Sioni kama hiyo ni huruma, serikali ilikua imelala mpaka ikaajiri wafanyakazi wenye vyeti feki? Huoni kama makosa ni ya serikali na serikali ilitakiwa iwajibike kwa uzembe na sio hao wafanyakazi
Mtu yupo kwenye ajira zaidi ya miaka ishirini au 30 leo unakuja kumwambia kwamba ana vyeti feki, unamwachisha kazi, ana familia na wategemezi, mbaya zaidi yupo katika age ya kustaafu
Kama Magufuli na washauri wake wangekua makini, wangeweka mkakati wa kuwaendeleza wale wafanyakazi ambao hawakua na vyeti kwa sababu tayari wana uzoefu mkubwa kazini na pengine wanafanya kazi vizuri kuliko hata wenye vyeti halali, na kwa wale ambao walifika umri wa kukaribia kustaafu wangewaacha wamalize muda wao.