Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Tunakunywa Pombe,Tukilewa tunatafuta SULUHU,Tukipata Majaliwa tunarudi Kupiga Job.
 
mie ndiyo namsikia leo hata sijui ni mbunge wa wapi,,,,,ngoja nigoogle takuja
 
Hongera sana Mh Kassim Majaliwa Allah amekujaalia kuwa waziri Mkuu.

Lowasa pole sana.
 
attachment.php
 

Attachments

  • kassim.jpg
    kassim.jpg
    17 KB · Views: 822
M?fisadi chali tena tumeweza tumethubutu na sasa tunasonga mbele.
 
MTAJIBEBA NA MBEREKO!!!! Hii ndio CCM chama cha Kitaifa..... Team inapangwa kwa kuzingatia Uwezo, Matabaka, Kanda, na Jinsia...... Rais - Kanda ya Ziwa (Mwanaume)..... Makamu - Zanzibar (Mwanamke)....Speaker....kanda ya kati (Mwanaumeme) ......Naibu Speaker Nyanda za juu kusini (Mwanamke)...... Waziri Mkuu ....Kusini Pwani (Mwanaume)...... CCM ni Raha tupu.....purely Scientific........ Walee jamaa Zetu Wanazidi kupagawa!!!

Kama hivyo ndy vigezo basi tuna sfari ndefu ya kuiona kaanani
 
Katika kazi ya kuteuwa Waziri Mkuu umefanywa kwa weredi nimeona binafsi kuwa Kassim Majaliwa ni bora kuliko wale tuliowazoea maana Bora Panya mpya kuliko panya wa Ghalani" Maana panya wa ghalani kumfukuza ni kazi na usipokuwa makini unaweza kuangukiwa na magunia!ila panya mpya ni bora si muharibifu kama mwenyeji!Naona sasa ile dhana ya kuwa na viongozi tulio wazoea inaanza kupotea,hapa naanza kuona hata mawaziri wanaweza kuwa wapya!
Hii inaweza kurudisha imani katika chama cha mapainduzi.

Ndugu yangu usipoteze muda wako kusifia huu uozo, hapo hakuna jipya anafanyia kazi maelekezo ya Msoga!! Ningemwona hatabiriki kama angemwibua mtu kama Livingstone Lusinde, Steven Ngonyani, Jah People (ha ha ha haaa utani mkuu). Sasa hapa katumia ushauri wa Msoga ili kuwapoza na maumivu ya kuukosa urais kama walivyokuwa wamejipangia (mama Salma huyo). Gufuli naye afanye kwa kujitegemea bwana, hiyo nafasi ajue kabisa hakuipata kwa hisani ya watu wa Msoga (vinginevyo atatufanya tuamini kwamba alikuwa amepigwa kwenye sanduku la kura, akabebwa na Msoga - ingawa kuna kachembe ka ukweli).
 
Kweli tumepata pm mchapa kazi sasa kazi tu twende pamoja sasa.
 
Bora bhana najivunia kuzaa sasa hivi ila utuletee tu umeme pale kijijini kwetu na rami kutoka Nanganga mpaka Ruangwa sio kutuwekea rami mita 100 kutoka hospital mpaka sokoni.
 
Jamani mwenye CV ya Mheshimiwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya 5 wa Serikalai ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hebu atusaidie hapa, maana hili jina sio famous sana miongoni mwa masikio ya watanzania.

Tunamtakia Mhe. Kila la kheri
 
Lowasa angekua Rais ungeshangaa Waziri Mkuu angekuwa Fisadi mwenzake Freeman DJ Mbowe a.k.a Mkwe wa --------- Mtei...

Kwi kwi kwiii...

Ukawa Bange sana.
 
Back
Top Bottom