom