Rais Magufuli amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kupendekeza jina la PM Nov 19

Rais Magufuli amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kupendekeza jina la PM Nov 19

Mijitu mingine shida. Mumuache Mh Rais afanye kazi yake. Acha ateue anaoona wanafaa kumsaidia yeye kufanya kazi zake kwa muhibu wa katiba na sheria za nchi. Kwa sababu tu mabadiliko feki yamepigwa chini basi kila atakalofanya Rais mpya lazima mijitu hii itapinga itapinga itapinga. Hata akianza ujenzi wa flyover lazima itasema tu aah mbona amechelewa mbona hivi mbona vile. Kama hupendi kale malimao.
 
Kwa nukuu za Katabazi alizozibatiza 'kimolo moyo' sasa sina shaka tena kwamba huyu Masaju hafai kabisa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Tetezi zake katika kesi zote ni zuio la kujadiliwa hoja mbele za mahakama, vigezo ambavyo vinaonekana havikuzingatiwa. Nilidhani kama mwanasheria mkuu wa serikali ni sehemu pia ya kuona nchi inabaki salama katika mawimbi ya mabadiliko. Na hii inamaanisha kweli vipengele vya sheria vinaweza vikazuia mijadala muhimu ya maendeleo na hata yenye uhalali katika maisha ya serikali (legitimate rights not only of the governed but also the governor) na kwa ajili hio ni busara kuruhusa fursa zinazojitokeza haya yafanyike.

Sioni ni kwa namna gani Serikali au Taifa lilinufaike kwa Masaju kukomalia hivyo vipengele vya sheria kwa kesi ya mgombea huru au kwa ile kesi ya kutahadharisha matumizi ya matamko ya viongozi kama aliyotoa Pinda ambayo yanaweza kusababisha uonevu na kukosesha taifa amani. Hata lile la Kubenea- angalia gharama zote zile za kuendesha bunge la katiba na hakuna kilichopatikana bali ufa mkubwa katika taifa, tumejenga UKAWA na wasio UKAWA.

Zamani nilifundishwa kuwa kuna mahakama ya Kifalme na ya Kimalkia- kwamba kuna uwezekano ukahurumiwa kutokana na kosa ulilofanya kama utakuwa na usafi fulani mbele ya benchi la kimalkia lakini mbele ya kifalme kamwe! Masaju anapaswa aisadie serikali ijithibiti na ithibitiwe kwa ukadiri ili tu isije ikawa ni kutekeleza sheria kama zilivyo kwenye kitabu bali pia kuumbulia zinazotokana na hali halisia- kuwa legal sawa lakini pia uonekana legitimate kwa macho, masikio na mnuso wa sasa!

Magufuli umenoa! Umeanza vibaya! Hakuna haraka katika jambo nzuri! Tafuta ushauri!
 
Hii nafasi inatakiwa kuombwa inapigwa interview ya wazi ili mtu anapopatikana ionekane amepatikana kwa uwazi, tubadili sheria kama wakenya
 
Nilitegemea kuona sura mpya kwenye serikali inayoitwa ya awamu ya tano. Uteuzi wa mwanasheria mkuu ni mwanzo wa kuonyesha mapungufu.
 
Watu wamefikiri na wametumia busara zao ndio maana wakapata maamuzi sahihi kuwa Lowassa si mtu sahihi wa kumpa nchi.

Badala ya kuangalia sera ambazo ni long term wewe unaangalia mtu, hapo ndipo uliposhindwa kushirikisha ubongo wako. Magufuli na Lowasa ni wanadamu na wana mapungufu yao kama wanadamu, cha msingi kuzingatia ni sera na mifumo waliyokuwa wanainadi.

Mathalani Lowasa alizungumzia katiba mpya ya wananchi ambayo ingetengeneza mfumo mpya na wenye ufanisi kwa vizazi vijavyo hata kama yeye hayupo duniani. Kwa katiba ile hata kama CCM ikikaa madarakani itakuwa na ufanisi mkubwa. Kinachotuponza mpaka tunashindwa kupiga hatua ni katiba hii mbovu ambayo imezalisha mfumo wa rushwa, usiri wa serikali na chama kuendesha vyombo vya dola kwa faida yao.

Wakati ambapo Lowasa alikuwa anaongelea mikakati ya kitaifa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo, Magufuli alikuwa anaongelea kujenga barabara, mambo ya kiutendaji zaidi ambayo ukiwa na katiba bora barabara zitajengwa tena kwa ufanisi mkubwa.
Hapo ndipo utakapogundua kuwa kuna tatizo kubwa sana la jinsi ya kufikiri kwa watanzania.
 
Alikuwa na cheo ikoiko baada ya mzee wa tumbili kuangushwa yeye ndie aliekuwa Attoney General.

Naona magufuli kaanza vibaya, huyu masaju alionesha udhaifu mkubwa bungeni katika sheria za makosa ya mitandao na gesi na mafuta, alipelekeshwa na akina Tundu Lissu na wote tunakumbuka aliwai admit mbele ya lissu baada ya ku hustle sana kuwa mimi si mtaalam sana wa ku draft sheria ila kwa kuhisi tu najua hapa umepatia au la! Ha ha

Magufuli kaanza na huyohuyo mteuliwa wa awali wa kikwete kwa nafasi iyoiyo. I can start sensing a dark future, same CCM we used to see.

Tusubiri!

si Ndio wenyewe wanasema sisiem ileile....
 
Yangu wala haikuwa protest vote. So pamoja na uwezo mzuri wa mama kujieleza, bado uahalisia wa kushinda ulikuwa finyu zaidi.

My wish ilikuwa Pombe apate lakini bunge liwe UKAWA. Unfortunately haikuwa hivyo.

Kwa muda mrefu niliokuwa US, na kushuhudia na pia kushiriki kampeni za urais. Nilipata shida na EL kwakuwa sikupata kumsikia vyema akisema atalifanyia nini taifa letu, hata mahojiano aliyofanya ni yale ya bbc hayakuni impress given nafasi anayogombea. Kujieleza ni muhimu sana kwa nafasi ya urais. I believe people who wants to be president of Tanzania should be able to answer tough questions.

Bora Lowassa aliongea huyo Magufuli aliyekimbia BBC hahahaha
 
Mijitu mingine shida. Mumuache Mh Rais afanye kazi yake. Acha ateue anaoona wanafaa kumsaidia yeye kufanya kazi zake kwa muhibu wa katiba na sheria za nchi. Kwa sababu tu mabadiliko feki yamepigwa chini basi kila atakalofanya Rais mpya lazima mijitu hii itapinga itapinga itapinga. Hata akianza ujenzi wa flyover lazima itasema tu aah mbona amechelewa mbona hivi mbona vile. Kama hupendi kale malimao.
Fly overs kwa pesa ipi iliyobaki. Kama msaada sawa.
 
Mshauri mkuu ni yeye, haluna M4C hapa ya mahufuli, Mungu ibariki Tanzania, maana Watanxania wenyewe hatujitambui tunasubiri neema zako
 
Haya ndiyo mabadiliko ya CCM bana. Unabadili kijani unatia njano. Ahadi zote zilikuwa zaidi ya hewa. Watanzania nimesoma huu uzi ni dawa inaanza kutuingia taratibu. Mpaka mwaka huu uishe tutakuwa tumesoma namba zote. Uchaguzi ujao kila mmoja atakuwa barabarani na mkewe na watoto, hata babu na bibi hakuna atakaeenda nyumbani hadi kieleweke. Kama huamini soma huu uzi wote.

Juzi mdogo wangu kaenda Hospitali Mwananyamala na Dawa zikawa hazipo, alipouliza ni vipi dawa hakuna? Jamaa Drs wakamwambia ..."HAPA NI KAZI TU", kweli mpaka 2020 tutakuwa tumeipata
 
Wakati nikiwa secondary kipindi cha UMISETA kulikua na mashindano ya awali ya kutafuta wanamichezo wachache watakao wakilisha shule ama mkoa kwenye mashindano hayo. Basi kati ya michezo iliyokua inafurahisha ilikua riadha ambapo baadhi walikua wanaanza kukimbia kwa kasi mno na watazamaji wanawashangilia mno. Jamaa walikua wanaacha gap kubwa sana kiasi cha kutaka kuwazunguka wenzao waliobaki nyuma lakini cha ajabu unaanza kuona jamaa wanaanza kuzingua...taratibu unaona jamaa wanaanza kukaa chini hawawezi tena kukimbia japo walianza kwa kasi kubwa na bado wamewaacha wenzao mbali..

Jana JPM kaapishwa na bila kuchelewa akateua mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ni wazi alishapwaya... kasi aliyoanza nayo ni ya kukimbiza upepo kama wakimbia riadha ambao mbio zao wenyewe ndio zinazowachosha na kuwakalisha chini.. Sio mbaya lakini wanakua wameshangiliwa vya kutosha japo wanaoshinda ni wengine.....
JPM inawezekana anakimbia vizuri....lakini nje ya mstari
 
Inaonyesha anaongozwa kwa remote, vile vile ni kama ana ka-inferiority complex Fulani toka kwa mtangulizi wake, asipoondoka nacho kitamghalimu.
 
Back
Top Bottom