Kweli tumevuka mipaka na kukubuhu kwenye mambo ya kienyeji na uongozi usio na kanuni. Tunapenda sana kufanya mambo bila utaratibu na miongozo ndio maana mambo mengi tunashindwa halafu tunashangaa kwanini tunashindwa. Sio viwanda au michezo tunaboronga bila kujua kwamba ni kwasababu ya kutashika kanunu na taratibu husika.
Huku Namibia ikimchamba rais wao kwa kutokuvaa barakoa, hapa kwetu spika anashutumiwa na boss wake kwa kuvaa barakoa.
Inashangaza.
Huku Namibia ikimchamba rais wao kwa kutokuvaa barakoa, hapa kwetu spika anashutumiwa na boss wake kwa kuvaa barakoa.
Inashangaza.
Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni rahisi tu, barakoa mbona imekaa kama titi moja la Mtu mmoja hivi limekatwa upande mmoja, weka huku kama... aaah samahani Mh.Waziri nimesema hapa, nilikuwa nachomekea tu kidogo”
Juzi nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari kuna group linaitwa Magufuli Forum wala silijui, ila sishangai Mtu kujiita Magufuli hata akijiita fisi ni hiyari yake, lakini walikuwa wanagawa barakoa wala hazijulikani zinatoka wapi, tutaumia kwa kukosa maarifa
Njia nyingine ambayo inaweza kutumika ni kuletewa vifaa vya corona vyenye corona, anapokuletea Mtu barakoa hujui ameitoa wapi kataa, mwambie kavae wewe na Mke wako na Watoto wako nyumbani, tutaumizwa