Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Sawa ni uteuzi mzuri lakni akishaanza kuharibu mnajifanya kama sio nyie mliokuwa mnamsifia
Kiongozi, mtu yoyote akiboronga lazima asemwe. Hujui kuna watu kazi yao ni kuhoji, kupinga, kukataa...hatuwezi kufanana. Critics ni muhimu kwa ustawi wa nchi.
Hata Mh. Raisi akiboronga lazima asemwe..
 
Kwa mara ingine ccm imedhirisha inaongozwa na nguvu za giza! wadau mtakuwa mnakumbuka kwenye kampeni za mwaka 2010 shehe yahaya aliwahi sema kuwa atamuongezea nguvu ya ulinzi baada ya baba riz kuanguka jangwani. leo tena magufuli anatuletea mzee wa matambiko!

pole,nchi hii ni ya wote
 
Ni mda sahihi sasa kwa watanzania kupigania katibu mpya, hiki cheo cha waziri mkuu kina maana gani kama kuna makamu wa rais?? Kwanini makamu wa rais asifanye kazi za waziri mkuu au awepo waziri mkuu tuu?? Hizi nchi ndogo ndo zina vyeo vya ajabu sana.
Rais akisafiri/ akifariki ni nani atafanya shughuli za serikali bungeni ma shughuli zingine za waziri mkuu?
 
Pongezi Mh Kasim Majaliwa Kwa Nafasi Hii Mungu Awapeni Nguvu
 
Kwa kweli ni mara yangu ya kwanza kumsikia yeye mwenyewe pamoja na jimbo lake.

Hilo jimbo la Ruangwa lipo mkoa gani!!?
 
Sura za zamani zikitoweka kwenye baraka la mawaziri.........Imani yangu na serikali inaweza kurudi...........

Tuombe Mola tupate baraza zuri la mawaziri.
Ila huyu Bwana aliyechaguliwa sasa kuwa PM nadhani
watu kama hawana mazoea nae ya kumpa michongo ya dili.
 
tuambieee saa ngapi tunarejea!! mm pia hata kibaruani ndo sijafika nasubiri speech ya PM nitoa mtazamo wangu ni mtu wa aina gani!!!
 
Muda mfupi tu uliopita Spika wa bunge kwa mamlaka aliyopewa na Bunge na Rais wa Jamhuri wa Muungano, amemtangaza Ndugu Kassimu Majaliwa kuwa ni Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano ya Dk.John Pombe Magufuli.

Je, ulikuwa unalijua hili?
Tupate historia fupi ya Waziri Mkuu mteule:-
-
Majaliwa alikuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa serikali ya awamu nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
-
Siyo jina kubwa kwenye medani ya siasa na aliingia katika medani hiyo mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Ruangwa na kuteuliwa kushika wadhifa huo serikalini na kudumu nao hadi Rais Kikwete alipong?atuka.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya duru za serikali zinasema Rais Magufuli anataka kuteua mtu mpya atakayetekeleza kauli mbiu yake ya `Hapa kazi tu?.
-
-Je , kumbukumbu yetu inasemaje juu ya history ya Mawaziri Wakuu walipita mpaka leo hii:-
-
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Rais Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, watu wengi walitabiri kwa usahihi kuwa angemteua Edward Lowassa, kuwa Waziri Mkuu.-
-
Na hicho ndicho kilichotokea, kwani siku chache baadaye, jina la Lowassa liliwasilishwa bungeni na mwishowe akapitishwa na wabunge kwa kishindo kuwa Waziri Mkuu.
-
Kadhalika, inaelezwa vilevile kuwa hata baada ya Lowassa kujiuzulu kufuatia sakata la mitambo ya kufua umeme ya Richmond, wengi walitabiri kuwa Mizengo Pinda, angeteuliwa na Rais Kikwete kuwa Waziri Mkuu. Na ndivyo ilivyokuwa.
-
Hata hivyo, Nipashe imebaini kuwa hivi sasa tetesi kuhusiana na jina la Waziri Mkuu wa Serikali ya Dk. Magufuli, ziko tofauti sana kulinganisha na vile ilivyokuwa katika uteuzi wa Lowassa ambaye sasa yuko Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Pinda.
-
Na mpaka leo hii kuteuliwa, je tunaweza kumuelewa Waziri Mkuu?

Majaliwa anaaminika kuwa ameonekana kuwa ana uwezo wa kuendana na kasi aliyoanza nayo Rais Magufuli katika kuhakikisha kuwa ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni zinatimizwa.
-
Hivyo ni Chaguo sahihi , kuendana na haya?


Kwanza, ni kitendo chake cha kushika wadhifa wa Naibu Waziri kwenye ofisi ya Waziri Mkuu kwa miaka mitano, kumemfanya kuvuna uzoefu wa kufanya shughuli za taasisi hiyo na kukidhi vigezo vya kuaminiwa kupewa nafasi hiyo.
-
Pia ukizingatia kuwa Majaliwa ndiye aliyekuwa na jukumu la kusimamia masuala ya elimu kwenye Tamisemi, ambayo ni miongoni mwa ahadi kubwa za Rais Magufuli.
-
Ikumbukwe kuna suala la utekelezaji wa ahadi ya elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Kutokana na uzoefu wake wa kuongoza masuala ya elimu kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, kunamwongezea sifa ya kushika nafasi hiyo.
-
Kutokana na ukweli kuwa sifa mojawapo ya Waziri Mkuu anatakiwa kuwa mtu ambaye anaujua mfumo wa serikali, ndiyo maana kunafanya jina la Majaliwa kutajwa kushika nafasi hiyo.
-
Hali ilivyo sasa kwa Mh.Majaliwa!

Kuna taarifa zimedokeza kuwa familia yake yote kwa sasa iko mjini Dodoma huku kukiwa na ulinzi mkali kwenye nyumba ya serikali anayoishi eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
-
?Mheshimiwa na familia yake wamekwenda Dodoma tangu Jumapili iliyopita. Nyumbani kwake hakuna mtu kwa sasa,? alidokeza mmoja wa wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye hata hivyo, siyo msemaji wake rasmi.
-
Mmoja aliye karibu na Majaliwa, naye aliiambia Nipashe hajawasiliana na kwa njia ya simu na Majaliwa tangu Jumapili iliyopita.
-
?Unajua ninafahamiana na Mheshimiwa Majaliwa kwa miaka mingi. Huwa ninamsaidia shughuli zake nyingi. Siyo kawaida yake kutojibu simu. Hata kama hatapokea, basi ni mwepesi kupiga baadaye. Nadhani kuna kitu hapa. Nina wasiwasi. Ila yote kheri kama mambo yatamnyookea,? alidokeza rafiki yake wa karibu, ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.
-
Pia kutajwa kutokana na ukweli kuwa Majaliwa anatoka Mkoa wa Lindi ambao Kanda ya Kusini kunafanya awe na nafasi kubwa.
-
Kutokana na ukweli kuwa suala la jiografia huzingatiwa ingawa siyo la kikatiba, lakini uwezekano wa Waziri Mkuu kutoka Kanda ya Ziwa ni mdogo.
-
Na hizi ndio majina yaliyokuwa yakipambanishwa na Waziri Mkuu Mteule.

Wengine wanaopewa nafasi kubwa ya kupambanishwa ni kama ifuatavyo:-
-
Sifa hizo ni pamoja na mahali atokako ambako siyo Kanda za Magharibi, Ziwa wala Kaskazini.-
-
Sifa ya pili ya mtu huyo ni kutowahi kujitokeza katika mbio za kuwania urais ndani ya CCM; sifa yake ya tatu ni kwamba hajawahi kudhaniwa kushika nafasi hiyo na sifa ya nne amewahi kushikilia nafasi ya uwaziri/naibu waziri katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Kikwete iliyomaliza muda wake Novemba 5, mwaka huu.
-
Pamoja na Majaliwa, wengine wanaoangukia kwenye kundi hilo ni Mbunge wa Peramiho aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama, Mbunge wa Kibakwe aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene na Mbunge wa Bagamoyo aliyekuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
-
Wengine waliomo katika orodha hiyo ya wabunge saba wanaotajwa kuwa wanaweza kupewa nafasi hiyo ni Mbunge wa Newala, Kapteni George Mkuchika, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia na pia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Juma Nkamia.
-
Majina mengine yanayotajwa-
Pamoja nao hao, wengine ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa tajwa ni William Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; aliyekuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba; Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu; aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na pia aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro

Nawasilisha.
 
kweli kwa uteuzi huu nimeamin hapa kazi itakuwepo...Tunataka kiongozi ambaye ataendana na kasi ...hii ...

alisaidiaje taifa akiwa naibu waziri wa elimu TAMISEMI?
shule zetu alzifanyia nini? madeni ya walimu katika halimashauri aliyashughulikia vipi? je hiyo kazi ya magufuri ataiweza kama ni kazi kweli?
 
nakupongeza sana mh Rais kwa uteuzi wako kwa kumteua ndugu Kassimu Majariwa kuwa Waziri Mkuu wa JMT wa kumi tangu Nchi yetu ijitawale yenyewe, hakika watanzania tutampa ushirikiano makini ili kuleta maendeleo ya watu na pia nategemea atakuwa msomaji mzuri wa hotuba ya Mwalimu Nyerere ya mwaka 1968. June 8 " Uhuru na Maendeleo ya watu" kwani jicho ndicho kiini cha mabadiliko tunayolilia leo, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Back
Top Bottom