Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Mbona viongozi wengi tu duniani wanaondoka madarakani kikomo cha uongozi wao unapofika
 

Mkuu mimi siamini hao viongozi waliotoka ccm kupewa nafasi ndani ya cdm. Sijui ni kwanini unaniletea Mbowe V/s hao watoka ccm. Hata hivyo kama kweli cdm haikupaswa kumpa mwanaccm nafasi ya uenyekiti huyo Mwambe au Sumaye, mbona walimpa Lowasa nafasi kubwa kuliko ya uenyekiti wa chama na wala hukuhoji?

Hiyo paragraph yako ya mwisho naona ni mjadala mwingine. Ukiuweka hapa tutakuwa tumechanganya mambo mengi. Ila siwakatazi cdm kushiriki uchaguzi huo, lakini mimi na wale ninaweza kuwashawishi kutokupiga kura bila tume huru ya uchaguzi, hata maamuzi tumeshachukua.
 
Ananipamia akidhani mimi ni mwepesi wa hivyo. Hebu akuulize ww maana huwa unaipata fresh shughuli yangu kwenye huo upande wenu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 

Hizi sifa za kijinga ulizomwaga hapa kama ccm wangekuwa nazo, nchi hii isingekuwa moja ya nchi masikini duniani.
 
Hizi sifa za kijinga ulizomwaga hapa kama ccm wangekuwa nazo, nchi hii isingekuwa moja ya nchi masikini duniani.
Kama Upinzani haujaamua kuingia kwenye siasa za kweli, siasa za hoja na ushawishi, hakuna Chama kitakachoitoa CCM miaka Elfu ijayo

Sasa ninyi endeleeni kuombea yasiyowezekana
 
Kama Upinzani haujaamua kuingia kwenye siasa za kweli, siasa za hoja na ushawishi, hakuna Chama kitakachoitoa CCM miaka Elfu ijayo

Sasa ninyi endeleeni kuombea yasiyowezekana

Hiki unachosema kinaendana na zile sifa za kijinga ulizomwaga mwanzo?
 
Wewe ungeshauri Dr Slaa angefanyaje kipindi kile chadema kinampitisha Lowasa
 
Una mitazamo mizuri sana.
 
Hahaaa kumbe unawafuasi wako ndani ya CDM! navyojua kususa sio tabia ya kiume.

Halafu kumbe na Zitto nae alitoka CCM!.
 
Angekaa kimya kama Mnyika.
Kukaa kimya ni kukubaliana yanayoendelea , yeye hakukubaliana na mchakato kwahiyo hakuona haja ya kukaa kimya ukiangalia na nafasi aliyokuwa nayo ilikuwa vigumu sana kukaa kimya, hata wewe mwenyewe usingeweza kukaa kimya kuona ulichokijenga kwa muda mrefu kinaenda tofauti na misingi uliyoijengea
 
Basi tuondoe mfumo wa vyama vingi maana CCM wanauzoefu
 
Kumbe na Zitto nae alitoka CCM!.

Zito ni case tofauti, na wakati huo muda wa madarakani wa Mbowe ndani ya hiyo nafasi ulikuwa unakubalika. Boss naona shida yako unasaka ushindi kwenye huu mjadala, ndio maana unaishia kuchomekea kila kinachokujia kichwani. Pitia post zangu wakati wa mgogoro wa Zito, uone kama niliwahi kusema muda wa Mbowe kuwa mwenyekiti umetosha na ampishe Zito. Kama unasaka ushindi, mimi siko kwenye hiyo league, ninaelezea ninachokiamini. Najua vizuri kuwa nimekukwaza, na sio ww tu, na wengine pia. Ila huna jinsi zaidi ya kuvumilia mawazo mbadala, hii ni kwa afya ya cdm kama taasisi.
 

Sawa boss, hata hivyo ninamuheshimu Slaa hasa mchango wake ndani ya cdm, na pia niliheshimu msimamo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…