Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Tunakunywa Pombe,Tukilewa tunatafuta SULUHU,Tukipata Majaliwa tunarudi Kupiga Job.
 
mie ndiyo namsikia leo hata sijui ni mbunge wa wapi,,,,,ngoja nigoogle takuja
 
Hongera sana Mh Kassim Majaliwa Allah amekujaalia kuwa waziri Mkuu.

Lowasa pole sana.
 
M?fisadi chali tena tumeweza tumethubutu na sasa tunasonga mbele.
 

Kama hivyo ndy vigezo basi tuna sfari ndefu ya kuiona kaanani
 

Ndugu yangu usipoteze muda wako kusifia huu uozo, hapo hakuna jipya anafanyia kazi maelekezo ya Msoga!! Ningemwona hatabiriki kama angemwibua mtu kama Livingstone Lusinde, Steven Ngonyani, Jah People (ha ha ha haaa utani mkuu). Sasa hapa katumia ushauri wa Msoga ili kuwapoza na maumivu ya kuukosa urais kama walivyokuwa wamejipangia (mama Salma huyo). Gufuli naye afanye kwa kujitegemea bwana, hiyo nafasi ajue kabisa hakuipata kwa hisani ya watu wa Msoga (vinginevyo atatufanya tuamini kwamba alikuwa amepigwa kwenye sanduku la kura, akabebwa na Msoga - ingawa kuna kachembe ka ukweli).
 
Kweli tumepata pm mchapa kazi sasa kazi tu twende pamoja sasa.
 
Bora bhana najivunia kuzaa sasa hivi ila utuletee tu umeme pale kijijini kwetu na rami kutoka Nanganga mpaka Ruangwa sio kutuwekea rami mita 100 kutoka hospital mpaka sokoni.
 
Jamani mwenye CV ya Mheshimiwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya 5 wa Serikalai ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hebu atusaidie hapa, maana hili jina sio famous sana miongoni mwa masikio ya watanzania.

Tunamtakia Mhe. Kila la kheri
 
Lowasa angekua Rais ungeshangaa Waziri Mkuu angekuwa Fisadi mwenzake Freeman DJ Mbowe a.k.a Mkwe wa --------- Mtei...

Kwi kwi kwiii...

Ukawa Bange sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…