Rais Magufuli amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kupendekeza jina la PM Nov 19

Rais Magufuli amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kupendekeza jina la PM Nov 19

Namkumbuka kwa uvumilivu wake ukimlinganisha na Werema, mara nyingi Tundu kwa kupenda sifa alipenda kum-provoke kwa kumutita 'Mrithi wa Frederik Werema', lakini akamjibu kwa upole na hoja, kumbuka Tundu alikuwa na advantage mbili, au tatu, anajua sheria, anapenda sifa, na upepo ulikuwa kwake.

Lakini huyu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yuko pale kulinda Serikali iliyokuwa na madhalimu walioagiza vipengee vya katiba viondolewe wakijua wao ndio watakuwa Marais, wakapitisha Sheria ya Makosa ya Mtandaoni na Sheria ya Uchaguzi (marekebisho) kwa kuwa walijua wao ndio wagombea wa CCM... Well, huwezi kumlaumu, walikuwa anawatetea walaji, na sio kazi rahisi!

Kwa kuwa #KaziImeanza , natarajia aroll na kasi ya mpakwa mafuta, kivuli cha Julius Nyerere, akifeli tutasema....
 
lissu ni mropokaji tu hana lolote

Nina mashaka na upeo, uelewa uliokuwa nao katika maswala ya sheria! Kunaongelewa kingine na wewe unaleta utumbo ndo maana mnaishia kupewa Tshirt na fulana halafu mnaishi maisha ya kupiga mzinga kwetu.
 
Yale Yale. BWM alisema Mwanaume unayetaka Mabadiliko ushike mimba ha! ha! ha! Education Ma-S
CCM ni ileile ile ile
Umeitaka mwenyewe
Utaisoma namba
kwi! kwi! kwi!
Lissu yuko anashangilia anajua atapiga Knock out za kutosha!
Maskini Tanzania...............................
 
Badala ya kuangalia sera ambazo ni long term wewe unaangalia mtu, hapo ndipo uliposhindwa kushirikisha ubongo wako. Magufuli na Lowasa ni wanadamu na wana mapungufu yao kama wanadamu, cha msingi kuzingatia ni sera na mifumo waliyokuwa wanainadi.

Mathalani Lowasa alizungumzia katiba mpya ya wananchi ambayo ingetengeneza mfumo mpya na wenye ufanisi kwa vizazi vijavyo hata kama yeye hayupo duniani. Kwa katiba ile hata kama CCM ikikaa madarakani itakuwa na ufanisi mkubwa. Kinachotuponza mpaka tunashindwa kupiga hatua ni katiba hii mbovu ambayo imezalisha mfumo wa rushwa, usiri wa serikali na chama kuendesha vyombo vya dola kwa faida yao.

Wakati ambapo Lowasa alikuwa anaongelea mikakati ya kitaifa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo, Magufuli alikuwa anaongelea kujenga barabara, mambo ya kiutendaji zaidi ambayo ukiwa na katiba bora barabara zitajengwa tena kwa ufanisi mkubwa.
Hapo ndipo utakapogundua kuwa kuna tatizo kubwa sana la jinsi ya kufikiri kwa watanzania.

Huwezi kutekeleza sera nzuri wakati msimamizi wa hizo sera ni mbovu na hafai. Lowassa si msimamizi sahihi wa sera. Kama hata suala la ufisadi tu alishindwa kujibu atawezaje kusimamia sera zinazoziba rushwa na mianya yake?
 
Swali hapa ni watu wenye upeo upi, si watu tu.

Unaweza kuwabatiza upeo wowote unaoona unawafaa lakini ukweli ni kwamba hao ndio wapiga kura na wamefanya maamuzi sahihi. Lowassa si mtu sahihi wa kupewa nchi. Rais ameshapatikana na ameshakabidhiwa madaraka.
 
Hana budi kubadili na washauri wot. Itasaidia kuondoa vi- elments vya awamu iliyopita!!!
 
Alikuwa na cheo ikoiko baada ya mzee wa tumbili kuangushwa yeye ndie aliekuwa Attoney General.

Naona magufuli kaanza vibaya, huyu masaju alionesha udhaifu mkubwa bungeni katika sheria za makosa ya mitandao na gesi na mafuta, alipelekeshwa na akina Tundu Lissu na wote tunakumbuka aliwai admit mbele ya lissu baada ya ku hustle sana kuwa mimi si mtaalam sana wa ku draft sheria ila kwa kuhisi tu najua hapa umepatia au la! Ha ha

Magufuli kaanza na huyohuyo mteuliwa wa awali wa kikwete kwa nafasi iyoiyo. I can start sensing a dark future,
Hardly had I known comes after....
 
Watanzania bwana yaani vitu vidogo kama hivi unashindwa kuvijua sasa ulitegemea mabadiliko yapi...

Suala la Tindu Lissu kumzidi hoja mwanasheria mkuu halina uzito kiasi hicho maana nyinyi ndio mliamua kwamba kamzidi yeye alikuwa wanafanya Kazi yake, kitu ambacho pia mnashindwa kujua ni matumizi ya lugha ya kiswahili Tindu lisu anaongea kiswahili kama chiriku tofauti na Masaju ambaye kiswahili chake kizito ambapo yeye anamaneno 2 mwenzake anamaneno 20 sasa nyie Ukawa kwa upashukuna wenu mnaona amemshinda
 
Back
Top Bottom